Kaunga
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 12,529
- 13,502
Pole sana mkuu kwa hiyo changamoto ...
Nashindwa kuchangia sana maana umesema kuwa mgogoro ulianza baada ya yeye kuanza kumiliki pesa nyingi. Ktk hali ya kawaida ni vigumu mtu kubadilika kwa kupata pesa pekee yake, lazima kutakuwa na chanzo halisi cha tatizo maana inaweza kuwa hata umiliki wake wa pesa nyingi kwa upande wako umekuwa tatizo na kukufanya ujijengee hali ya kujidharau au pengine kuona unadharauliwa.
Hebu kaa chini na jaribu kuchunguza chanzo cha tatizo bila kufikiria suala la yeye kumiliki pesa nyingi ...
Kwa sehemu nafahamu mabadiliko ya kisaikolojia yanayoweza kumpata mwanaume aliyekuwa na uwezo mkubwa kuliko mpenziwe mambo yanapogeuka na yeye kuwa na kipato cha chini kuliko mpenziwe ...!
Ni vizuri kujiassess na yeye; lkn nikiangalia jinsi gani watu hubadilika pindi wapatapo pesa naweza amini aisee.
Angalia wababa wangapi waliozisaliti ndoa zao baada ya kupata pesa na kuona huyo mwenzi wake sio class yake tena.
Kina dada nasi tumo, unakuwa na mtu kwakuwa anakutimizia mahitaji yako lkn haumpendi sana kiasi kwamba ukiweza simama kwa miguu yako mwenyewe umuhimu wa huyo mtu unakuwa haupo tena.
Mkaka akubali yaishe, akijifanyia analysis sana ndipo anaweza akajiona inferior; ni bora amuone mwanamke opportunist na kwamba she is not worth his love!