Ushauri: Anadai mtoto ni wa kwangu

shukran mkuu ila tatizo yeye analazimisha niwe karibu na mtoto wakati kwangu naona ni hatar sana ananiforce nimuweke kwenye mtandao kumuwish birthday dah hapo panakuwa magumu
Itakuwa mizimu ya kwenu inamsumbua sana, fanya mpango umuone tu mtoto
 
Muulize mamaako nin cha kufanya. Akina mama wana mipango mkakati ambayo huwez hata kufikiria
mkuu kumshirikisha bi mkubwa katika huu upuuzi ni ujinga wa kiwango cha lami na bado sijafikia uko bado niko katika barabara ya vumbi
 
Habari za jioni wana JF,

Mwenzenu nina mtihaani ambao unanisumbua,

Kuna binti mmoja niliwahi kuwa na mahusiano naye na mwishoni siku akaolewa, kutokana na mimi kutokuwa na mwelekeo wa maisha.

Ila karibia anaolewa aliniletea mzigo na nikapiga kama kawaida, kama kuagana na kuniahidi mambo mengi kwamba kinachompeleka kule ni maisha tu na akipata uko basi nami atanitoa.

Aliniambia mimi ndio chaguo lake na siku mmoja akifanikiwa angerudi kwangu na kuishi pamoja baada ya kuchoma mali kwa mshefa, nilimkubalia kwa shingo upande japo moyoni nikijua fika aninifariji tu, basi tukapiga game siku ile tukaachana, baada ya wiki akaolewa na kwenda kuishi kwa mumewe ambapo ni mji mwingine.

Baada ya ndoa kupita mawasiliano yakakata maana hata namba alibadilisha, niliumia sana na kuhisi kuhadaiwa, nilijiona mjinga na lofa niliyekubali kirahisi kuhadaika, baada ya mwaka na kitu kupita yule binti alinitafuta na kufanikiwa kunipata, nachakushangaza hicho alichokuja kuniambia kuwa mtoto aliyenae kuwa ni wa kwangu.

Nilistaajabu sana sikutaka kuamini kirahisi ila alinionyesha picha ya mtoto na nikamuona kweli alikuwa amefanana na mimi na pia hata mwanangu ambaye nimezaa na mke wangu baada yeye kuniacha maana niliamua kuoa, akaniomba ni mjue yule mtoto kama navyojua huyu mtoto niliyezaa na mke wangu, pia napata tabu maana saivi imekuwa kero anataka hata akiumwa niende nikamuone hosptal.

Nashindwa maana tiyari yeye mke wa mtu na hata kama mtoto ni wangu ila alishampa mtu mwingine na pia anajulikana kwa ubini wa uyo jamaa na pia hata mwenye hataki watu wengine wajue kama ni mwanangu zaidi ya yeye na mimi, nashindwa nifanyeje, plz wanajamii nisaidieni mawazo maana ananisumbua sana huyu mtu naona maisha yangu yako hatarini?

Kipi nifanye?


Matusi, kejeli sitaki kama huna cha kunshauri pita kule, kila mtu anakosea katika maisha hakuna mkamilifu.
Mhh kuna wanawake wanavimbwanga hatari sasa huyu nae anaakili timamu kweli?
 
Shimo la tewa linakuita.. Stop being a boy.. Be a man..

Hapo anakuvuta tu umpe wa pili

Jamaa angu kafikisha watatu.. Kwa staili hyo.. And simply mwanamke akamjibu kuwa hakutaka kuzaa na Wanaume tofauti.. Japo kaolewa mimba zote kabeba kwa mchizi..
Be careful with that woman
 
Shimo la tewa linakuita.. Stop being a boy.. Be a man..

Hapo anakuvuta tu umpe wa pili

Jamaa angu kafikisha watatu.. Kwa staili hyo.. And simply mwanamke akamjibu kuwa hakutaka kuzaa na Wanaume tofauti.. Japo kaolewa mimba zote kabeba kwa mchizi..
Be careful with that woman
Duh hatar yaan apa ntakaa nae mbali kabisa mita 90 kama za kipindi kile cha uchaguzi
 
mkuuu icho ndo kinanifanya nasita na kumpotezea ila cha ajabu huwa ananitafta hata nibadilishe namba basi ataipata maana nimehama mji ila cha ajabu kajua nilipo na ananiambia yeye shida yake niwe karibu na mtoto tu
Acha upuuzi wewe, mwanaume unabadilishaje namba? Jisimamie huyo malaya mwambie ana mume wake akukome na akiendeleza huo umalaya wake taarifa zitamfikia mumewe na kama hawezi Lea huyo mtoto basi amlete umlee wewe na asikusumbue kwa namna yoyote alichagua mwenyewe fungu la kukosa sasa asikusumbue. Ningekuwa mimi akiniita hospital kumwona mtoto Nampa kipigo namwita mumewe na mwanangu namchukua. Mianamke mingine ni mipoyoyo kabisa kama hilo haijawahi kuwa na akili timamu, yaani ndoa kwake ni kitu rahisi kweli sasa ngoja liachike lizae na kila mwanaume mtaani. Sorry wewe na hilo jike malaya wote inaonekana dish limeyumba mbayaaa
 
Kaeni chini mweleze ukweli wa unachohofia juu ya ukaribu wake na yeye kwa sasa, akishindwa kukuelewa tafuta wazee wakushauri nini cha kufanya
 
Alileta mzigo ukapiga kama njia ya kuagana. Sasa anakuletea mtoto kama njia ya kukumbukana.

Elewaneni tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom