Humu katika JF kuna baadhi walikuwa mawakala wa vyama wakati wa mchakato wa kura.nimefanikiwa kuona nakala za matokeo walizopewa mawakala baada ya kuzisaini.Matokeo yalibandikwa pia kwenye vituo(kwa sehemu nyingi)Na wakati wa kujumlisha matokeo ya Rais,Wabunge kutoka kwenye vituo ulifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya chini ya WAWAKILISHI wa Vyama na wadau wengine na walipewa nakala za matokeo kwa nafasi ya Ubunge na Rais kisha nyingine kutumwa NEC makao makuu.Sasa kuna suala kuwa NEC taifa inabadilisha takwimu tofauti na halisi kutoka majimboni(Inawezekana)Hapa tuwekane sawa kuhusu suala hili la kubadilisha matokeo alyosema Dk Slaa.Kwa kuwa Vyama vina Nakala za matokeo kwa ngazi ya jimbo ,ebu watio mfano mmoja kwa kuskan zile nakala za matokeo ya jimbo fulani ambazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo ya NEC kisha waziweke hapa JF .Tusiongelee tu kwamba kule Moshi kituo kimoja kilibadilishwa takwimu bila udhibitisho wa kutoshaInawezekana kabisa Wizi wa kura ulikuwepo na Kipenzi chetu DK Slaa akawa ameibiwa kura LAKINI ushahidi unaotolewa na Dk Slaa,Marando na wana JF haina uzito wa kutosha kuudhibitsha.hapa Twende kwa ushahidi tu
Ushahidi huwezi kuupata hapa ndugu yangu. Mimi binafsi nilikuwa wakala hapa dsm, nilipewa kazi ya ku-compile matokeo toka vituoni.
Kuna mambo kadhaa niliyagundua ambayo yalikuwa ya kutilia mashaka na umakini wa tume ya uchaguzi pamoja na wasimamizi kuanzia vituoni kura zilikopigwa na kuhesabiwa hadi kwenye ofisi za watendaji wa kata matokeo yalipokuwa yanatolewa na kubandikwa.
1. Kwanza ni fomu za kujaza matokeo ya kura za uraisi na ubunge hazikuwepo katika vituo vingi, hii ilipelekea matokeo hayo kuandikwa kwenye karatasi za kawaida, kitu ambacho sio tu kiyume na utaratibu lakini pia inatoa mwanya wa uchakachuaji.
2. Nakala nyingi za matokeo kwa vile vituo ambavyo vilibahatika kupata fomu halisi za kujaza matoeo zilikuwa zinaonekana kurudiwa kuandikwa(kugandamizia ukipenda) na nyingine zilikuwa zinasomeka kwa mbali, kitu ambacho kinaweza kutiliwa shaka kuhusu usahihi wa idadi ya kura alizopata mgombea.
3. Wakati wa kufanya majumuisho kwenye ofisi za watendaji wa kata, niligundua baadhi ya fomu za matokeo kuonekana zimechezewa kwa kufutwa futwa na kuandikwa upya, na tulipojaribu kuwahoji wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wakali sana na kutaka asiyeridhika aende mahakamani na wanajeshi walikuwepo hapo ofisini wao wakawa wanatoa vitisho badala ya kutolea ufafanuzi wasiwasi na mashaka tuliyokuwa nayo. Maeneo niliyokuwa mimi masanduku ya kura yalikuwa yanakusanywa na magari ya jeshi na wanajeshi wenyewe hilo nalo lilikuwa jambo la kujiuliza kulikoni wanajeshi kusimamia uchaguzi? au walikuwa wametumwa na shimbo?
Kwahali niliyoishuhudia siku ile, mtu asiyetaka kuamini na kukubali kwamba matokeo ya uchaguzi huu yamechakachuliwa kwa kiwango kikubwa sana, aidha ana maslahi kutokana na uchakachuaji uliofanyika ama la hajui kinachoendelea.