Ushauri:Kuoa mwanamke mwenye mtoto

Ushauri:Kuoa mwanamke mwenye mtoto

ACHA IYO MANENO MBOF MBOF KAKA,mapenz hapo ivo et nioe kisa hana mtto,vp kama sijampenda??ndoa n upendo kwanza umpende dem ,sasa uyu msela kampenda dem mwenye mmto,haikataliw ,kina cho msumbua jamaa ni wvu tu,bt km mwanamke ni Smart enough hawez fanya lolote na uyo babà watto wake,suala apo ni jamaa kujua dem wake ANA akil gan na upeo wake maana madem wa sku iz chup mkonon akil zpo matakon,na ishu ya mtto kwenda kule its ok ndo kwao kwan ww sio babà ake na hata ukimsomesha jua atasaidia kwao ww ztabaki shukran tu mbele ya mungu,ishu apa ni dem wako aheshimu feelings zako kua hupend awe karbu na kule paspo na kifo au maradh,na km dem ana akil bas atakusoma vema,ww n mmoja ktk wanaume bab,sio wote wanaweza fanya ivo kama kwel hujawai taliki(talaka) au hujawai oa yan ndo ndoa yako ya mwanzo bas you r the best among the best ,msitiri uyo dada na Allah atawafanya ndoa yenu iwe n yenye baraka nying fi dunia wal akhera
Katika watu wenye busara wewe unabusara sana.
 
Mkuu mlezi (kama jamaa atamlea mtoto) ana nafasi kubwa pia katika maisha ya mtoto maybe kuliko hata biological father (kama huyo mzazi hatatoa malezi).
Mkuu hujui mtoto wa mtu wewe,
Wapo wanaume wengi walilea watoto ambao Baba zao walifariki ila baadae watoto waligeuka na kuwa kivyao na kuto kujali huyo Baba mlezi.
Kumbuka huyo mtoto Baba yake yupo hai.
 
Kwahio mkuu yaani wewe umeona ni tatizo sana kwa mtu kupewa damu na mtaliki / ex wake ? Pia katika matatizo yote wewe unaona la kukaa high table siku ya harusi ni issue ya maana ?

Mkuu mlezi (kama jamaa atamlea mtoto) ana nafasi kubwa pia katika maisha ya mtoto maybe kuliko hata biological father (kama huyo mzazi hatatoa malezi).
Mkuu tafiti zinaonyesha wanaume wengi wanajuta ambao walio wanawake wenye watoto.

Take this unalea mtoto toka mdogo hadi kuwa mkubwa afu akiwa mkubwa anarudi kwa Baba yakena kwako haji tena , ikitokea hivyo utachukua uamuzi gani??????

Pili ukimlea mtoto mpaka kuja kufanikiwa huko ukubwani afu wewe ukagombana na mama yake tena kwa ugomvi mkubwa mkaachana unafikili atarudi huyo mtoto kwako???
 
Mkuu hujui mtoto wa mtu wewe,
Hakuna mtoto asiye wa mtu; pili cha maana zaidi ni nini (sperm donation) au malezi kuhakikisha kwamba huyo mtoto anapata malezi na kuwa mwanajamii bora
Wapo wanaume wengi walilea watoto ambao Baba zao walifariki ila baadae watoto waligeuka na kuwa kivyao na kuto kujali huyo Baba mlezi.
Wewe unasaidia mtu / mtoto ili akujali ? Au unatenda wema unakwenda zako unafanya jema sio ili urudishiwe unafanya jema sababu ni right thing to do..., kutokujali mtu au mlezi sio sababu sio mtoto wako bali ni mtu mwenyewe after all wangapi hawajali wazazi wao waliowazaa au ni wazazi wangapi kwa ukorofi wao wanasababisha uwepo wa umbali ?
Kumbuka huyo mtoto Baba yake yupo hai.
Sisemi mtu aoe mke mwenye mtoto lakini sijasema asioe pia ? Huo ni uchaguzi binafsi sababu kuna changamoto zake, na kama mtu una sita acha kufanya hivyo sababu kuna three parts kwenye hii equation wewe, yeye na mtoto..., kwahio unahitaji kuwa na busara ya hali ya juu ama sivyo unaweza ukasababisha madhara zaidi (kama huwezi usifanye) ila kama umeyavulia nguo sio kweli kwamba hayawezi kuogeka..., na kama mtoto huyo ana busara na akili atakushuru maisha yake yote (sababu ulichofanya hakikuwa obligation ila ulifanya despite yeye sio damu yako)
 
Mkiambiwa hamtaki kusikia , ni hivi narudia tena Kuoa mwanamke mwenye mtoto hakuna tofauti na kuoa single maza..

sasa wewe endelea kukaza fuvu shauri yako kijana..
 
