Uchaguzi 2020 Ushauri: Ahadi za wanasiasa ziwe supported na 'Indemnity' ili wananchi wawe na uhakika wa utekelezaji wake

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Tumeshuhudia wanasiasa wakituahidi mambo mengi sana kipindi cha kampeni, laiti kama kwa miaka 15 iliyopita, ahadi za wanasiasa (Rais, Wabunge, na Madiwani) zingetekelezwa walau kwa asilimia 50 tu, hii Tanzania ingekuwa ni ya tofauti sana na hii tunayoiona hapa.

Mfano ahadi kama ya Milioni 50 kila kijiji ambayo ilitolewa mwaka 2015, kama ingetekelezwa, ingekuwa na matokeo chanya sana. Mbolea ya Di-Ammonium phosphate inaweza kugharimu wastani wa Tzs 52,000 kwa mfuko wa Kg 50, sasa hiyi Milioni 50 maana yake unapata mifuko ya mbolea kama 961 kwa kila kijiji. Kama uzalishaji unategemea sana mbolea, na watanzania wengi ni wakulima karibu 60%, maana yake ni kwamba, investment ya Tzs 50 Million kila kijiji ambayo ilikuwa ni ahadi ya wanasiasa, ingeweza kuongeza uzalishaji na utajiri wa wakulima waishio vijijini kwa kiasi kikubwa sana.

Vivo hivyo, kuna wabunge huko majimboni walishatuahidi, watauza zile VX V8 wanazogawiwa bungeni ili watengeneze dispensary majimboni, ila baada ya kupata ubunge, ahadi hazijawahi kutimizwa.

Kwa ufupi, watanzania tumekuwa ni wahanga wa kupewa ahadi fake na wanasiasa, na ni kama vile tumekuwa na akili fupi sana ya kusahau.

Kwa mtizamo huo, nimekaa chini nikafikiri, ni namna gani, tunaweza kuwa na namna ya kuhakikisha kwamba ahadi ambazo zinatolewa na wanasiasa zinatimizwa.

Kupitia INDEMNITY
Nadhani hii itakuwa njia ya kisheria nzuri sana ambayo itaweza kuwabana wanasiasa kutokutoa ahadi za uongo ama zisizotekelezeka, na pia itakuwa inawabana wanasiasa kutekeleza ahadi zao. Kwa sababu INDEMNITY, lazima itaainisha adhabu endapo kama itashindikana kutekeleza ahadi mtu aliyoitoa, na enforcement yake iwe kisheria kabisa.

Namna itavofanya kazi
Mfano, kama mgombea amekuja kumwaga ahadi zake endapo akichaguliwa, kinachofanyika ni kwamba, zile ahadi ambazo anazitoa, zinaorodheshwa zote na kutengenezewa INDEMNITY ambayo itakuwa ni legal document ambayo ipo binded kisheria.

Sasa endapo kama mgombea akishinda, anakuwa yupo legally binded kuhakikisha kwamba anatekeleza vyote alivyoviwekea INDEMNITY.

Ukweli wa mambo, hakuna namna yoyote ya kuweza, kuwabana hawa wanasiasa watekeleze ahadi zao.

Wataalamu ongezeeni nyama, kama vipi, tuanzishe petitition ya hichi kitu, na iwe ni mojawapo ya kanuni za uchaguzi, kuhusu kutoa sera.

Nawasilisha,
N.Mushi
 
Hii ni siasa tofauti na sheria. Tunacheza na utashi wa kisiasa na ushawishi zaidi kwa ahadi za ilani na si vinginevyo ambazo utekelezaji wake unategemea bajeti, hali ya uchumi wa nchi, vipaumbele vya kitaifa na upatikani wa fedha nje ya uwezo wa mtoa ahadi za chama chake. Hata hivyo kibanwe chama au mgombea?
 
Back
Top Bottom