ferucho lamborgini
Senior Member
- Nov 25, 2023
- 185
- 599
Napitia changamoto kuhusiana na maswala ya mizimu, nataka ninunue mbuzi, mbege na vitu vyingine vitakavyotumika kwenye mila.
Nipo mkoa mwingine sipo moshi, ila changamoto nyingine kule kijijini wazee waliacha mila baada ya kushawishiwa na ndugu zetu wasomi uchwara waliobahatika kupata pesa na kukimbilia kwa mwamposa, ila mila hazikuvunjwa zingatieni hili wakuu kwahiyo bado tupo kwenye mikataba na mizimu.
Ombi langu ni kwamba nitawezaje kuwapooza hawa wazee wangu(mizimu) kwa kuchinja mbuzi angali sipo moshi na kule kuna changamoto nilizozitaja hapo juu wale wazee hawatakubali kirahisi.
kuna mtu kanishauri niende moshi nikachukue udongo alafu nirudi mkoani nichinje mbuzi na kuomba mizimu je hii itafaa?
Naombeni ushauri wachagga wenzangu.
Wale wafia dini naombeni mpite kimya kimya kama umeona kinyesi kibichi.