Napagawa na Bati: ALAF, ANDO, DRAGON - uchaguzi mgumu. Watu wa mauzo saundi kibao!

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Nimemaliza Kupiga Mbao, site yangu wameshakuja watu wa sales wa makampuni mbalimbali, na wamenipiga saundi za kutosha.

Mafundi nao waliopiga mbao wamenishauri ila walivyoona nimepagawa sielewi nitumie bati kampuni Gani wakaniambia wewe Bosi leta bati yeyote sisi tutapiga mana sijui tukushaurije.

Katika watu na makampuni niliongea nao Kila mmoja anavutia kwao, nimeamua Sasa nibaki na choises tatu tu ANDO, ALAF na Dragon mana nisije kuchizika.

Katika bei ukipanga Kwa namba 1, 2 ,3 wakwanza na wapili tofauti ya bei ni 2800 , wapili na watatu tofauti ya bei ni 3000, na wakwanza na watatu tofauti ya bei ni 5300 Kwa Kila MITA ya bati, Mimi nahitaji mita 600.

Sasa mabati yote ni mazuri, ila kati ya Ando, ALAF na Dragon nani Bora zaidi, hapa ndo mtego umejificha, makampuni mengi yanasema hiyo kampuni bei yao IPO juu c Kwa sababu ya ubora Bali ni kwasababu Wana brand kubwa.

Naombeni mnishauri, nichukue bati Gani ambayo itakuwa ni Bora zaidi kati ya hizo tatu hapo juu.
 
Mkuu acha kupata shida njooo sunbank nikuuzie bati Bora kwa gharama nafuu kuhusu ubora tunazo evidence za project ambazo tumeezeka nazo nyingi Zina 5yrs +
No kupauka
Kabla ujanunua fanya research za izo project
Mfno kwa moja ya project zetu Kati ya nyingi apa dar tumeezeka maktaba kuu ya taifa

0685572320
 
Uchaguzi wa mabati inabidi uende moja kwa moja kiwandani wakuelekeze Wakala wao wakuaminika.

Kuna kampuni moja niliwahi kununua miaka kama 8 nyuma sijui kama sasa ipo. Inaitwa Lugoba Mabati Imara.

Nilijenga nyumba za wapangaji kipindi hicho hiyo kampuni mpya. Zile bati mpaka leo zinang'aa. Yaani mvua ikinyesha zinajisafisha zinakuwa kama zimepigwa jana.

Hayo majina ni brands tu. Ongea na mafundi wakongwe wa mapaa kama Muarami Kinguku watakushauri
 
Back
Top Bottom