Ushauri huu kuhusu Wafadhili serikali imeutoa wapi?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,070
151,323
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la leo tarehe 05/04/2016, serikali imeajiri mshauri elekezi atakaeandaa mpango kazi kwa ajili ya kuwabana wafadhili wasiweze kujitoa katika ufadhili mara baada ya kusaini mkataba na serikali wa kutoa fedha za ufadhili.

Chanzo:Nipashe

Hakika hii misaada imetudumaza na tusidanganyane eti tunaweza kujitegemea kama hivi ndivyo tunavyowaza.

Hivi wakigoma kusaini nani mwenye hasara?!
 
Sasa hawa vijana wamiliki wa vyeti akina polepole mbona wanatuambia serikali yao haiitaji misaada? Kumbe wakubwa wamefikia hatua ya kufikiria kutunga sheria ya kung'ang'ania wahisani!!
 
Polepole mwenyewe asipopewa pesa hukaa kimya, kabuni mladi wa kula pesa za ccm kwa kisingizio cha kuwahujumu Ukawa.
 
Sasa hawa vijana wamiliki wa vyeti akina polepole mbona wanatuambia serikali yao haiitaji misaada? Kumbe wakubwa wamefikia hatua ya kufikiria kutunga sheria ya kung'ang'ania wahisani!!
Hapo ndipo wanaposhangaza na kudhihirisha unafiki wao.
 
Hata wao waliandika mikataba ya kupeana misaada sasa kama wamekiuka basi hata wakitunga za kuwabana bado itakuja kutubana coz hakuna anayetekeleza mikataba kiufasaha tatizo serikali haikuwa na mipango na mikataba zaidi ya kuwa na tamaa na ahadi nyng wkt hela za kuomba kutekeleza ilani za chama na c mikakati ya serikali ya maendeleo kifupi hatuna DIRA wala MALENGO tunaenda tu bora ifike kesho
 
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la leo tarehe 05/04/2016, serikali imeajiri mshauri elekezi atakaeandaa mpango kazi kwa ajili ya kuwabana wafadhili wasiweze kujitoa katika ufadhili mara baada ya kusaini mkataba na serikali wa kutoa fedha za ufadhili.

Chanzo:Nipashe

Hakika hii misaada imetudumaza na tusidanganyane eti tunaweza kujitegemea kama hivi ndivyo tunavyowaza.

Hivi wakigoma kusaini nani mwenye hasara?!
kujitegemea una maana gani? kama nchi gani?
 
Nawao watasainishwa watangaze matokeo ya uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 na wafute sheria ya mtandao. Mbona mshauri elekezi hapo atachemka kabla hajaelekeza
 
Jamani ombaomba kama wanaweza kutumia sheria kuwabana wanaorusha fedha kwenye kopo lao basi hayo yatakuwa maendeleo makubwa lakini si ya ulimwengu wa sasa maana hiyo ni hatua ambayo walioendelea wanakuwa wajinga na ombaomba waelevu sasa sijui kwa nini ombaomba hao wasitumie akili hizi kujitoa kwenye umasikini badala ya kudhani watafuta mbinu za kuwabana wafadhili.

ukimtishia mfadhili kumbana kwa sheria eti akiahidi asibadilishe kauli basi hatokuahidi tena, sio wajinga kiasi hicho cha kudhani tunaweza kupata misaada bila kupewa masharti.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la leo tarehe 05/04/2016, serikali imeajiri mshauri elekezi atakaeandaa mpango kazi kwa ajili ya kuwabana wafadhili wasiweze kujitoa katika ufadhili mara baada ya kusaini mkataba na serikali wa kutoa fedha za ufadhili.

Chanzo:Nipashe

Hakika hii misaada imetudumaza na tusidanganyane eti tunaweza kujitegemea kama hivi ndivyo tunavyowaza.

Hivi wakigoma kusaini nani mwenye hasara?!
 
Madhara ya elimu ya bure kumbe yalianza hata kabla ya elimu ya bure kuanza.Hivi mtu anakaa na vyeti vyake vyoote amejaza kwenye lumbesa anataka kutunga sheria ya kuwabana wahisani kweli! na wakati huo huo anawatangazia wananchi kwamba amejipanga vyakutosha wala hahitaji hiyo misaada na yuko tayari kujitegemea.
 
Hivi pesa za misaada ni kitu cha lazima. Msaada ni hiari ya yao huu ni upumbavu uliokithiri kutegemea misaada tena unataka kwa lazima huyo aliyakabidhiwa hii shughuli akili zake hapo sawa sawa hii ni aibu kubwa sana kuwa na viongozi wasio na maono.
Sasa nimeamini kwamba serikali hii imeishiwa pumzi hawana jipya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom