Ushauri: Kuna mapenzi ya kweli kwa huyu mwanamke?

Ushauri: Kuna mapenzi ya kweli kwa huyu mwanamke?

Status
Not open for further replies.

Ndama Jeuri

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
1,541
Reaction score
1,550
Habari zenu wapendwa?

Nianze hivi! Miezi 5 iliyopita nilikutana na binti mmoja hivi na nikafanikiwa kutengeneza mahusiano naye. Lengo kubwa lilikuwa kufunga naye ndoa kwa kuwa nilimpenda sana, lakini huyu mwezangu hakuwa ameajiriwa na mimi nimeajiriwa.

Tuliishi mikoa tofauti kwa sababu mkoa ninaofanyia kazi ni tofauti na yeye alipo, pia alipo yeye, mimi kule ndo nyumbani, hivyo kila ninapopata likizo huwa nakwenda kusabahi ndugu kwasababu hiyo basi nikamwambia kwa kuwa huna kashughuli kanakoweza kukufanya upate mia mbili mia mbili, ni shughuli ipi unayoweza kuifanya, ikakusaidia hadi tutakapofunga ndoa? Maana si muda wote ninaweza kuwa na hela utakapohitaji hivyo hiyo shughuli inaweza kukusaidia.

Akaniambia kuwa anaweza kununua bidhaa za wanawake kama madera, viatu vya kike, mikoba na kukopesha, hivyo angehitaji mtaji wa kama 500,000, mimi nikampa 400, 000 nikamwambia anzia hiyo na kweli akaanza, but tatizo lilianza pale siku moja aliponiambia kuwa kuna simu ndugu yake anauza, yenye thamani ya 450,000 ila anaiuza kwa shilingi 250,000, hivyo anataka ainunue, ila mimi nikapinga hilo nikamwambia, shughulika na hiyo biashara kwanza, ikichanganyia vizuri mbona unaweza kununua simu ya aina yoyote? Lakini mwezangu akawa kama amebisha hivi hivyo sikutaka kubishana naye, ingawa alikuwa na simu nyingine aina ya tecno W3, aliamua kuinunua na ile kwa kutoa pesa ya mtaji.

Bahati mbaya alipokwenda saloon ile simu aliyonunua 250,000 aliibiwa. Aliniomba radhi kwa kilichotokea na mimi nilimuelewa ingawa aliniambia hata nipa jukumu la kununua simu nyingine, na mimi nikakaa kimya, bdae ikabidi auze ile tecno w3 ili arudishe hela ya mtaji, maana aliitumia kununua ile simu aliyoibiwa saloon.

Baada ya kuuza hiyo tecno w3 akawa hana simu so nikamuonea huruma nikampa 70,000 akaongezea nyengine akaenda kununua smart nyengine, sasa hapo kipindi cha katikati elfu ishirini ishirini nyingi tu nimetuma kwake, so nikifanya majumlisho kama 800,000 imetumika wake ukijumlisha na mtaji niliompa.

Sasa juzi kati kaniambia kuwa ameambiwa kuwa achangie jiko la gas kwa ajili ya harusi ya ndugu yake, mimi nikamuuliza wanakupa majukumu hayo kwani wewe una kazi? Nikamwambia sasa hivi sina pesa, maamuzi aliyochukua ni kuuza ile simu niliyomchangia 70,000 kununua, ili akanunue jiko la gas kwa ajili ya huyo ndugu yake anayeolewa.

Sasa sakata likapamba moto aliponiambia kuwa hana simu hivyo nimpe 30,000 akanunue simu ndogo, nikamwambia sina, vumilia nitakupa, akaniambia kanikopee, nikamwambia siwezi kwenda kukopa, akaniambia sasa wewe ni mwanaume gani huna hata akiba ya 30,000? Nikamuuliza mbona wewe huna hiyo 30,000, akanambia siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana uwezo wa kunisaidia nikiwa nadharula ya pesa Kama hivi. Nikamwambia sawa mama.

Ushauri wenu wadau kuna mapenzi ya kweli hapa?

Au nimepotea njia?
 
Mkuu huyo hana akili nzuri. Ukiendelea naye nadhani by December utaleta uzi kuwa mmeachana na ledger yako inakua ina hisabati ya million 10 ulizomtumia.

Bora ufanyie hela yako biashara za kukuingizia kipato tofauti na ajira kaka. Usipoteze time
 
semester moja tu ya mapenzi mmekuwa kama mmeishi miaka mitano!
Kwa kweli kaka nakushauri usiwe unatoa pesa hovyo hovyo kwa mwanamke wako,
Akikuzoea kihela hela, utamkoma.....
Tatizo nilikuwa namuonea huruma the way anavyoishi, so nikaamua kuchukua uamuzi huo
 
Inaonekana huyo mlembo wako anahitaji ushauri nasaha ju ya matumizi mazuri ya pesa hasa ya biashara, vinginevyo mmmm!utakuja juta zaidi ya sasa !
 
Mkuu huyo hana akili nzuri. Ukiendelea naye nadhani by December utaleta uzi kuwa mmeachana na ledger yako inakua ina hisabati ya million 10 ulizomtumia.

Bora ufanyie hela yako biashara za kukuingizia kipato tofauti na ajira kaka. Usipoteze time
Ahsante mkuu
 
Tatizo nilikuwa namuonea huruma the way anavyoishi, so nikaamua kuchukua uamuzi huo
unamuonea huruma chatu kisa yuko kwenye tope?
ona sasa umemtoa, alichokufanya unasimulia huku na kule
btw, sijamaanisha usiwaonee huruma she wako, namaanisha kuwa makini na wallet yako
Open it where necessary only...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom