Ushauri: Kuna mapenzi ya kweli kwa huyu mwanamke?

Status
Not open for further replies.
Hakuna mwanamke hapo.huyo ni mwanamke brezia tu piga chini endelea na maisha yako utapata mwingine mwenye mapenzi ya dhati
 
Ana tension sana ya maisha ya ushindani,ni mpumbavu hana moyo wa kukujali,hana akili...piga chini mkuu huyo n mwanamke wa kutiwa na kuachwa sio wa malengo ya maisha mkuuu..shtuka mapema kabla hujaumia atakuletea ukimwi ndani huyo ni shetani mkuu
 
Huyo sio demu ni M PESA maana kwa miamala hiyo inatosha kujua kwamba huyo sio mke bali M PESA
 
Habari zenu wapendwa?

Nianze hivi! Miezi 5 iliyopita nilikutana na binti mmoja hivi na nikafanikiwa kutengeneza mahusiano naye. Lengo kubwa lilikuwa kufunga naye ndoa kwa kuwa nilimpenda sana, lakini huyu mwezangu hakuwa ameajiriwa na mimi nimeajiriwa.

Tuliishi mikoa tofauti kwa sababu mkoa ninaofanyia kazi ni tofauti na yeye alipo, pia alipo yeye, mimi kule ndo nyumbani, hivyo kila ninapopata likizo huwa nakwenda kusabahi ndugu kwasababu hiyo basi nikamwambia kwa kuwa huna kashughuli kanakoweza kukufanya upate mia mbili mia mbili, ni shughuli ipi unayoweza kuifanya, ikakusaidia hadi tutakapofunga ndoa? Maana si muda wote ninaweza kuwa na hela utakapohitaji hivyo hiyo shughuli inaweza kukusaidia.

Akaniambia kuwa anaweza kununua bidhaa za wanawake kama madera, viatu vya kike, mikoba na kukopesha, hivyo angehitaji mtaji wa kama 500,000, mimi nikampa 400, 000 nikamwambia anzia hiyo na kweli akaanza, but tatizo lilianza pale siku moja aliponiambia kuwa kuna simu ndugu yake anauza, yenye thamani ya 450,000 ila anaiuza kwa shilingi 250,000, hivyo anataka ainunue, ila mimi nikapinga hilo nikamwambia, shughulika na hiyo biashara kwanza, ikichanganyia vizuri mbona unaweza kununua simu ya aina yoyote? Lakini mwezangu akawa kama amebisha hivi hivyo sikutaka kubishana naye, ingawa alikuwa na simu nyingine aina ya tecno W3, aliamua kuinunua na ile kwa kutoa pesa ya mtaji.

Bahati mbaya alipokwenda saloon ile simu aliyonunua 250,000 aliibiwa. Aliniomba radhi kwa kilichotokea na mimi nilimuelewa ingawa aliniambia hata nipa jukumu la kununua simu nyingine, na mimi nikakaa kimya, bdae ikabidi auze ile tecno w3 ili arudishe hela ya mtaji, maana aliitumia kununua ile simu aliyoibiwa saloon.

Baada ya kuuza hiyo tecno w3 akawa hana simu so nikamuonea huruma nikampa 70,000 akaongezea nyengine akaenda kununua smart nyengine, sasa hapo kipindi cha katikati elfu ishirini ishirini nyingi tu nimetuma kwake, so nikifanya majumlisho kama 800,000 imetumika wake ukijumlisha na mtaji niliompa.

Sasa juzi kati kaniambia kuwa ameambiwa kuwa achangie jiko la gas kwa ajili ya harusi ya ndugu yake, mimi nikamuuliza wanakupa majukumu hayo kwani wewe una kazi? Nikamwambia sasa hivi sina pesa, maamuzi aliyochukua ni kuuza ile simu niliyomchangia 70,000 kununua, ili akanunue jiko la gas kwa ajili ya huyo ndugu yake anayeolewa.

Sasa sakata likapamba moto aliponiambia kuwa hana simu hivyo nimpe 30,000 akanunue simu ndogo, nikamwambia sina, vumilia nitakupa, akaniambia kanikopee, nikamwambia siwezi kwenda kukopa, akaniambia sasa wewe ni mwanaume gani huna hata akiba ya 30,000? Nikamuuliza mbona wewe huna hiyo 30,000, akanambia siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana uwezo wa kunisaidia nikiwa nadharula ya pesa Kama hivi. Nikamwambia sawa mama.

Ushauri wenu wadau kuna mapenzi ya kweli hapa?

Au nimepotea njia?
mwanamke akishakutajia bkuwa biashara anayoiweza ni kuuza madela,pochi za wanawake sijui vitu vya saloon jua hapo mwanamke wa ndoa hamna.
 
