Ushauri: Bundle ya Voda Internet Yanifanyia Uhuni

Ushauri: Bundle ya Voda Internet Yanifanyia Uhuni

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Enyi wataalamu wa tech gadgets, Nawasalimu wote!
Kwa mahitaji yangu ya internet, nanunuaga bundle ya voda ya siku moja (masaa 24) kwa sh 700 kwa mb 100. Inaanza vizuri masaa ya mwanzo lakini inapotimia masaa 21 au 22 hivi uhuni unaanza. Ama nitapata meseji kwamba huduma imeisha au hutoweza ku-access webpage yoyote. Mara nyingi ninapojiunga na huduma hii, ninaingiza vocha ya elf moja na kubakiwa na mia tatu. Ajabu ni kwamba ninapoambiwa huduma imeisha kabla ya masaa 24 kuisha, hata zile 300 zilizobaki nazo huyeyuka! Nawaomba muungane na mimi kuishangaa huduma ya internet ya voda kwenye bundle ya sh 700 mb 100, unless pengine kuna mwenye maelezo/ushauri wa nini kinatokeaga.
 
sasa si umemaliza mb zako mkuu? Au unafkiri ukiambiwa 24 hrs basi ndo haiishi.
 
Hapo bundle ilikwisha, na hizo 300 zimekatwa kwa kuwa umezitumia baada ya 100mb kuisha tu
 
jifunze kutumia mpesa mkuu. unapotaka kujiunga asubuhi, unavuta vocha ya mia saba via mpesa.. becoz hawa voda ni wahuni, ila sio kama unavyodhani.. what they do ni kuwa as long as una vocha kwenye line yako, hawakushtui kuwa umemaliza bundle yako. ni mpaka vocha ikate yote. ukiweka hata buku kumi, watailamba yote then ndo wakuambie bundle imekata. tangu nigundue hilo nimehamia vocha za mpesa 100% as wana ofa nyingi nzuri lakini ndo hivyo na kulamba vocha za watu
 
hahaha!!!! Skuiz option Nyingi Ukipenda Kuisave Hio 300 uwe unanunua bundle kwa line tofaut!!! Mfano unaweka vocha Kwa Mtu wa Karibu Then Unapiga *149*01# chagua INTERNET .. then Chagua Buy Internet For A Friend Jaza namba then weka kias... Then Click 1 kukubali ... Hapo utakua Umemalizaaaa
 
jifunze kutumia mpesa mkuu. unapotaka kujiunga asubuhi, unavuta vocha ya mia saba via mpesa.. becoz hawa voda ni wahuni, ila sio kama unavyodhani.. what they do ni kuwa as long as una vocha kwenye line yako, hawakushtui kuwa umemaliza bundle yako. ni mpaka vocha ikate yote. ukiweka hata buku kumi, watailamba yote then ndo wakuambie bundle imekata. tangu nigundue hilo nimehamia vocha za mpesa 100% as wana ofa nyingi nzuri lakini ndo hivyo na kulamba vocha za watu

Asante leh;5619700. Umenielewesha vizuri sasa nshajua jinsi ya kukwepa uhuni wao!
 
Last edited by a moderator:
Leo voda wako vizuri!
Hata tuliomadongo kuinama tunapata reception nzuri, sio bar 1 na 2 tu. Leo reception ya uhakika tena wala haikatikikatiki. Nafikiri wapo kwenye maboresho, kwani nimepewe siku 7 free za kutumia internet. Angalao walipie siku nilizokuwa napata taabu ya reception.
 
angalia upload + download kama vyote ukivijumlisha vikafika mia au hata 90 NA kitu mwisho
 
Hakuna uhuni hapo, ni kwamba umemaliza hiyo 100MB na umeanza kukatwa kwa pay as you go. Hiyo 24 hours ni kwamba bundle inaexpire baada ya siku moja hata usipoitumia.
 
Ahsanteni kwa kumjibu mwenzetu lakini sikuona mtu aliyemsaidia jamaa kuwashangaa voda acha mi nitekeleze wajibu E e e e e e jamani jamani nini hiki.
 