Hakuna mtoto asiye wa mtu; pili cha maana zaidi ni nini (sperm donation) au malezi kuhakikisha kwamba huyo mtoto anapata malezi na kuwa mwanajamii bora
Ingekuwa hivyo jamii yote duniani kungekuwa na ushirikiano na ndugu
 
Wewe unasaidia mtu / mtoto ili akujali ? Au unatenda wema unakwenda zako unafanya jema sio ili urudishiwe unafanya jema sababu ni right thing to do..., kutokujali mtu au mlezi sio sababu sio mtoto wako bali ni mtu mwenyewe after all wangapi hawajali wazazi wao waliowazaa au ni wazazi wangapi kwa ukorofi wao wanasababisha uwepo wa umbali ?
Take this unasema unalea utaki chochote kile. Usiwe mnafiki
Hivi wewe unamtoto wako wa kumzaa unamlea unamsomesha kwa ghalama zote ,
Then baadae anakuja kuwa na mafanikio mazuri tuu tena makubwa. Lakn wewe mzazi upo chini tena chini si unajua maisha ya uzeeni.
Sasa utasema mwanao akuache tuu hivi kisa ushamaliza kazi.
Kuwa mkweli tuu.
 
Wewe unasaidia mtu / mtoto ili akujali ? Au unatenda wema unakwenda zako unafanya jema sio ili urudishiwe unafanya jema sababu ni right thing to do..., kutokujali mtu au mlezi sio sababu sio mtoto wako bali ni mtu mwenyewe after all wangapi hawajali wazazi wao waliowazaa au ni wazazi wangapi kwa ukorofi wao wanasababisha uwepo wa umbali ?
Take this.
Mfano umemkuta mkeo yupo na mtoto ana miaka 3 Baba yake alimtelekeza kabisa hana mpango nae. Wewe unachukua majukumu kama Baba unalea mtoto, na malezi sio pesa tuu ndio utaweka Bima yako, ada , chakula , mavazi.
Lakn pia kuna issue ya kumlea mtoto kwa tabia njema kabisa.
Ukazaa na watoto wako let say 3.
Lakn yule wa mkeo akaja kuwa mkubwa mpaka kumaliza chuo.
Gafla ukagombana na mama yake ambae ni mkeo mkagombana tena kwa ugomvi mkubwa na kutengana kabisa, huyo mtoto akawa mtu mwenye mafanikio mkubwa katika maisha.
Wewe unafikili atakuja kwako huyo mtoto????

Na tena ukute watoto wako ni watu wa kuangaika tuu na maisha hawana mbele wala nyuma lakn wana kaka yao au dada yao mkubwa na mafanikio. Tena utakuta mwingine anaamua kumtafuta Baba yake na kumpata na unaona kafanana naye kabisa akaamua kumsamehe Baba yake mzazi na kuwa karibu nae.
Wewe utajisikiaje kwa kitu kama hicho kuwa mkweli usifiche mkuu.
 
Yaani ugombane na mama yake tena ugomvi mkubwa na huenda umemuonea mama yake alafu aje kwako ili iweje ? Kumbuka na yeye ni Binadamu na ana mapungufu...

Lakini kama mama yake ndio mkorofi na yeye hilo ameliona nadhani hata akijifanya anakuchukia kwenye conscious yake itakuwa vinginevyo, lazima atakuwa anajua wema uliomtendea

Vaa viatu vya huyo mtoto wewe kama hata baba yako mzazi alikutendea mabaya siku ukimuona hana mbele wala nyuma utamkomoa au utamsaidia (don't kick a dying man); pili haimaanishi nikimpenda mlezi nimtelekeze mzazi ; what's wrong kwa kuwapa nafasi wote..., wewe utapata faida gani akimchukia baba yake mzazi (ndio inamaanisha kwamba atakupenda sana wewe)?
 
