Ushauri:Kuoa mwanamke mwenye mtoto

Ushauri:Kuoa mwanamke mwenye mtoto

Jamani na mimi nisaidieni ushauri nataka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto halafu tuko kwenye mahusiano kwa miaka mitatu ila yy yuko mkoa mwingine na mimi mwingine, huwa anampigia huyo mama wa mtoto anamleta mtoto anamuacha kwa baba yake au anamtuma msichana wa kazi amlete. Hiki kitu kinaniuma sana kwani kila w.kend anakuwa na mwanae na akiwa nae hata ukimpigia cm hamsikilizani yuko busy na mwanae. Nishachoka kuvumilia ila tatizo tushapoteZeana muda miaka 3 na bado nampenda.
 
Mmh huyo bidada hana msimamo aisee. hapa cmaanishi mtoto asiende kwa babu/bibi bt ukaribu hautakiw kuwa kiivyo kama anachofanya. ndugu kuwa makin asije akabadilisha mawazo ukabaki ukisema ungejua ungejua
 
Hivi kijana mdogo kama wewe huwaoni mabinti wote wanaotoka vyuoni ambao wako fresh?

Hebu tazama kwa mfano huyo mama anaumwa na anahitaji damu na kwa bahati mbaya damu yako wataalam wanasema haimfai halafu anakuja mzazi mwenzake anapimwa damu wataalam wanaihafiki na anatolewa damu ili kumuokoa huyo unayemuona wewe ni mpya je baada ya kupona wewe utajisikiaje?

Na ukumbuke siku ya mtoto wao kuoa au kuolewa wao ndio watakaa high table kama Baba na Mama mzaa chema.

Mnatuchosha kila siku kuomba ushauri wa kijinga wakati mabinti kibao wanahitaji kuolewa.

mwenye mtoto na aolewe na mwanaume mwenye mtoto pia hapo ndio ngoma droo na siyo mvulana mzima na barehe zako unataka used.

Kwahio mkuu yaani wewe umeona ni tatizo sana kwa mtu kupewa damu na mtaliki / ex wake ? Pia katika matatizo yote wewe unaona la kukaa high table siku ya harusi ni issue ya maana ?

Mkuu mlezi (kama jamaa atamlea mtoto) ana nafasi kubwa pia katika maisha ya mtoto maybe kuliko hata biological father (kama huyo mzazi hatatoa malezi).

Anyway maisha ni chaguo la mtu na yeye anavyoona ila kama mtu ana mashaka basi asiwe-involved na single mother sababu busara au upumbavu wake utakuwa na effect kwa mtoto pia (kiumbe asiye na hatia wala kosa). Ila nadhani mawazo ya kwamba mama mwenye mtoto ni lazima kuolewa na baba mwenye mtoto hayana nafasi kwenye ulimwengu wa sasa.
 
Nna mahusiana na dada mmoja na nlitegemea awe mke wangu hapo baadae.Huyu dada ana mtoto na jamaa mwingine na alivyoniambia na kwamba hawana mahusiano tena na baba mwenye mtoto nkakubali ntamuoa.Cha kunitia wasiwasi ni ukarbu uliopo kati yake na familia ya huyo baba mwenye mtoto,yani wako karibu kiasi kwamba mtoto anaenda kulala huko.Huu ukarbu unanipa wasiwasi kama kweli waliachana au ni kunidanganya tu.Je baadae si utaleta shida kwenye familia yetu.Waungwana hebu naombeni ushauri wenu.

Katika maisha yako usije ukaoa mtalaka au mwenye mtoto unless awe amefiwa na huyo mzazi mwenzie. Kusema hivyo mimi nilishauriwa na wazee wangu nikakaidi wakati huo penzi limeshika hatamu, lakini baadae nilijionea mwenyewe. Mimi ninae mzazi mwenzangu pamoja na kuwa alishaolewa lakini mawasiliano yapo, hata yale mambo yetu kama kawaida tena kwa staili zote. ACHA.
 
suruhu mtoto aende kwa baba yake, maswala ya mtoto kwenda na kuludi kwa baba yake. ndio mwanzo wa mtoto kujifunza uongo
 
Katika maisha yako usije ukaoa mtalaka au mwenye mtoto unless awe amefiwa na huyo mzazi mwenzie. Kusema hivyo mimi nilishauriwa na wazee wangu nikakaidi wakati huo penzi limeshika hatamu, lakini baadae nilijionea mwenyewe. Mimi ninae mzazi mwenzangu pamoja na kuwa alishaolewa lakini mawasiliano yapo, hata yale mambo yetu kama kawaida tena kwa staili zote. ACHA.

Aksante mkuu kwa kunifungua upeo.
 
