Ushauri jamani, anataka turudiane

Ushauri jamani, anataka turudiane

The Professor

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
2,223
Reaction score
4,586
Nakuja mbele zenu wana JF ushauri wenu ni muhimu sana,

Nilikua na mpenzi wangu, nilimpenda sana toka moyoni, awali tulipendana sana, watu kibao waliisifia relation yetu, nilijiona kua miongoni mwa wanaume wachache wenye bahati ya kupenda na wakapendeka.

Lakini huwezi amini, baada ya kama miezi 11 hivi ya mahusiano yetu, mpenzi wangu alianza kubadilika, nilijipa moyo kua huenda anatingisha kiberiti kunipima kama bado nampenda.

Daanh hapo ndipo akili ziliponifunguka, kumbe nilivokua najiona kua miongoni mwa wanaume wachache wenye bahati nilikua najidanganya kwa sababu licha ya kumfanyia kila kitu mpenzi wangu aliniacha, sikumkosea wala siku cheat, niliumia sana, nilikua nampenda sana, nilihisi nataka nife kwa jinsi nilivyompenda.

Nikiwa katika maumivu yangu yasiyo na hata lepe la ahueni, msichana mwingine akatokea kunipenda, anaitwa Clara, kumbe nyuma ya pazia huyu michana alikua best yake na msichana wangu wa zamani, awali nilimkataa huyu msichana sabu nilianza kuchukia mapenzi lakini kwa jinsi alivyonijali nikajikuta namkubalia.

Muda wote yule msichana wangu wa zamani alikua anatoka na jamaa mmoja wa kiarabu ambaye alikua ana hadi gari ya kutembelea ya mshua wake, so baada ya ujo jamaa kumtumia msichana wangu wa zamani na kumchoka, amemuacha.

Sasa alivopigwa chini ndo ameanza kunitafuta anadai bado ananipenda, mara nyingi anakuja hadi home kunitafuta, mimi bado nampenda lakini namheshimu sana Clara naogopa kumuumiza sabu ananisaidia mambo mengi, yani uwepo wake umenifaidisha na kunijenga sana kifikra na kila kitu.

Naombeni mnishauri wadau
 
Acha ujingaa, mpende clara, wewe utakuaje spea,alafu moyo wa kurudiana na mwanamke unaejua kabisa alikua anatembea na mwanaume mwingine unatoka wapi.

Kama alikuacha akaenda kwa mwarabu,hata sasa atakuacha tu akipata mhindi au mchina.

Mimi mwanamke nikishajua anaetembea nae huwa simtongozi hata bure sitaki.

Hapo sasa uko njia panda gani,mbona kila kitu wazi kabisa. Acha ujinga.
 
Libenna

Mapenzi ni msimamo! Unaonekana hujiamini na msimamo wako, amua moja tu. Unasimama na uliye naye au unarudi ulikopigwa chini simple tu kama hivyo mijadala mingine huwa haitakiwi kwenye mapenzi!!
 
Last edited by a moderator:
Libenna achana na huyo x tena katiza mawasiliano naye, tulia na Clara maana huyo x anataka tu kuganga majeraha halafu atasepa tena akishapona!!
 
Last edited by a moderator:
kuwa na msimamo! mambo ya bado unampenda yatakufanya ukose yote. tulia na huyo m-clara wako, huyo x mshauri apeleke tangazo jf connect
 
Penda pendwa, una ukakika gani hatakufanya spea tair tena akipata jamaa mwingine. Tulia na Clara wako mkuu. Kama anakuheshim na kukujali usigeuge nyuma.
Jasiri haachi asili....
 
Kitulize kihemuhemu chako kwa clara hiyo kuku nyingine tupa kule chaliagu, afu iambie itake mazoea yakuja home kabisaaaa
 
Acha tabia za kulia lia na kula matapishi...jiulize kwanza kilichomuondoa kwako hakitoweza kumuondoa tena? Kama aliweza kukuacha kwanini ashindww kukuacha tena?

