carmel
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,836
- 262
Tafadhali wana jamvi, nauliza kuhusu biashara ya dry cleaning, yani kwa mtu mwenye mtaji basic tu wa kuanzia, ina weza kucost shilingi ngapi? Na pia inalipa? Tfadhali, naombeni mawazo yenu maana sina idea yoyote kabisa.
Thanks
WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUELEWA BIASHARA HII
Wakuu, nataka kufanya biashara ya dry cleaning. Naomba kujua kwa mjuvi wa biashara hii anisaidie kunipa taarifa ni vitu gani nahitaji ili niweze anza.
Msaada wenu unahitajika great thinkers
OTIS
The Illuminati
Hello wadau!
Nataka kuanzisha biashara ya dry cleaning somewhere in this country lkn nataka kuanza kwa small scale ili kutest biashara!nataka kujua mtaji kiasi gani ambao unaweza kuhitajika kwenye hiyo bussiness pia ni machine gani ambazo natakiwa kuwa nazo!na hz machine zinaweza kucost sh ngapi na zinapatikana nchini au mpk niagize na km kuagiza wakina nani ni reliable suppliers.
Natazamia kufungua biashara ya kufua nguo kwa hiyo nahitaji mashine kwa kazi hiyo. Tafadhali naomba mwenye kujua bei zake na mahali kwa kuzipata anipe taarifa.
Mashine ni kama zifuatazo
1. Dry cleaning machine (16kg)
2. Packaging Machine
3. Ironing table - aspiration with boiler, height adjustable
4. Stain removing machine
5. Industrial washing machine (16kg) - for blankets etc
6. Wringer (8kg)
7. Domestic washing machine
8. Semi-silent compressor
Natanguliza shukrani
Habari wakuu,
Nataka kuanzisha biashara yakufua nguo kwa mashine (dry cleaner) Naomba mwenye uzoefu wa hii biashara anipe maufundi kidogo yavitu kama, mtaji, faida naipaje pamoja na changamoto zake.
Shukrani.
MICHANGO NA USHAURI WA BAADHI YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
UKWELI KUHUSU BIASHARA HII
Assumption - Unaangalia uwezekano wa kuanzisha hiyo biashara Dar.
Kulipa kwake kutategemea na nguvu za kiasi gani utawekeza kwenye kuiba wateja wa drycleaning ambazo tayari zina majina. Kuna mlolongo wa drycleaning stores jijini ambazo zimeshakamata sehemu na wateja muhimu wa hiyo huduma.
Hii biashara ni moja ya biashara ambayo soko la ukua polepole sana. Hii ina maana kiwango cha namba ya wateja wapya kujiingiza kwenye uhitaji wa huduma hii ni ndogo sana. Hii inatokana na kuwa, huduma hii bado inaangaliwa kama huduma ya 'anasa' kwa asilimia kubwa ya watu. Kwa hiyo, utakuta asilimia kubwa ya wateja ni hao hao miaka nenda miaka rudi.
Hivyo basi, ili uweze kufanikiwa, itakubidi usuke mbinu za kuwaiba wateja wa drycleaning zingine. Kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu sana ukizingatia kuwa hizo drycleaning zimekuwa karibu sana kiuhusiano na wateja wao kiasi kwamba ni vigumu kwa wateja hao kuzikimbia.
-o-o-o-o-o-
Sasa basi, kuangalia upande mwingine wa shillingi, hii biashara inaweza kufanikiwa kama utajaribu kuongeza upana wa biashara yenyewe. Unachoweza kufanya ni kuweka mashine za self-service.
Yaani pamoja na kutoa huduma ya drycleaning, pia unaweka washers na dryers kwa wateja ambao wangependa kuosha nguo zao wenyewe. Kitakachotokea wateja watakuja na nguo zao, wataziosha, watazikausha, na kuondoka nazo papo hapo.
Wewe unachofanya ni kuwachaji gharama za utumiaji wa mashine zako tu. Mfano, unaweza kuwachaji load moja kwenye washer inagharimu kiasi kadhaa, na dyer kiasi kadhaa. Au ukaweka chaji moja kwenye combination ya utumiaji wa washer na dryer moja.
Vitu vinne muhimu vya kuzingatia kwenye self-service hii ni:
1) Kuhakikisha gharama za utumiaji wa mashine ni nafuu kuliko za drycleaning.
2) Kunakuwa na maji na umeme wa uhakika
3) Kuziweka hizo mashine katika hali ya usafi muda wote
4) Kuna usimamizi wa utumiaji wa hizo mashine ili zisiharibiwe na waharibifu
Well, ningependa kugusia suala la maji na umeme. Kama hii huduma ikichanganya, basi ujue kuwa itakugharimu maji na umeme zaidi kuliko kodi ya fremu. Kwa hiyo itabidi ujiandae vilivyo kwenye hivyo vitu viwili. Na kama unavyojua, maji na umeme ni matatizo sugu ambayo yako kwenye top 5 nchini mwetu. Na hiyo biashara bila ya hivi vitu viwili haiendi. Unajua hilo! Kwa hiyo, utakubidi uweke matanki na jenereta za kutosha.
Pia, itakubidi uwe mwangalifu kwenye suala la usafi wa maji. Kama unavyojua, maji ya dar ni maji tope. Kwa hiyo, ili usijekujikuta na lundiko la malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu nguo zao kuchafuka zaidi (badala ya kusafishika), itakubidi utafute njia ya kuya-filter hayo maji. Nafikiri wizara ya maji ina ma-engineers ambao wanaweza kupatia mbinu ya ku-filter maji.
~~
ENEO NI MUHIMU. PUNGUZA GHARAMA ZA UENDESHAJI
Bado unaweza kuanza, kimkakati - mkoani sidhani kama italipa.
