Ushauri: CHADEMA na NGO's waitishe maandamano ya amani kudai Katiba ya Warioba na Tume Huru ya Uchaguzi

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,848
Muda ni sasa, kesho ipo karibu sana na tutashtukia tayari 2025 hiyo. Hatuna Tume Huru wala Katiba mpya.

Kama tuna pesa za Mwenge wa Uhuru tunakosa vipi pesa ya kumalizia Katiba ambayo ipo tayari kwa 90%?

Kama tuna pesa za kufanya SENSA ya watu na makazi mwaka 2022 tunakosaje pesa ya kumalizia Katiba ya Warioba?

Naomba kutoa rai kwa Watanzania wote wapenda mabadiliko wakati ni sasa kipindi ambacho Mama ajajipanga na kukita mizizi kwenye urais wake tutoke vijana kwa maelfu tuandamane kwa amani kudai Katiba.

Takataka na uchafu wa yote yanayoendelea ni kutokana na nchi kukosa Katiba na mifumo iliyo imara.

Naomba CHADEMA na wadau wengine mnaotaka Tanzania kupiga hatua za kweli toeni tamko na mikakati ya kudai Katiba mpya ya Warioba kama bado haoni umuhimu wa kuwaita mezani mapema.

Tujifunze kudai vitu sio kupewa kwa hisani ya mtu.

Ukipewa atapewa credit ukidai na ukapewa utapewa credit.
 
Katiba mpya haileti umeme.
Katiba mpya haileti barabara.
Katiba mpya haileti maji.
Katiba mpya haileti madarasa.
Katiba mpya haileti ajira.

Wanaodai katiba mpya ni wanasiasa ili wapate upenyo wa kupata madaraka wapige hela.

Dubai ina katiba gani?
Kenya kilibadilika nini baada ya kupata katiba mpya tena ya mfano Africa nzima?

Tuchapeni kazi tupate maendeleo hakunaga shortcut ya maendeleo.
 
Muda ni sasa kesho ipo karibu sana na tutashutukia tayari 2025 hiyo hatuna tume huru wala katiba mpya.

Kama tuna pesa za Mwenge wa Uhuru tunakosa vipi pesa ya kumalizia katiba ambayo ipo tayari kwa 90%?..
Katiba ni ya nchi na ipo kwa manufaa ya kila mtanzania! Sasa kwa nini unategemea CHADEMA peke yao ndio wadai wakati wananchi wenyewe wametulia ndani wakiwa wameridhika na hali iliyopo?

Siku wananchi wa Tanzania, ambao hawajaonesha mpaka sasa kuguswa na mapungufu ya katiba iliyopo, watakapoona uhitaji wa Katiba Mpya, wataidai bila kusubiri kusukumwa au kushawishiwa na CHADEMA au NGO. Kwa sasa acha wananchi washangilie kwanza ujio wa Mama SSH.
 
Watanzania waandaliwe kisaikolojia kwanza, wafundishwe umuhimu wa Katiba Mpya na mapungufu yaliyopo kwenye hii Katiba ya sasa, wakielewa hili somo vizuri vuguvugu la kudai Katiba Mpya litakuwa kubwa zaidi na kuleta matokeo chanya.

Hakuna jambo litakalokuja hata kama ni zuri likakosa upinzani hasa toka kwa wale wanaonufaika na hii Katiba iliyopo, ni vyema kuwafunga midomo hao kwanza kwa kufungua akili za watanzania ili baadae kazi iwe moja tu ya kuidai Katiba Mpya.
 
Hayo yote yalishafinyika. Hatuwezi kuendelea kuwasaburi vilaza wote wasiojua umuhimu wa katiba imara yenye "checks and balances" za kutosha .
Watanzania waandaliwe kisaikolojia kwanza, wafundishwe umuhimu wa Katiba Mpya na mapungufu yaliyopo kwenye hii Katiba ya sasa, wakielewa hili somo vizuri vuguvugu la kudai Katiba Mpya litakuwa kubwa zaidi na kuleta matokeo chanya.

Hakuna jambo litakalokuja hata kama ni zuri likakosa upinzani hasa toka kwa wale wanaonufaika na hii Katiba iliyopo, ni vyema kuwafunga midomo hao kwanza kwa kufungua akili za watanzania ili baadae kazi iwe moja tu ya kuidai Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom