Kwa utangulizi mimi ni expert member humu ndani lakini juzi kati hapa nimeona nifungue hii akaunti mpya maana ile nyingine ina majina yangu halisi kwa hiyo inaninyima uhuru wa kujiachia ukizingatia kuna washkaji kadhaa humu wananijua.
Huyu binti tulianza naye mahusiano tukiwa chuo tukiwa mwaka wa pili. Yeye kozi yake ilikuwa ya miaka mitatu huku yangu ikiwa ya miaka minne. Tulipofika mwaka wa tatu alipata ujauzito huku akibakiza kama miezi mitatu hivi kabla ya kumaliza chuo huku mimi nikibakiza mwaka mmoja zaidi mbele.
Alisisitiza kuwa hasingeweza kutoa ile mimba maana huko nyuma alivomaliza kidato cha sita aliwahi kuwa na boyfriend wake na alitamani sana apate ujauzito ndo aje chuo lakini hakubahatika, nami sikuona tabu kuzaa maana nimewahi kuwa na mahusiono huko nyuma lakini sikuwai kumpa binti mimba kwa hiyo hili lilikuwa ni tukio la kwanza kwangu na lilikuwa amazing fulani hivi kwangu.
Tatizo hadi kipindi hicho anapata mimba tulikuwa tunavutana mara nyingi maana alikuwa ana kiburi sana kwa hiyo ingawa nilikuwa nampenda sana lakini niliona hatuwezani kabisa. Nilipopata taarifa hii ya mimba nilibadili mawazo juu yake maana niliwaza kuwa ningeendelea na yale mawazo ya kushindwananaye ingeonekana nakwepa majukumu ya kulea mimba na hatimaye mtoto.
Tulifunga chuo huku yeye akiwa amehitimu masomo yake akiwa mjamzito. Ilinibidi niahirishe masomo kwa mwaka mmoja ili niweze kumtunza. Nilipanga nyumba ya vyumba vitatu Dar naye akahamia kwangu tukiishi kama mke na mume.
Ila alipata mapingamizi mengi toka kwao akiwemo huyu mama yake (mama mkwe) ambaye hakutaka tuoane kwa sababu za majungu ya huko kijijini kwetu maana tunajuana hadi nyumbani. Alijifungua mtoto wa kike na mtoto tunafanana kweli kweli.Huyu binti aliendelea na kiburi vile vile kwa kipindi chote hichi kabla na hata baada ya kujifungua.
Sasa mwaka mwingine wa masomo ukawa umewadia nikarudi chuo, nikamuacha huyu mke nyumbani nikamfungulia na duka la simu. Kilichotokea huko nyuma huwezi amini macho yako. Mke alikomba vitu vya ndani na akaenda kupanga kwingine na akampeleka mtoto kwa mamake huko mkoani kwa ushauri wa huyo mamake. Kumbuka hapo hatukuwa na ndoa maana kwa tabia zake sikuona haja ya kuharakisha ndoa. Nilimtafuta ndani ya muda mfupi nikampata na nikarudisha vitu vyangu nyumbani.
Mpaka sasa huyo mwanangu yuko huko mkoani kwa mama mkwe huyo na natoa matumizi kama kawaida maana bado niko masomoni namaliza mwezi wa sita mwaka huu, huku huyu mama mtoto yupo Dar anaponda raha akijidai anatafuta kazi.
Sasa leo nimempigia simu mama mkwe kwa lengo la kujua hali ya mtoto na hili nalifanya mara kwa mara, na mwisho wa maongezi kaniomba laki na nusu eti ana shida sana na kama vipi atanirudishia.
Naombeni ushauri wandugu, nimpe hii hela kweli huyu mama mkwe ukizingatia sina tena mpango wa kuishi na binti yake? Nina mpango tu wa kwenda kumchukua mwanangu punde tu nikimaliza chuo. Ukizingatia pia mchango wake kwenye kuvuruga huu uhusiano?