Kuwa na msimamo wewe mwenyewe juu ya mahusiano yako na yeye pia juu ya mtoto na familia ya baba mtoto.kama atakuwa tayari kubadilika basi oa!!!
 
kuoa mwanamke aliye na mtoto huna tofauti na kuishi na alishababu muda wowote mnatibuana chanzo mtoto
 
Sikushauri kuoa maana unamashaka na hiyo itakuletea shida sana maana utakuwa umeingia ktk mzigo usio kuhusu maana wivu utakuwepo na matokeo yake imani itakutoka lkn zaidi ya yote maamuzi unayo wewe nafsi inasemaje
 
Katika maisha yako usije ukaoa mtalaka au mwenye mtoto unless awe amefiwa na huyo mzazi mwenzie. Kusema hivyo mimi nilishauriwa na wazee wangu nikakaidi wakati huo penzi limeshika hatamu, lakini baadae nilijionea mwenyewe. Mimi ninae mzazi mwenzangu pamoja na kuwa alishaolewa lakini mawasiliano yapo, hata yale mambo yetu kama kawaida tena kwa staili zote. ACHA.[/QUOT] Hiyo hali siyo guarantee bwana....kama wew umepitia hayo siyo lazima naye apitie hayo...
 
Kuwa na msimamo wewe mwenyewe juu ya mahusiano yako na yeye pia juu ya mtoto na familia ya baba mtoto.kama atakuwa tayari kubadilika basi oa!!!

Unajua nashndwa hata nianzie wapi kwan mahusiano kati yake ni hyo familia ni stong,kesho ni shule,nmeulza kwa hyo mtoto hataenda shule,akaniambia eti huko kuna nguo zngne zko huko atabadili aende shule.Yan hata nguo za mtoto zngne zko kwa dada wa huyo baba mtoto(shangaz wa mtoto),znakaa huko sio kwamba anaenda nazo
 
Ok,huyu jamaa hajakataa mtoto.

mkuu hiv hakuna wanawake mtaani kwenu ambao hawajazaa?? Au hata kama vip nenda katafute kijijin kwenu katafute wanawake lakin sio kuoa mwanamke mwenye mtoto. Hapo unajipa stress na masononeko moyon mwako. Achana na waliozalishwa watakusumbua
 
Nna mahusiana na dada mmoja na nlitegemea awe mke wangu hapo baadae.Huyu dada ana mtoto na jamaa mwingine na alivyoniambia na kwamba hawana mahusiano tena na baba mwenye mtoto nkakubali ntamuoa.Cha kunitia wasiwasi ni ukarbu uliopo kati yake na familia ya huyo baba mwenye mtoto,yani wako karibu kiasi kwamba mtoto anaenda kulala huko.Huu ukarbu unanipa wasiwasi kama kweli waliachana au ni kunidanganya tu.Je baadae si utaleta shida kwenye familia yetu.Waungwana hebu naombeni ushauri wenu.

eleza kwanini waliachana.mke huyo anafikiri mini kuhusu ex wake,mama salsa na motto anus Mojave awe waking na Hamas Asiatic Maguire Kaman hamtambui na kumhudumia au mama Saugatuck mote sense kwao na usimtambue Kaman Banque anangangania
 
Hivi kijana mdogo kama wewe huwaoni mabinti wote wanaotoka vyuoni ambao wako fresh?

Hebu tazama kwa mfano huyo mama anaumwa na anahitaji damu na kwa bahati mbaya damu yako wataalam wanasema haimfai halafu anakuja mzazi mwenzake anapimwa damu wataalam wanaihafiki na anatolewa damu ili kumuokoa huyo unayemuona wewe ni mpya je baada ya kupona wewe utajisikiaje?

Na ukumbuke siku ya mtoto wao kuoa au kuolewa wao ndio watakaa high table kama Baba na Mama mzaa chema.

Mnatuchosha kila siku kuomba ushauri wa kijinga wakati mabinti kibao wanahitaji kuolewa.

mwenye mtoto na aolewe na mwanaume mwenye mtoto pia hapo ndio ngoma droo na siyo mvulana mzima na barehe zako unataka used.
naomba nikukumbushe kitu, KUZAA NA MTU HAIMAANISHI NDIYE MUME AU MKE......naona kama hakuna ulichokisema cha maana hapo....
 
mimi kwa mtazamo wangu nahisi huyo mtoto ndugu wa jamaa ndo wanamuulizia /kumpenda.....na wakisema wanamhitaji aende si rahisi kila siku baby mama kutoa visingizio...ila hakuna kinachoshindikana just tok to her,mweleze pia unavyojisikia kuhusiana na hilo....ukishindwa hamieni mbal na maeneo ya hao watu
 
Mkuu umechuma majanga, ukifanikiwa kuachana naye chagua mwanamke asiye na mtoto
 
eleza kwanini waliachana.mke huyo anafikiri mini kuhusu ex wake,mama salsa na motto anus Mojave awe waking na Hamas Asiatic Maguire Kaman hamtambui na kumhudumia au mama Saugatuck mote sense kwao na usimtambue Kaman Banque anangangania

Screen touch noma aisee!
 
Back
Top Bottom