Mkuu mbona unakwepa jibu ulichoulizwa
 
Unaongea coz hayaja kukuta😃😃😃
Wapo wanaume yamewakuta hivyo na wanajuta kuwa nao hao watoto.
Kuna uzi mmja humu kuna mtu mzima aliwahi toa kisa chake cha kulea watoto wa mkewe wake wawili aliyowakuta nao wakiwa na 5 year mwingine 2 years.
Mwishoni wakasepa zao Na baba yao alishafariki tangu siku nyingi.
Akiongea na mama yao anasema yeye ajui kwa nini wamekuwa hivyo
 
Hata angalia kwa diamond platinum kuhusu mzee Abdul.
Kuna kingine kuhusu serena wa USA.
 
Yaani ugombane na mama yake tena ugomvi mkubwa na huenda umemuonea mama yake alafu aje kwako ili iweje ?
Kwani wanaogombana na wake zao ishu ni mwanaume ndio chanzo.
Bro asilimia kubwa ya wanawake watoto wao wakija kufanikiwa wanakuwa na viburi sana.
Unajua hilo.
 
Cha kunitia wasiwasi ni ukaribu uliopo kati yake na familia ya huyo baba mwenye mtoto,yani wako karibu kiasi kwamba mtoto anaenda kulala huko.
Ohoo! Ushapigwa hapo. Subiri kumfumania manzi wako akiwa kwenye staili ya mbuzi kagoma kwenda

Waliozaa kamwe hawaachani.
 
Mkuu mbona unakwepa jibu ulichoulizwa
Ndicho hicho nilichokujibu Binafsi nafanya mambo sio ili baadae nipewe shukrani au nikumbukwe au nirudishiwe fadhila; Nafanya jambo jema sababu ni right thing to do at the time....

Kwahio kama umependa Boga basi ni lazima upende na ua lake..., na wakati bado huyu mtoto ni kinda utatimiza wajibu wako kama mlezi..., hayo baadae huyu mtoto akileta ukorofi ni yeye wala sio wewe, na wala haitakupunguzia wema uliotenda....

Ukiangalia kwa marefu na mapana hii Dunia ni ya kupita ishi na furahia leo sio ujinyime furaha ya leo kwa hofu ya shida zinawezoweza kukupata au kutokukupata kesho...
 
Baadae ntaambiwa sjtambui kwa kumkataza kwenda kumuona mzaz mwenzake. Ishu ilyopo ni kwamba jamaa kashasema kumuoa haipo kwa sababu ilikuwa one nightstand,yan nn sasa kujpeleka kwao ili hal jamaa ashamkataa na haeleweki? If she let the man go even the relatives,yan nn wakat kashakukataa kwamba mind your own business,unamwambia mtoto nenda kalale huko. Ntajkocommt only if hamna ukarbu nnao uona sasa.Nshamwambia kama wana ukarbu huo amuombe huyo jamaa amuoe,ila sio mim.
Una utoto mwingi kwaio unamtishia kumuoa,?huyo mtoto hata ufanye nini hatakaa awe damu yako pambana tafuta mke wa ujana wako,achana na wake za ujana wa watu
 
Ndicho hicho nilichokujibu Binafsi nafanya mambo sio ili baadae nipewe shukrani au nikumbukwe au nirudishiwe fadhila; Nafanya jambo jema sababu ni right thing to do at the time....

Kwahio kama umependa Boga basi ni lazima upende na ua lake..., na wakati bado huyu mtoto ni kinda utatimiza wajibu wako kama mlezi..., hayo baadae huyu mtoto akileta ukorofi ni yeye wala sio wewe, na wala haitakupunguzia wema uliotenda....

Ukiangalia kwa marefu na mapana hii Dunia ni ya kupita ishi na furahia leo sio ujinyime furaha ya leo kwa hofu ya shida zinawezoweza kukupata au kutokukupata kesho...
Ni mtazamo wako binafsi wapo wengi yamewakuta na wanajutia kwa maamuzi walioyafanya.
Binafsi nikiona mwanamke mwenye mtoto huyo mtoto anihusu kwa lolote lile.
 
We muoe kama unampenda bwana, sasa mtoto asisalimie kwao 😀
 
Back
Top Bottom