Ushauri:Kariakoo Business usiness Tour, September/October 2023.

Muigai Jr

JF-Expert Member
Jun 3, 2020
1,529
2,969
Salaam Wana JF,
Kama kichwa cha habari kinavo jieleza hapo juu,baada ya mapambano makali ya kujinasua kiuchumi,hatimaye nimepanga kufika mjini Dar es Salaam hususani maeneo ya Kariakoo kwa ajili ya Uchunguzi wa biashara mbali mbali.

Lengo haswa la Uchunguzi huu ni kujua bei mbali mbali za bidhaa tofauti lkn pia kugundua fursa mpya ambazo zitajitokeza.

Ushauri itajika kutoka kwenu;

1.Malazi;Yawe ni karibu na Eneo husika lkn pia kwa bei ya wajasiriamali.

2.Muda;Ni mda gani recommended kufanya tour km hiyo??

3.Chocho;nianzie wapi na nimalizie na wapi?

4.Mazingatio;Ni nini haswa cha kuzingatia nikiwa kwenye tour km hiyo na haswa Mjini Dar as Salaam?

5.Mengineo; uzoefu kutoka kwenu wana jamvi.

Asanteni.
 
3.Chocho;nianzie wapi na nimalizie na wapi?

4.Mazingatio;Ni nini haswa cha kuzingatia nikiwa kwenye tour km hiyo na haswa Mjini Dar as Salaam?

5.Mengineo; uzoefu kutoka kwenu wana jamvi.
Ni vyema ukapata mwenyeji, kwa mafanikio zaidi.
 
Biashara ya aina gam unapendelea, mana kkoo kila mitaa ime specialize na bidhaa fulan
 
Biashara ya aina gam unapendelea, mana kkoo kila mitaa ime specialize na bidhaa fulan
kwa sasa nafanya biashara mchanganyiko,ikijumuisha uuzaji wa vitu vidogo vidogo na tofauti ni ubunifu wangu mwenyewe...ila kwenye hiyo tour nataka ku explore.
 
Uwe na vibebea taarifa km notebook au camera.
Muda wowote wakati nuru ya jua ikiangaza kwa sababu usiku hakuna bishara.
Chocho inategemea umelenga kutembelea maeneo gani kulingana na bidhaa/huduma unayotoa wewe.
Malazi, njoo kaa maeneo ya mabibo, kigogo, luhanga usafiri hadi kariakoo upo muda wa kuaminika jero tu kwa ruti moja.
Ukihitaji muongozo zaidi, nipm
 
Back
Top Bottom