Ushauri: Anadai mtoto ni wa kwangu

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,637
2,000
Habari za jioni wana JF,

Mwenzenu nina mtihaani ambao unanisumbua,

Kuna binti mmoja niliwahi kuwa na mahusiano naye na mwishoni siku akaolewa, kutokana na mimi kutokuwa na mwelekeo wa maisha.

Ila karibia anaolewa aliniletea mzigo na nikapiga kama kawaida, kama kuagana na kuniahidi mambo mengi kwamba kinachompeleka kule ni maisha tu na akipata uko basi nami atanitoa.

Aliniambia mimi ndio chaguo lake na siku mmoja akifanikiwa angerudi kwangu na kuishi pamoja baada ya kuchoma mali kwa mshefa, nilimkubalia kwa shingo upande japo moyoni nikijua fika aninifariji tu, basi tukapiga game siku ile tukaachana, baada ya wiki akaolewa na kwenda kuishi kwa mumewe ambapo ni mji mwingine.

Baada ya ndoa kupita mawasiliano yakakata maana hata namba alibadilisha, niliumia sana na kuhisi kuhadaiwa, nilijiona mjinga na lofa niliyekubali kirahisi kuhadaika, baada ya mwaka na kitu kupita yule binti alinitafuta na kufanikiwa kunipata, nachakushangaza hicho alichokuja kuniambia kuwa mtoto aliyenae kuwa ni wa kwangu.

Nilistaajabu sana sikutaka kuamini kirahisi ila alinionyesha picha ya mtoto na nikamuona kweli alikuwa amefanana na mimi na pia hata mwanangu ambaye nimezaa na mke wangu baada yeye kuniacha maana niliamua kuoa, akaniomba ni mjue yule mtoto kama navyojua huyu mtoto niliyezaa na mke wangu, pia napata tabu maana saivi imekuwa kero anataka hata akiumwa niende nikamuone hosptal.

Nashindwa maana tiyari yeye mke wa mtu na hata kama mtoto ni wangu ila alishampa mtu mwingine na pia anajulikana kwa ubini wa uyo jamaa na pia hata mwenye hataki watu wengine wajue kama ni mwanangu zaidi ya yeye na mimi, nashindwa nifanyeje, plz wanajamii nisaidieni mawazo maana ananisumbua sana huyu mtu naona maisha yangu yako hatarini?

Kipi nifanye?

Matusi, kejeli sitaki kama huna cha kunshauri pita kule, kila mtu anakosea katika maisha hakuna mkamilifu.
 
ArD67

JF-Expert Member
Nov 14, 2016
2,821
2,000
Chukulia poa tu, ni mwanao asiyekuja kujulikana daima, mchukulie hivyo. Kwakuwa umeshaoa na ukilianzisha litawakost wote, atachika nawe utaachika na mkeo na kuwasumbua watoto. Ila kama ulikuwa na idea kuhusu malezi ya wanao, shea nae amlee hivyo, itakupunguzia maumivu na akikuwa mfanye kuwa Best anko wako.
 
Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,637
2,000
ndo maana mimi natafuta bikira mariam hizi za kuokota okota mi sipendi ila basi tuuu hamna namna.

sina cha kukushauri ila angalia mke wa mtu ujue unatembea na bomu shauri yako
mkuuu icho ndo kinanifanya nasita na kumpotezea ila cha ajabu huwa ananitafta hata nibadilishe namba basi ataipata maana nimehama mji ila cha ajabu kajua nilipo na ananiambia yeye shida yake niwe karibu na mtoto tu
 
Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,637
2,000
Chukulia poa tu, ni mwanao asiyekuja kujulikana daima, mchukulie hivyo. Kwakuwa umeshaoa na ukilianzisha litawakost wote, atachika nawe utaachika na mkeo na kuwasumbua watoto. Ila kama ulikuwa na idea kuhusu malezi ya wanao, shea nae amlee hivyo, itakupunguzia maumivu na akikuwa mfanye kuwa Best anko wako.
shukran mkuu ila tatizo yeye analazimisha niwe karibu na mtoto wakati kwangu naona ni hatar sana ananiforce nimuweke kwenye mtandao kumuwish birthday dah hapo panakuwa magumu
 
Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,637
2,000
hapa ndio unapojua kuwa wanaume wengi wanalea watoto wasio wao........

kwani wewe unataka nini haswa....
mimi nataka namna ya kumwepuka maana anahatarisha maisha yangu maana inavyoonekana hajali usalama wangu na kila navyojaribu mkwepa au kuhama basi anapajua tu
 
Da Lu

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
929
1,000
Duuuh maisha haya sijui hata niandike vp ila huyo dada anachokitafuta atakipata
 
ArD67

JF-Expert Member
Nov 14, 2016
2,821
2,000
shukran mkuu ila tatizo yeye analazimisha niwe karibu na mtoto wakati kwangu naona ni hatar sana ananiforce nimuweke kwenye mtandao kumuwish birthday dah hapo panakuwa magumu
Mara nyingi kwenye michezo ya hatari tuichezao na hao viumbe lazima tuwashikie akili zao vinginevyo watakupeleka shimoni.
 
UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
2,334
2,000
Hayo mbona hata Mimi yalinikuta ila nilimwambia kitu kimoja TU kwamba akifikisha miaka kumi anitafute nitajua nifanye nini na hata siwezi kusogelea huko kwake coz Mtoto ni copy yangu
 
ArD67

JF-Expert Member
Nov 14, 2016
2,821
2,000
shukran mkuu ila tatizo yeye analazimisha niwe karibu na mtoto wakati kwangu naona ni hatar sana ananiforce nimuweke kwenye mtandao kumuwish birthday dah hapo panakuwa magumu
Ila hata hilo lina suluhisho jepesi, mwambie we umeshaoa hautaweza kumwacha mkeo, kwanza hilo then kuusu hayo ayatakayo kwa mwanae mwambie kwanza amjulishe mumewe kuwa mtoto si wake ili we uwe nae huru, najua atashindwa na hiyo kero itakutoka kihivyo.
 
ArD67

JF-Expert Member
Nov 14, 2016
2,821
2,000
Mara nyingi kwenye michezo ya hatari tuichezao na hao viumbe lazima tuwashikie akili zao vinginevyo watakupeleka shimoni.
Atakapoifikisha hiyo miaka 10 kipi utakachokifanya? Naona kama umelihairisha tu tatzo mkuu, embu shea nami utakachokifanya.
 
Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
20,899
2,000
shukran mkuu ila tatizo yeye analazimisha niwe karibu na mtoto wakati kwangu naona ni hatar sana ananiforce nimuweke kwenye mtandao kumuwish birthday dah hapo panakuwa magumu
Hapa bila kua mkali na kumwonyesha msimamo atakuyumbisha atakavyo
 
flulanga

JF-Expert Member
Jul 1, 2016
4,373
2,000
Nikwel mtoto angekuwa wakwako ila sasa sio wakwako so kaa nae mbali kuepusha shali naukizingatia wote wawili mpo kwenye ndoa
 
sisame

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
364
500
Hayo mbona hata Mimi yalinikuta ila nilimwambia kitu kimoja TU kwamba akifikisha miaka kumi anitafute nitajua nifanye nini na hata siwezi kusogelea huko kwake coz Mtoto ni copy yangu
Haaaaaah haaaaaah ....mkuu umenifanya nicheke kwa sauti...heeeeeh maisha yana mengi wajemeni!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom