PLATO MAGELE
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 203
- 54
Kuna mwanamke nilimpenda sana na tukapeana ahadi ya kuoana, baada ya makubaliano hayo alikuwa na mtoto nikaamua kumsomesha kwenye shule ya English medium karo zaidi ya milioni moja na mtoto huyo sasa mwaka huu atakuwa darasa la sita. Mgogoro katika mahusiano umeanza baada ya yeye kuanza kumiliki hela nyingi za kwake. Kipindi nampata alikuwa mnyenyekevu sana, mwenye upendo na utii usio wa kawaida kwangu. Kwa sasa siko karibu naye nikipiga simu hata hapokei kabisa. Jamani mimi nifanyeje?