Ushauri juu ya Bati ya kuezeka ALAF

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
2,022
2,592
Salaam kwa wanajukwaa.Naamini tuko poa kabisa.
Kwenye mada hapo naombeni ushauri juu ya geji ya bati ya kupaua kutoka kampuni ya Alaf.
Nimezunguka kwenye maduka nakutana na za geji 30 tu hizi ni zile migongo mipana ( Cover max). Kila nikiulizia geji 28 naambiwa ni kwa oda maalum na wanakiri hzo n kwa ajili ya majengo ya serikali.
Bei zipo kama ifuatavyo.
Cover max geji 28 70000/= kwa bati la ft 10.
Cover max/Resincoat geji 30 ni 42000 kwa bati la ft 10
Muundo wa kigae 78000/= hili n geji 28 tu linapatikana.
Kwa mliopaua na wajuvi wa mbati naombeni ushauri je nikichukua migongo mipana geji 30 linafaa kwa upauaji?.
Mbarikiwe. NB nipo mkoani na bei zimechangamka maana kwenye tovuti ya alaf naona bei n nzuri mfano geji 28 migongo mipana ni 51500 tu.
Karibuni kwa ushauri
 
kwa upande wangu nilinunua hili bati ambalo kwa nilipo alaf wanauza 39500, ni bati zuri ila kama una mfuko mrefu chukua ile ya kigae ina muonekano maridadi.
Asante kiongozi kwa ushauri nitazingatia.Kigae balaa bei yake aisee upande wa Alaf.Itabd nikae humo humo migongo mipana.
Vipi swala la kuwa yanawahi kuvuja kwako hujalipitia tangu uliponunua?
 
Salaam kwa wanajukwaa.Naamini tuko poa kabisa.
Kwenye mada hapo naombeni ushauri juu ya geji ya bati ya kupaua kutoka kampuni ya Alaf.
Nimezunguka kwenye maduka nakutana na za geji 30 tu hizi ni zile migongo mipana ( Cover max). Kila nikiulizia geji 28 naambiwa ni kwa oda maalum na wanakiri hzo n kwa ajili ya majengo ya serikali.
Bei zipo kama ifuatavyo.
Cover max geji 28 70000/= kwa bati la ft 10.
Cover max/Resincoat geji 30 ni 42000 kwa bati la ft 10
Muundo wa kigae 78000/= hili n geji 28 tu linapatikana.
Kwa mliopaua na wajuvi wa mbati naombeni ushauri je nikichukua migongo mipana geji 30 linafaa kwa upauaji?.
Mbarikiwe. NB nipo mkoani na bei zimechangamka maana kwenye tovuti ya alaf naona bei n nzuri mfano geji 28 migongo mipana ni 51500 tu.
Karibuni kwa ushauri
Kama unataka kitu ambacho hata mjuu atakuja kukusifia kwa kazi bora basi funga za geji 28. Kama unataka nunua kwa jumla nenda kiwandani kabisa.

NB: Rahisi ni gharama.
 
Nimekusoma kiongozi wacha nijikusanye mdogo mdogo nikabebe za 28g.
Tatizo hapa nilipo nyingi zipo za gauge 30 upande wa cover max.Geji 28 ni zile versatile tu.But nitapambana nikamatie tu gauge 28 kivyovyote
 
Back
Top Bottom