USHAURI: CCM ijipange upya kwa kuwafungulia Vijana uongozi wa juu

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Baada ya kipigo katika uchaguzi uliopita, Wachambuzi wengi wa Kisiasa, wanaishauri Chama Tawala CCM kuwakamata mapema Vijana SAFI ambao wanaonyesha Uwezo wa Uongozi na ambao wanakubalika. Majina Machache ambayo yatakuwa Chachu ya Jamii na moto wa kuotea mbali kwa Wapinzani ni kama Jeri Silaa, John Mashaka, Shy-Rose Banji, Bashe, Pamoja na Nape Nauaye.

January Makamba angewekwa kwenye hili kundi lakini kujiingiza kwake kwenye mambo makubwa ya kifisadi kunamfanya awe ni mtu ambaye hataweza kukubalika na atazidisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama, hasa ukizingatia kwamba analo jina la Makamba

Hawa ni vijana makini mno, ambao kama CCM haitaweza kuwakimbilia mapema na kuwapa nafasi nyeti katika uongozi, basi wataangukia mikononi mwa Wapinzani. Wakidhania kwamba walipigwa katika uliopita, basi wasubiri 2015 wakione cha Moto kutoka Upinzani chini ya John Myika na Halima Mdee... Zitto Kabwe amekwisha kutokana na ulafi na unafiki wake. Yeye amekwisha kisiasa, kwanza hauna uwezo wa kifikra zaidi ya kuropoka

Ikiwa kuna majina makubwa ambayo nitakuwa nimeyaacha nyumba, kunradhi. mnaruhusiwa kuyaongeza !
 
ccm wapo saturated! hawahitaji ushauri wowote. kama ni ushindi kwenye uchaguzi mbona mbinu zipo nyingi sana, ukiachana na ile waliyotumia mwaka huu ya uchakachuaji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom