Beberu Mwitu
JF-Expert Member
- Mar 31, 2019
- 491
- 692
Habari za muda huu ndugu zanguni, niende moja kwa moja kwenye mada husika;
Naomba msaada au ushauri wa haraka kuhusu mahali pa kupanga chumba au vyumba kwa maeneo ya karibu na kambi ya Jeshi ya Mgulani au Uwanja wa Taifa. Nimepangiwa kufanya kazi eneo la karibu na hayo niliyoyataja, na natarajia kuhamisha makazi kutoka mkoani kwenda huko mjini hivi karibuni. Binafsi si mgeni sana na Dar Es Salaam, niliwahi kuishi huko miaka kuanzia 2011- 2019. Japo maisha yangu yalikuwa upande wa Kunduchi.
Manispaa ya Temeke na maeneo ya jirani si mwenyeji kabisa.Naomba ushauri sehemu salama na nafuu(isiwe prone to flooding au wizi uliokithiri)ya kuweka makazi yangu ambayo hayatakuwa mbali sana na eneo langu la kazi. Na kama nitahitajika kupanda gari basi liwe gari moja tu. Gharama ziwe za chini kwendana na mishahara ya serikali na si makampuni makubwa.
Natanguliza shukrani.