Kama upo Dar chagua eneo moja la kuhudumia kwa mfano vyuoni ukaanzania Mlimani ukaunganisha na vyuo vya jirani au nenda kwenye hostels kubwa kubwa. Hauhitaji kufungua duka ila unatakiwa kununua bajaj moja kuifanya kuwa duka la kutembea. Bajaj yako jaribu kuijengea ka-body and then tenga sehemu mbili; upande mmoja ya kuchukulia nguo chafu na upande wa pili kuchukulia nguo safi zinazorudishwa.
Kwa kuanza huhitaji mashine, ili kukupunguzia gharama za uendeshaji. Ajiri watu wawili wa kufua na mmoja wa kunyoosha na ku-pack nguo vizuri. Kazi hizi unaweza kuzifanya kutokea nyumbani (kama haukupanga chumba). Maji Dar ni mgao itakubidi kununua tank la kuhifadhia maji, ukipata ya kubeba lita 5000 itafaa sana. Ajiri mlinzi mmoja kukuangalizia nguo zilizoanikwa.
Hii ni biashara kama zingine hakikisha unapata vibali na kujitambulisha kama mlipa kodi ili kuhalalisha shughuli zako. Tafuta label yako ya kukutambulisha eg DOWANS Laundry Services. Label na contact zako zote ziweke kwenye bajaj, zing'arishe kadri utakavyoweza. Kazi kubwa utakayofanya mwanzo mwanzo ni kutambulisha biashara (promotion) na kazi hii itabidi uifanye bila kuona aibu. Kwa huo mtaji nakushauri kazi ya promotion ufanye mwenyewe na jinsi hiyo itakubidi pia uwe dereva bajaj.
Nakutakia mafanikio mema.
WAWEZA KUANZA NA MASHINE NDOGO. HAKIKISHA OFISI INAVUTIA
Mayu nataka nikutie moyo kuwa unaweza kabisa kufungua hiyo biashara kwa huo mtaji wako wa m7 (nahisi ni hela yako ya uhamisho ).
Chakufanya kwanza anza na mashine ndogo ya wastani najua mkoani wateja mwanzo hawatakuwa wengi kivile, nunua washing mashine ya kama m1 hadi m2, inatosha sana kwa kufulia nguo za kawaida kama mashati, suruali, magauni, sketi, bauzi.pia mashuka, mapazia,nk.
Makoti hayafuliwi na washing mashine yana utaratibu wake wa ku dry clean, waweza tafuta kuna dry cleaner simple kwa aajili ya kusafishia makoti manual.
Pia tafuta mshine ya kusafishia makarpet ya kama lk5 inatosha sana nahii unaweza kuwafuata wateja hata majumbani si lazima walete ofisini.
Cha umuhimu tengeneza ofisi kali inayovutia nje na ndani, weka muudumu smati hakikisha unatoa muda sahihi kwa mteja kuja kuchukua nguo zake.
Hakikisha unapata mifuko ya plastiki na enga simple kuwekea nguo za wateja.
Siku za mwanzo uwe kipromotion zaidi kwa kutoa viofa vya hapa na pale mfano, mteja kaleta nguo kumi basi mbili mwambie unamfanyia free.
Mikoani kuna tv cable zinafanya matangazo bei powa sana, peleka matangazo,tengeneza vipeperushi vizuri jisifie sana kuwa unafua kutumia mashine na utaalamu wa kisasa zaidi.
Kaunta ukiweza weka ka pc pale, feed kila kitu ili uwe unatoa risiti nk utaonekana makini na smati zaidi.
Hakikisha at start zoezi unalisimamia wewe mwenyewe na hakikisha customer care ndio silaha yako no moja.
Jitahidi upate ofisi sehemu nzuri kama katikati ya mji, unahitaji ofisi kwa maana ya sehemu ya kupokelea na kutoa nguo, hii ndio inayohitajika iwe ya viwango.
Pia unahitaji sehemu ya kufulia na kuanikia hii inaitwa factor, hapa inaweza kuwa hata nyumbani kwako kama utakosa sehemu utakayoshindwa kuigawa ofisi na factory.
Pia kuwa mjanja si kila mara uwe unatumia washing mashine wakati mwingine tumia watu wako kufua kawaida labda kwa nguo maalum.
Google namna mbali mbali za kufua aina mbali mbali na kupiga basi even how to dry clean suit nk jifunze mwenyewe kisha wafundishe watu wako na wasimamie.
Mwisho nakutakia kila la heri ndugu yangu na usisite kurudi ukumbini kutujuza yaliyojiri
VIFAA VINAVYOHITAJIKA KATIKA BIASHARA
Mashine zinazohitajika kwa kuanzia ni kama zifuatazo, (ingawa itategemea hasa mtaji ulionao na aina ya huduma unazotarajia kutoa)
1. Dry cleaning machine - 16kg kwa kuanzia inatosha kwa population ya watu 40,000
View attachment 42877
2. iIroning table - aspiration with boiler (height adjustable)
View attachment 42878
3. Stain removing machine
View attachment 42879
4. Packaging machine
View attachment 42880
5. Industrial washing machine (16kg inafaa kuanzia) - hii ni mashine kwa ajili ya kufulia mablanketi nk
View attachment 42881
6. Domestic washing machine (16kg)
View attachment 42882
7. Wringer (8kg) - kwa ajili ya kukausha nguo
8. Compressor
View attachment 42886
9. Computer equipment (cash register, ticket printer etc)
10. Clothes rack - kwa ajili ya kuning'iniza nguo - hii unaweza itengeneza kwa kutumia local materials hapo hapo dukani