Ushauri kuhusu biashara ya Suzuki Carry (Kirikuu) unahitajika

madam akii

New Member
Sep 13, 2015
1
0
Natumaini muwazima wa afya humu ndani, naomba anae jua biashara hii ya magari haya, anieleweshe inaendaje? Nataka nikope benk, ninunue kama vi 3, je zina faida?
 
Kabla haujapata presha ya magari utaipata kwanza ya huo mkopo!Anyway nakushauri tumia pesa yako mwenyewe hata kama itakuwa inatosha gari moja tu!Kuhusu kulipa hakuna biashara isiyolipa hapa duniani ndio maana watu wanazifanya!,Akili yako ndio mafanikio yako!kila la kheri mkuu
 
Me ninazo 4, ila kua makini na madereva maana cku ya kuleta hesabu ni shida unaweza ambulia mkate.
 
Mkuu Madam akii Engine rock alichokwambia ndiyo ukweli Madereva ni pasua kichwa kwenye hiyo biashara chunga sana.
 
Natumaini muwazima wa afya humu ndani, naomba anae jua biashara hii ya magari haya, anieleweshe inaendaje? Nataka nikope benk, ninunue kama vi 3, je zina faida?
Ukikopa njoo nikuuzie hii ya kwangu bado mpya
 
Inashangaza michango ya wengi hapa. Ni kukatisha tamaa zaidi.

Ina maana hizo gari zinaletwa Tanzania kwa makusudi gani ?

Wakati mwingine, inabidi uyapokee maoni ya watu kwa hadhari sana, maana kila jambo utakalotaka kufanya watakuambia haiwezekani.

Lakini kila siku, tunaona gari barabarani zimebeba mizigo.

Ushauri ni kwamba, kama unafikiria kuanzisha biashara hiyo , uwe na mpango kazi ( business plan)

Fungua kampuni ya usafirishaji.

Tafuta makampuni ambayo unaweza kuwapa huduma ya usafiri wa kutumia gari yako.
Mfano, kuna makampuni ambayo ni distributor .... Hawawezi kufika kila eneo katika mji huu wa DSM hapo ndipo unaweza ukaingia.

Hebu angalia mtaani kwako, bidhaa gani zinaletwa kwa magari , unaweza ukapata idea, ongea na madereva kutaka kujua undani kidogo wa mambo. Bidhaa ni nyingi, kuna mikate, maji, bidhaa mbalimbali za duka nk.

Fanya biashara na makampuni , watakuwa wanahitaji huduma ya usafirishaji .

Ni bora ukajiingiza kwenye kutafuta soko kwa ajili ya gari, kuliko kumuachia dereva jukumu hilo.

Unapomuachia dereva jukumu hilo, basi matokeo yake dereva anafanya chochote, ambayo italeta madhara kwa mwenye gari.

Dereva aajiliwe tu kwa ajili ya huduma na alipwe mshahara .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom