USHAURI: CCM ijipange upya kwa kuwafungulia Vijana uongozi wa juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: CCM ijipange upya kwa kuwafungulia Vijana uongozi wa juu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Dec 1, 2010.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Baada ya kipigo katika uchaguzi uliopita, Wachambuzi wengi wa Kisiasa, wanaishauri Chama Tawala CCM kuwakamata mapema Vijana SAFI ambao wanaonyesha Uwezo wa Uongozi na ambao wanakubalika. Majina Machache ambayo yatakuwa Chachu ya Jamii na moto wa kuotea mbali kwa Wapinzani ni kama Jeri Silaa, John Mashaka, Shy-Rose Banji, Bashe, Pamoja na Nape Nauaye.

  January Makamba angewekwa kwenye hili kundi lakini kujiingiza kwake kwenye mambo makubwa ya kifisadi kunamfanya awe ni mtu ambaye hataweza kukubalika na atazidisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama, hasa ukizingatia kwamba analo jina la Makamba

  Hawa ni vijana makini mno, ambao kama CCM haitaweza kuwakimbilia mapema na kuwapa nafasi nyeti katika uongozi, basi wataangukia mikononi mwa Wapinzani. Wakidhania kwamba walipigwa katika uliopita, basi wasubiri 2015 wakione cha Moto kutoka Upinzani chini ya John Myika na Halima Mdee... Zitto Kabwe amekwisha kutokana na ulafi na unafiki wake. Yeye amekwisha kisiasa, kwanza hauna uwezo wa kifikra zaidi ya kuropoka

  Ikiwa kuna majina makubwa ambayo nitakuwa nimeyaacha nyumba, kunradhi. mnaruhusiwa kuyaongeza !
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  ccm wapo saturated! hawahitaji ushauri wowote. kama ni ushindi kwenye uchaguzi mbona mbinu zipo nyingi sana, ukiachana na ile waliyotumia mwaka huu ya uchakachuaji.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nani huyumshauri? Anajua vizuri majukumu yake?
   
Loading...