Maadhimisho ya miaka miwili ya Hayati Magufuli na utekelezaji wa ahadi zake

Kwaasenga

Member
Jan 28, 2023
73
102
Kwanza naanza kwa kumshukuru Mungu kwa maisha ya aliyekuwa rais wa JMT hayati JPM.

Lakini pia nimpongeze rais wetu wa sasa mama yetu kipenzi SSH kwa kutimiza miaka miwili ya kuliongoza taifa letu. Mama anatuongoza vizuri sana.

Katika kutekeleza ahadi zote za mtangulizi wa rais wetu, mama ameendelea kutekeleza zile ahadi ambazo zilikuwa zimeshaanzishwa tayari.

Namuomba mama pia wakati anatekeleza zile ahadi zilizokuwa zimeanza basi na zile JPM (RIP) alizokuwa ameahidi tunaomba zitekelezwe ili kuweza kutimiza ndoto zake alizokuwa ameshaziainisha. Na hiyo itakuwa maana halisi ya kumuenzi. Wakati JPM anazindua kituo cha mabasi cha mbezi mwisho, alimuahidi mbunge wa akibamba juu ya ujenzi wa barabara za jimbo hilo ambalo kwa ujumla wake jimbo zima lia lami kwa asilimia 5 tu.

Kwa kuwa tayari hii ilikuwa ni ahadi, tunaomba utekelezaji wake ili tumuenzi rais wetu aliyetwaliwa. Angalau hili jimbo lipate barabara kwa asilimia 10.
 
Back
Top Bottom