Leo voda wako vizuri!
Hata tuliomadongo kuinama tunapata reception nzuri, sio bar 1 na 2 tu. Leo reception ya uhakika tena wala haikatikikatiki. Nafikiri wapo kwenye maboresho, kwani nimepewe siku 7 free za kutumia internet. Angalao walipie siku nilizokuwa napata taabu ya reception.

Hapo uongo pia nimepata msg hiyo ila kukatwa vocha kama kawa mwana nimeshanunua mara mbili bundle za 700 pamoja na hiyo msg yao.
 
Hapo uongo pia nimepata msg hiyo ila kukatwa vocha kama kawa mwana nimeshanunua mara mbili bundle za 700 pamoja na hiyo msg yao.
Basi unajua, wewe umefanya haraka kuweka vocha. Nafikiri ukiweka vocha wanalamba kama kawaida, mimi bundle yangu imeisha leo ila nikangoja mpaka ikate. Badala ya kukata ndio nikaona ofa yao, na kama unavyoona bado nadunda. Labda kama haitafika siku 7, ngoja nione.
 
jifunze kutumia mpesa mkuu. Unapotaka kujiunga asubuhi, unavuta vocha ya mia saba via mpesa.. Becoz hawa voda ni wahuni, ila sio kama unavyodhani.. What they do ni kuwa as long as una vocha kwenye line yako, hawakushtui kuwa umemaliza bundle yako. Ni mpaka vocha ikate yote. Ukiweka hata buku kumi, watailamba yote then ndo wakuambie bundle imekata. Tangu nigundue hilo nimehamia vocha za mpesa 100% as wana ofa nyingi nzuri lakini ndo hivyo na kulamba vocha za watu
mdau hebu nielekeze fresh kuhusu ununuzi wa m-pesa
 
Hapo uongo pia nimepata msg hiyo ila kukatwa vocha kama kawa mwana nimeshanunua mara mbili bundle za 700 pamoja na hiyo msg yao.
VODA WANACHAKACHUA SANA,WE FIKIRIA UNANUNUA YA WIKI,NA WALA HAUDOWLOAD ILA UNATUMIA SIKU 2,MXIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII:shut-mouth::angry:,,,,
 
hamna kuchakachua ni uelewa wako tu. Kama unanunua bundle ndogo then huna means zozote za kuimanage unategemea nini?
 
mdau hebu nielekeze fresh kuhusu ununuzi wa m-pesa

mkuu, ni simples sana. (nitatumia picha za dashboard ya voda kwa PC ila ni sawa tu na simu na ninategemea una password ya m-pesa yako)

kwanza unapiga *150*00#
mpesa1_zpscf3bfc82.jpg

unachagua namba 3. Buy airtime

mpesa2_zpsf146d424.jpg

unachagua 1.my phone

utapewa option ya kiasi Enter Amount, unaweka salio (700)

mpesa3_zps07153b65.jpg

utawaweka PIN yako sasa (password)

hakikisha and umemaliza!!

mpesa5_zps5dabb490.jpg

simpleee
 
Hawa wamekuwa Wizi kila siku mimi wananiibia SMS Na zile Dak 15 hata ukiwapigia CC Yao hawana responds nzuri inawezekana kuna baadhi ya wafanyakazi wao upande wa ufundi sio waaminifu wezi maana wao wanakuwa ni Super User anaweza kuingia kwenye number yoyote
 
jifunze kutumia mpesa mkuu. unapotaka kujiunga asubuhi, unavuta vocha ya mia saba via mpesa.. becoz hawa voda ni wahuni, ila sio kama unavyodhani.. what they do ni kuwa as long as una vocha kwenye line yako, hawakushtui kuwa umemaliza bundle yako. ni mpaka vocha ikate yote. ukiweka hata buku kumi, watailamba yote then ndo wakuambie bundle imekata. tangu nigundue hilo nimehamia vocha za mpesa 100% as wana ofa nyingi nzuri lakini ndo hivyo na kulamba vocha za watu

hata wenye android tunalia sana nahuu uhuni, tena wanasubiri hadi wamalize na zile pesa zako ndio wanatuma msg lao la kumaliza mb
 
Kama una Android nenda Play Store install apps inaitwa My Data Manager ina uwezo was kupima matumizi yako na kukutaarifu unapozidi bundle, unakuwa unajua kabla haijaingilia credit yako.
 
Back
Top Bottom