Tulia wewe..mpende akupendae ..angekuwa ana kupenda wala asinge kuacha kwa sababu ya gari...!
 
ha ha ha kweli kizazi cha wanaume kinapotea... yani uliachwa bila sababu akatembea na mwarabu kamchakaza na wale jamaa kwa kupita uani hawajambo ha ha haha kashapasiwa huyo... basi sasa ni hivi ukirudiana nae jiandae kisaikolojia kuendelea kuachwa na kurudiwa tena na tena.... yaani bwana kitu unacho ndani lakini bado unaona vya nje unakimbizana navyo... HIVI KWELI UJAPATA FUNZO KWA HUYO MPENZI WA MWARABU ALIYEAACHWA ngoja nikufumbue ni hivi ALIKUACHA AKAENDA KWA MWARABU NA AAKAACHWA,, SASA NA WEWE UNATAKA KUMWACHA CLARA NA KWENDA KWA MPENZI ALIYEACHWA NA MWARABU JUA JIBU NI KUWA UTAACHWA HALAFU UJE URUDI KWA CLARA... ACHA UJINGA
 
Nakuja mbele zenu wana JF ushauri wenu ni muhimu sana,

Nilikua na mpenzi wangu, nilimpenda sana toka moyoni, awali tulipendana sana, watu kibao waliisifia relation yetu, nilijiona kua miongoni mwa wanaume wachache wenye bahati ya kupenda na wakapendeka.

Lakini huwezi amini, baada ya kama miezi 11 hivi ya mahusiano yetu, mpenzi wangu alianza kubadilika, nilijipa moyo kua huenda anatingisha kiberiti kunipima kama bado nampenda.

Daanh hapo ndipo akili ziliponifunguka, kumbe nilivokua najiona kua miongoni mwa wanaume wachache wenye bahati nilikua najidanganya kwa sababu licha ya kumfanyia kila kitu mpenzi wangu aliniacha, sikumkosea wala siku cheat, niliumia sana, nilikua nampenda sana, nilihisi nataka nife kwa jinsi nilivyompenda.

Nikiwa katika maumivu yangu yasiyo na hata lepe la ahueni, msichana mwingine akatokea kunipenda, anaitwa Clara, kumbe nyuma ya pazia huyu michana alikua best yake na msichana wangu wa zamani, awali nilimkataa huyu msichana sabu nilianza kuchukia mapenzi lakini kwa jinsi alivyonijali nikajikuta namkubalia.

Muda wote yule msichana wangu wa zamani alikua anatoka na jamaa mmoja wa kiarabu ambaye alikua ana hadi gari ya kutembelea ya mshua wake, so baada ya ujo jamaa kumtumia msichana wangu wa zamani na kumchoka, amemuacha.

Sasa alivopigwa chini ndo ameanza kunitafuta anadai bado ananipenda, mara nyingi anakuja hadi home kunitafuta, mimi bado nampenda lakini namheshimu sana Clara naogopa kumuumiza sabu ananisaidia mambo mengi, yani uwepo wake umenifaidisha na kunijenga sana kifikra na kila kitu.

Naombeni mnishauri wadau

waarabu wanatumiaga Sana 0713
 
ha ha ha kweli kizazi cha wanaume kinapotea... yani uliachwa bila sababu akatembea na mwarabu kamchakaza na wale jamaa kwa kupita uani hawajambo ha ha haha kashapasiwa huyo... basi sasa ni hivi ukirudiana nae jiandae kisaikolojia kuendelea kuachwa na kurudiwa tena na tena.... yaani bwana kitu unacho ndani lakini bado unaona vya nje unakimbizana navyo... HIVI KWELI UJAPATA FUNZO KWA HUYO MPENZI WA MWARABU ALIYEAACHWA ngoja nikufumbue ni hivi ALIKUACHA AKAENDA KWA MWARABU NA AAKAACHWA,, SASA NA WEWE UNATAKA KUMWACHA CLARA NA KWENDA KWA MPENZI ALIYEACHWA NA MWARABU JUA JIBU NI KUWA UTAACHWA HALAFU UJE URUDI KWA CLARA... ACHA UJINGA
Bora umemshauri ukiwa kama mwanamke naamin ujumbe atauelewa zaidi,,na kama manzi anakaribishwa nyumbani kama huyu jamaa ni dhaifu anaweza kuwa ashamla.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom