Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 142,795
- 287,769
Nafahamu kwamba ni vigumu kuwaondoa wamachinga , maana kwa mila za kiafrica mkubwa akisema sisi vidagaa ni lazima tutiii, mkubwa hakosei, Bali sasa iko wazi kabisa kwamba kuchanganya Magari na Wamachinga ndani ya barabara hiyo ni wazi kutasababisha mauaji makubwa sana, ama Wamachinga wataua Dereva aliyekanyaga kandambili au biscuti zao au dereva ataua mamia ya Wamachinga, ambao baada ya ruhusa hii mpya wameamua kuitumia barabara yote kuuzia mitumba .
Tuwe wakweli, tuzuie magari kutumia barabara ya msimbazi , tuache mabasi ya " wakubwa " ya mwendokasi, maana uchunguzi wangu unaoenyesha kwamba barabara yanayopita mabasi hayo angalau inaheshimiwa kwa 40%.
Majuto ni mjukuu .
Tuwe wakweli, tuzuie magari kutumia barabara ya msimbazi , tuache mabasi ya " wakubwa " ya mwendokasi, maana uchunguzi wangu unaoenyesha kwamba barabara yanayopita mabasi hayo angalau inaheshimiwa kwa 40%.
Majuto ni mjukuu .
Baada ya kauli ya Rais Magufuli ya kutaka wamachinga wasisumbuliwe, hali imekua mbaya Kariakoo kuna msongamano mkubwa mnoo unaotishia usalama wa pesa za wanaoenda kufanya manunuzi mbalimbali.
Serikali iangalie upya sehemu ya kuwapeleka hawa ndugu zangu ingawa si wote kutoka "Ntwala" Kariakoo sasa hivi imekua kero bidhaa zimemwagwa kila kona hata kutembea imekua shida unachechemea kukwepa biashara za watu.