Sio mke huyo kwanza hana huruma na wewe kbs pili hakusikilizi na ana kauli mbovu hapo bado hujamuoa ukimuoa je itakuwaje
 
Kwanza pole sana kwa kuhonga mtaji wa laki 8 huku wadogo zako wanalia hata wapate laki 3 waanzie mtaji lakini hukujali kwa kujali moyo wako ili upate unacho sitahiki ukahonga mtu asie na fadhila ushauri wangu kwako achana na huyo shetani asie tambua changamoto za kutafta pesa na pia usizoee kutongoza wanawake hoe hae bora tongoza mamantilie maana anajua changamoto za utaftaj pesa
 
Huyo hakupendi hata robo yaani wanawake ni very janjful hapo ana mtu anayempenda kwa dhati wewe unachunwa mpige chini tafuta mwingine atakukumbukaga mbele ya safari
 
Ulipenda kusikopendeka kaka. Pia una roho ya huruma yaani umetulia mpaka kala hizo zote 800000 daaaah!!!!! Mimi ningemteka arudishe hata nusu yake Ila ushauri wangu .... Uguza maumivu tu maana hamna namna
 
Habari zenu wapendwa?

Nianze hivi! Miezi 5 iliyopita nilikutana na binti mmoja hivi na nikafanikiwa kutengeneza mahusiano naye. Lengo kubwa lilikuwa kufunga naye ndoa kwa kuwa nilimpenda sana, lakini huyu mwezangu hakuwa ameajiriwa na mimi nimeajiriwa.

Tuliishi mikoa tofauti kwa sababu mkoa ninaofanyia kazi ni tofauti na yeye alipo, pia alipo yeye, mimi kule ndo nyumbani, hivyo kila ninapopata likizo huwa nakwenda kusabahi ndugu kwasababu hiyo basi nikamwambia kwa kuwa huna kashughuli kanakoweza kukufanya upate mia mbili mia mbili, ni shughuli ipi unayoweza kuifanya, ikakusaidia hadi tutakapofunga ndoa? Maana si muda wote ninaweza kuwa na hela utakapohitaji hivyo hiyo shughuli inaweza kukusaidia.

Akaniambia kuwa anaweza kununua bidhaa za wanawake kama madera, viatu vya kike, mikoba na kukopesha, hivyo angehitaji mtaji wa kama 500,000, mimi nikampa 400, 000 nikamwambia anzia hiyo na kweli akaanza, but tatizo lilianza pale siku moja aliponiambia kuwa kuna simu ndugu yake anauza, yenye thamani ya 450,000 ila anaiuza kwa shilingi 250,000, hivyo anataka ainunue, ila mimi nikapinga hilo nikamwambia, shughulika na hiyo biashara kwanza, ikichanganyia vizuri mbona unaweza kununua simu ya aina yoyote? Lakini mwezangu akawa kama amebisha hivi hivyo sikutaka kubishana naye, ingawa alikuwa na simu nyingine aina ya tecno W3, aliamua kuinunua na ile kwa kutoa pesa ya mtaji.

Bahati mbaya alipokwenda saloon ile simu aliyonunua 250,000 aliibiwa. Aliniomba radhi kwa kilichotokea na mimi nilimuelewa ingawa aliniambia hata nipa jukumu la kununua simu nyingine, na mimi nikakaa kimya, bdae ikabidi auze ile tecno w3 ili arudishe hela ya mtaji, maana aliitumia kununua ile simu aliyoibiwa saloon.

Baada ya kuuza hiyo tecno w3 akawa hana simu so nikamuonea huruma nikampa 70,000 akaongezea nyengine akaenda kununua smart nyengine, sasa hapo kipindi cha katikati elfu ishirini ishirini nyingi tu nimetuma kwake, so nikifanya majumlisho kama 800,000 imetumika wake ukijumlisha na mtaji niliompa.

Sasa juzi kati kaniambia kuwa ameambiwa kuwa achangie jiko la gas kwa ajili ya harusi ya ndugu yake, mimi nikamuuliza wanakupa majukumu hayo kwani wewe una kazi? Nikamwambia sasa hivi sina pesa, maamuzi aliyochukua ni kuuza ile simu niliyomchangia 70,000 kununua, ili akanunue jiko la gas kwa ajili ya huyo ndugu yake anayeolewa.

Sasa sakata likapamba moto aliponiambia kuwa hana simu hivyo nimpe 30,000 akanunue simu ndogo, nikamwambia sina, vumilia nitakupa, akaniambia kanikopee, nikamwambia siwezi kwenda kukopa, akaniambia sasa wewe ni mwanaume gani huna hata akiba ya 30,000? Nikamuuliza mbona wewe huna hiyo 30,000, akanambia siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana uwezo wa kunisaidia nikiwa nadharula ya pesa Kama hivi. Nikamwambia sawa mama.

Ushauri wenu wadau kuna mapenzi ya kweli hapa?

Au nimepotea njia?
Hapo huna mchumba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom