Mueleze tu msimamo wako na jinsi unavochukulia suala zima la yeye kujizoeza na wale kule. Na utoe amko rasmi je mtoto wewe msimamo wako uko vipi, unamlea au utajivua gamba?
Kuna tabia ya baadhi yenu hamtaki mtu ajihusishe na baby dady kwa lolote afu WAGUMU KAMA NYAMA CHOMA KUMUHUDUMIA YULE MTOTO matokea yake mnamuweka mama mtu kati. Ukiombwa ada na matumizi mengine wa kwanza kufungua bakuli lako "SI ANA BABA YAKE?" Afu mwenzio akiwa kwenye harakati za kujikombakomba ili ada itoke kwa urahisi WIVU unakujaaa! ni jambo lisilowezekana mawasiliano yakatike afu huduma iendelee. kama utkava kila kitu sioni kama kutakuwa na issue.
Hii ishu lara 1 nayo huwa kama sandakalawe...mwingine mama mtu anapewa huduma stahiki za mtoto lakini anagoma mtoto asiende hata kusalimia kwa huyo mtoa huduma (baba)!