Ushamba wa wabongo, Viewers wa youtube si kigezo cha uzuri wa wimbo

Yani wabongo sijui tutaelimika lini, yani mtu kisa tu wimbo unatrend namba moja youtube basi anashikiwa akili na kuamini kuwa huo ndiyo wimbo bora.

Kuntrend kunaweza sababishwa na uzuri wa video mfano mzuri huu wimbo wa baba lao ni mbovu kuanzia vocal, lyrics mpaka melodies lakini video yake ni kali tena sana.

Wimbo ni audio, kuna nyimbo hazina hata video lakini zimehit dunia nzima.

Tatizo letu wabongo ni washamba sana tupo kwenye kushangaa video wakati mziki ni audio.

USHAMBA MBAYA SANA, AFADHALI UWE MASKINI KULIKO UWE MSHAMBA.
Hiki kiazi kimelitambua hili Leo au in wivu dhidi ya baba lao?
 
USHAMBA MBAYA SANA, AFADHALI UWE MASKINI KULIKO UWE MSHAMBA.
Kuna dalili zote kwamba wewe ndo mshamba manake hata maana ya ushamba yenyewe huijui... that's ushamba #1.

Ushamba #1 brings us to ushamba wako #2 pale unaposhindwa kufahamu kwamba music is all about personal taste... kile unachoona kwako kina ladha mzuri, kwa mwenzako can taste shit!

Na kwavile it's all about personal taste, hapo ndipo namba zinapo- matter... that brings us to ushamba wako #3 kwa kutofahamu umuhimu wa namba ingawaje unajiita Srinivan Ramanujan!!

Kwavile huwezi kupima taste, ndo maana hata YouTube huwa wanapima wimbo unaofikisha Views wengi zaidi ndani ya kipindi fulani na hawapimi "wimbo mzuri" zaidi kwa sababu suala la uzuri ni psersonal taste, haliwezi kuwa quantified!

Na ni kutokana na ushamba wako huo huo ndio maana hujui kwamba YouTube huwa wanatoa tuzo kwa accounts zinazofikisha idadi fulani ya subscribers na sio accounts zinazo-post nyimbo mzuri... again, it's all about number, and not taste!!

Lakini ushamba mkubwa zaidi, which's ushamba #4 ni pale unaposhindwa kutofautisha kati ya muziki na tasnia ya muziki... kwa kizungu, music and music industry!

Kwenye ulimwengu wa leo, it's all about kuijua tasnia ya muziki na sio kuujua muziki! Ukiujua muziki bila kuijua tasnia ya muziki lazima utafeli!!!

Ni kutokana na huo ushamba #4 wa kutojua tofauti kati ya muziki na tasnia ya muziki... that brings us to ushamba #5 wa kushindwa kuona maana ya wimbo wa Baba Lao katika kipindi kama hiki, nikimaanisha muda mfupi kabla ya fainali ya Wasafi Festival!

Kwenye Festival, Club, and the like, mashabiki hawajali unaimba nini (lyrics) but what matters is shangwe itakayotokana na kile kinachowasilishwa mbele yao! Ambience itakayoletwa na Baba Lao kwenye crowd ni kubwa maradufu ya ambience inayoweza kuletwa na ngoma kama Ukimuona!!

Kwa bahati mbaya sana, mshamba asiyejua tofauti kati ya muziki na tasnia ya muziki hawezi kulifahamu hilo!!!!

Video Mzuri?! OH LORD... again hilo nalo linakupa ngao ya ushamba #6 manake kwa mara nyingine unashindwa kufahamu kwamba muziki ni sanaa! No Drama, No Art!

Video ya Baba Lao sio kwamba mzuri sana bali it's too artistic... too dramatic!

Leo hii inapokuja ngoma kama This Is America ya Childish Bambino watu hawaongei sana kuhusu uzuri wa wimbo bali "uzuri" wa video! Lakini pale kinachoongelewa hasa sio uzuri wa video bali art iliyotumika kwenye video ya This Is America!!

Itoshe tu kusema kwamba, hakuna ubaya wowote hata mkiwa mnaleta mada kuhusu kilimo cha magimbi au tangawizi, na haya mengine mkaishia tu kuwa wasomaji!!

Usipolifahamu hilo hapo juu, utabakia kuwa mtu wa kudhihirisha ushamba wako siku hadi siku maisha yako yote!!
 
ubora wa wimbo hupimwa na platfom na si mawazo yako mkuu, hapa ni sawa nakusema unapima uzito kwa kukibeba kitu badala ya mzani hapo utakua unakadiria tu, nakukadiria huwez pata uhalisia
NB:ka hujaelewa endelea kuubeba mzigo wako wa ujnga maana ndo umechagua
 
Hakuna kitu kunachoitwa mziki wa sasa ... kama wao wanaimba mziki wa sasa mbona wanarudia nyimbo za zamani za kina saida kalori na ile siri ya nini... mziki ni mziki... na mziki siku zote utabaki kuwa audio ... nyie endeleeni kukata viuno kwenye video lakini kaeni mkijua hiyo ni hulka yenu tu na msisingizie muziki.
Ndo zinakuwa hit BABA LAO
 
Lkn ndio follwers hao wanao mpa ugali Youtube,Tidal,Itunes,sportfy nk na ndio wanamfanya apate shows nyingi kuliko yoyote Tanzania wewe piga kelele mwenzako yake yana mwendea.

Wewe endelea kuwasupport hao unao waona bora,kwani usichokipenda wewe wenzako walio wengi wanakipenda kwa hiyo hupunguzi kitu.
Fact
 
Back
Top Bottom