Tatizo lako hujui na hutaki kujua na unakatisha tamaa wenzako wasijue ili wote msijue.
Kujua Display fake ama ya low quality si kazi ni kitu cha sekunde kadhaa tu ama dakika mfano.
1. Kioo kama ni ips ama low quality vya tft unaangalia tu viewing angle, nenda kulia, kushoto katikati ikiwa haioneshi kwa quality nzuri sio panel nzuri ya display, panel mbaya siku zote inakuwa na view angle mbovu.
2. Plasma siku zote ni kama Glass haina weusi wa LED inakuwa kama kijivu same kwa panel za zamani unazozikuta kwenye chogo.
3. Oled ukionesha Picha nyeusi ukiwa umezima taa inakuwa kama tv imezimwa, ama kwa mzoefu akiangalia tu kwa macho wakati inaonesha rangi nyeusi anajua hii oled, led/lcd haiwezi onesha nyeusi tii. Etc
Pia kila brand inakuja na Unique features
-Samsung smart zina Tizen
-LG smart zina Web os
-TCL smart zina Certified Google TV (Android TV) ama Roku ama opera TV
-Hisense zina Vidaa os etc.
Wachina wa kawaida ama TV fake zina android ambayo sio certified ni aosp ya kawaida kama kwenye simu ama tablet na wanaweka tu Launcher ku imitate, app zake ni za simu hazipo optimized kwa TV kwa macho tu unaona utofauti na Brand za juu.
Na Bei za TV ni within laki mpaka laki 2 Kibongo bongo, baina ya Wachina na brand kubwa
Mfano Tcl ni laki 4 mpaka 5, mchina choka mbaya ni ariund laki 2 na something mpaka 3, kama unaweza Afford toa laki 3 ukanunua TV isio na jina huwezi shindwa kuongeza kidogo ukanunua TCL ama Hisense.
Ukienda Inch 40, 43 ni hivyo hivyo unakuta LG na star x utofauti ni chini ya laki 2, unatoa laki 6 unanunua no name chinese unaacha laki 7 OG.