Ushauri kuhusu mashine za EFD; Gharama za kununua mpya na matengenezo ni ghali sana, mamlaka zifuatilie

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kulipa kodi ni jambo la muhimu kwa maendeleo ya nchi yeyote. Mfano barabara, vituo vya afya, miradi ya maji, madarasa, mishahara n.k. yote haya yanalipwa na kodi za Serikali na hivyo lazima tulipe kodi.

Kinachonishangaza ni Makampuni yaliyopewa ruhusa na Serikali kuwauzia wafanyabiashara mashine zilizotajwa. Kwa kweli Makampuni haya ni kero na siyo za Kitanzania.

Mfano hai ni pale unapoenda kununua mashine, bei ya mashine hizi ni kubwa na huchukua muda mrefu sana ili mfanyabiashara kuchukua mashine yake aliyonunua. Uharibifu wa mashine hizi zinatisha.

Kwa mwaka unaweza kuharibikiwa na mashine hizi takriban mara tano na ukienda kutengeneza utaambiwa na haya Makampuni kuwa gharama ya kuitengeneza ni Tshs.150,000 kwa wakati mmoja.

Ukichukua hayo mahesabu kwa mwaka mfanyabishara anatumia karibu Tshs.800,000. Nitoe ushauri kwa TRA kwanza Makampuni yanayouza mashine za EFD yawe ya Kitanzania.

Pili, wafuatilie gharama ya matengenezo ni kwanini yanakuwa ghali hivyo?.

Mwisho, nawashauri Watanzania tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Umefanya vizuri kumalizia kutushauri tulipe kod kwa maendeleo ya nchi yetu. Ingekuwa vizur pia ukamshauri na yule anayezitumia hizo Kodi kugawa zawadi ya birthday ya gar ya mil 400, na kudhurura nchi za watu kwa kod hizo hizo akaache. Ni hayo tu
 
Umefanya vizuri kumalizia kutushauri tulipe kod kwa maendeleo ya nchi yetu. Ingekuwa vizur pia ukamshauri na yule anayezitumia hizo Kodi kugawa zawadi ya birthday ya gar ya mil 400, na kudhurura nchi za watu kwa kod hizo hizo akaache. Ni hayo tu
Kweli aisee,na aliyejenga uwanja wa ndege wa ndege Kijijini kwake Chato asisahaulike aisee.
 
Back
Top Bottom