Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Leseni ya biashara achana nayo kwanza lipia fremu nunua vitu vinavyotoka sana kwenye eneo lako anza kazi.
Pesa zako za faida utakazopata za kwanza kabisa ndio uende huko TRA ukiwafata kabla wanakuulia mtaji hawana maana
 
Mtaani hakufai mkuu wangu, nimezunguka na vyeti mpk kichwa kinawaka moto, sasa nimeamua kuchukua akiba yangu nijilipue
Unauamuzi wa akili mingi mno hongera sana, TRA waliwahi kwenda kwenye duka la wazazi wangu wakafanya mahesabu yao wakamkadiria milioni 3 anauwezo wa kuiingiza kwa mwezi kutokana na ukubwa na mazingira lililopo hivyo kodi yake ilikua yakutisha.

Akili ni usiende mpaka upate faida wale ni harvest.
 
Tafuta fremu, weka miundo mbinu yako, weka bidhaa, nenda TRA kwa ajili ya TIN & kodi,t afuta leseni, fungua duka na anza kula matunda ya nchi.
 
Tafuta fremu,weka miundo mbinu yako,weka bidhaa,nenda TRA kwa ajili ya TIN & kodi,tafuta leseni,fungua duka,na anza kula matunda ya nchi
Bidhaa za duka mkuu mtaji bado mdgo, ni milion mbili na nusu tu, ndio maana nataka nianze na vinywaji baridi ili kuukuza huku mfumo ukibadiklika taratibu.
 
Kuna haja ya masomo ya business and entrepreneurship kuanza kufundishwa kuanzia secondary na kuendelea, ili kuondoa sintofahamu pindi mtu anapotaka kuanzisha biashara technics know how. Sio anamaliza chuo kikuu hajui hata procedures ya namna gani ya kuanzisha biashara kulingana na sheria za nchi yake aliyopo!.
 
Kuna haja ya masomo ya business and entrepreneurship kuanza kufundishwa kuanzia secondary na kuendelea, ili kuondoa sintofahamu pindi mtu anapotaka kuanzisha biashara technics know how. Sio anamaliza chuo kikuu hajui hata procedures ya namna gani ya kuanzisha biashara kulingana na sheria za nchi yake aliyopo!.
Kwel mkuu, hii imekuwa ni changamoto moja wapo
 
Habarini za mchana jamani nilikuwa naombeni ushauri nahitaji kufungua biashara ya duka la vinywaji mtaji nimetenga km sh. mil.2 ambavyo itakuwa ni kwareja reja. nilikuwa nataka kwa anaefanya biashara hyo nijue kiasi cha mtaji na maeneo ambapo unaweza kufanya biashara hyo.
 
Usisahau kuweka pombe kama prince na veve,konyagi ndogo na valeur ndogo pia kvant ndogo,shujaa
 
Back
Top Bottom