Ushauri: CCM tafuteni mtu makini wa kupambana na Bilionea Mbowe Hai, huyu mnayemtumia sasa Ole Sabaya ni sawa na kupoteza muda wenu bure

Mtu ambaye ni kapuku , mtu ambaye imethibitika kwamba umasikini wake umepelekea hadi kufoji nyaraka za Usalama wa Taifa ili atishe watu na kuwaomba rushwa ya kujikimu , mtu ambaye imethibitishwa mbele ya wakuu wa TRA kwamba anatumia mtutu wa bunduki kuomba rushwa ndogo hadi ya mil 2 za madafu , huyu hawezi kupambana na Tajiri Mbowe hata mkimkabidhi jeshi lote la polisi .

Freeman Mbowe atadhibitiwa kisiasa na mtu mwenye hoja za kisiasa aliyejaa utajiri wa wema na roho ya kibinadamu mwenye ushawishi , Mbowe ni jabali la kisiasa la nchi hii , huyu kauli zake ndio zinazotoa mwelekeo wa nchi , Mbowe ndiye dira ya Taifa , mipango yote ya kudhibiti siasa za nchi hii inapangwa baada ya Mbowe kuzungumza , Jabali kama hili haliwezi kutishwa na kijana mdogo asiye na kitu kama huyu Sabaya , na akiendelea na siasa za kishamba kutoka kwa wanaomtuma atakuja siku moja kukutwa mlangoni kwa Mbowe kapiga goti kuomba msamaha .

Kwa ufupi sana huu ushauri ninaowapa muuzingatie , Majuto ni mjukuu
Mkuu uliona mbali....
 
Huyu askari kada wa ccm yupo wapi siku hizi.
Ashuhudie sabaya akila mvua
 
Back
Top Bottom