Ushahidi wa Wizi wa kura uko wapi?

Rutunga M

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Messages
1,631
Likes
329
Points
180
Rutunga M

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2009
1,631 329 180
Humu katika JF kuna baadhi walikuwa mawakala wa vyama wakati wa mchakato wa kura.nimefanikiwa kuona nakala za matokeo walizopewa mawakala baada ya kuzisaini.Matokeo yalibandikwa pia kwenye vituo(kwa sehemu nyingi)Na wakati wa kujumlisha matokeo ya Rais,Wabunge kutoka kwenye vituo ulifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya chini ya WAWAKILISHI wa Vyama na wadau wengine na walipewa nakala za matokeo kwa nafasi ya Ubunge na Rais kisha nyingine kutumwa NEC makao makuu.Sasa kuna suala kuwa NEC taifa inabadilisha takwimu tofauti na halisi kutoka majimboni(Inawezekana)Hapa tuwekane sawa kuhusu suala hili la kubadilisha matokeo alyosema Dk Slaa.Kwa kuwa Vyama vina Nakala za matokeo kwa ngazi ya jimbo ,ebu watio mfano mmoja kwa kuskan zile nakala za matokeo ya jimbo fulani ambazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo ya NEC kisha waziweke hapa JF .Tusiongelee tu kwamba kule Moshi kituo kimoja kilibadilishwa takwimu bila udhibitisho wa kutoshaInawezekana kabisa Wizi wa kura ulikuwepo na Kipenzi chetu DK Slaa akawa ameibiwa kura LAKINI ushahidi unaotolewa na Dk Slaa,Marando na wana JF haina uzito wa kutosha kuudhibitsha.hapa Twende kwa ushahidi tu
 
marshal

marshal

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
354
Likes
33
Points
45
marshal

marshal

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
354 33 45
Brother na wan JF wote,Kwanza wazo la ushahidi ni bayana kwa kila kitu kinachohitaji uthibitisho.Lakini Sidhani kama ni wazo Muafaka kwa kila alie na matokeo kuyarusha kwenye mtandao maana itakuwa ngumu kwa wana JF kuyafanyia kazi ama kusimama nayo kama uthibitisho.Mimi naamini kama madai ya wengi kuwa CCM walichakachua kura yanathibitika,basi Chadema pamoja na Vyama vingine ambavyo nina imani vina watu makini (tukiwemo sisi ,The home of great thinkers) vitaweza kusimamia madai na kuyathibitisha.Kama Serikali ikiwemo NEC itatumia ushawishi wa Chama kinachodaiwa kuchakachua Kura,itakuwa ngumu sana kwa vyama pinzani kudai na kuapat haki.Mfumo wa mahakama ni sawa tu na NEC ambayo Majaji wote pamoja na jaji mkuu wana report kwa rais ambaye kawateua,na kama alishiriki kuchakachua kura itakuwa ngumu sana yeye kushindwa kuleta ushawishi katika mahakama na kubatilisha matokeo ya haki.Pamoja na yote ila bado tuan safari ndefu sana kuelekea katika amani ya kweli na utawala wa sheria.Serikali haitatimiza matakwa ya maisha bora kwa kila mtanzania kwa sababu wanatumia njaa za watanzania wenzetu ( Hasa majeshi na wafanya kazi wa serikali) kuweza kupata madaraka kupitia migongo yao.Tusidanganyane kila mtu ana ushahidi wa kile kilicho na kinachotea,isipokuwa hatuna tangible evidence ambayo ndio msingi wa kusimama nao.Nina uhakika Kikwete and the co. hawana mapenzi mema na nchi hii.Simaanishi kumwaga damu,ila makandamizo yakizidi na manyanyaso ya hadharani baadae nchi hii haitatawalika.Tamaa na undugunizeshenia na kufahamiana vinaiponza CCM.Sisemi CCM ina watu wote wabaya,la ila mfumo wa nchi na sera zinazokifanya kipate madaraka zitaipelekea nchi kutotawalika.Mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie,muongo mmoja ujao nchi itakuwa katika tense social relationships kama hali iliyopo sasa haitapatiwa majawabu.Asanteni kwa kutuongezea shule za kata maana hizo ndo zitakazowatoa madarakani walafi na mafisi msiokuwa na huruma ya nchi.
 
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
8,385
Likes
2,448
Points
280
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
8,385 2,448 280
Humu katika JF kuna baadhi walikuwa mawakala wa vyama wakati wa mchakato wa kura.nimefanikiwa kuona nakala za matokeo walizopewa mawakala baada ya kuzisaini.Matokeo yalibandikwa pia kwenye vituo(kwa sehemu nyingi)Na wakati wa kujumlisha matokeo ya Rais,Wabunge kutoka kwenye vituo ulifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya chini ya WAWAKILISHI wa Vyama na wadau wengine na walipewa nakala za matokeo kwa nafasi ya Ubunge na Rais kisha nyingine kutumwa NEC makao makuu.Sasa kuna suala kuwa NEC taifa inabadilisha takwimu tofauti na halisi kutoka majimboni(Inawezekana)Hapa tuwekane sawa kuhusu suala hili la kubadilisha matokeo alyosema Dk Slaa.Kwa kuwa Vyama vina Nakala za matokeo kwa ngazi ya jimbo ,ebu watio mfano mmoja kwa kuskan zile nakala za matokeo ya jimbo fulani ambazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo ya NEC kisha waziweke hapa JF .Tusiongelee tu kwamba kule Moshi kituo kimoja kilibadilishwa takwimu bila udhibitisho wa kutoshaInawezekana kabisa Wizi wa kura ulikuwepo na Kipenzi chetu DK Slaa akawa ameibiwa kura LAKINI ushahidi unaotolewa na Dk Slaa,Marando na wana JF haina uzito wa kutosha kuudhibitsha.hapa Twende kwa ushahidi tu
Soma magazeti ya leo hasa Mwananchi utaona ushahidi Dk Slaa: Tumeibiwa kura badala ya kutuandikia thesis ndefu ambayo ni weak!
 
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Messages
10,569
Likes
113
Points
160
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2008
10,569 113 160
Humu katika JF kuna baadhi walikuwa mawakala wa vyama wakati wa mchakato wa kura.nimefanikiwa kuona nakala za matokeo walizopewa mawakala baada ya kuzisaini.Matokeo yalibandikwa pia kwenye vituo(kwa sehemu nyingi)Na wakati wa kujumlisha matokeo ya Rais,Wabunge kutoka kwenye vituo ulifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya chini ya WAWAKILISHI wa Vyama na wadau wengine na walipewa nakala za matokeo kwa nafasi ya Ubunge na Rais kisha nyingine kutumwa NEC makao makuu.Sasa kuna suala kuwa NEC taifa inabadilisha takwimu tofauti na halisi kutoka majimboni(Inawezekana)Hapa tuwekane sawa kuhusu suala hili la kubadilisha matokeo alyosema Dk Slaa.Kwa kuwa Vyama vina Nakala za matokeo kwa ngazi ya jimbo ,ebu watio mfano mmoja kwa kuskan zile nakala za matokeo ya jimbo fulani ambazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo ya NEC kisha waziweke hapa JF .Tusiongelee tu kwamba kule Moshi kituo kimoja kilibadilishwa takwimu bila udhibitisho wa kutoshaInawezekana kabisa Wizi wa kura ulikuwepo na Kipenzi chetu DK Slaa akawa ameibiwa kura LAKINI ushahidi unaotolewa na Dk Slaa,Marando na wana JF haina uzito wa kutosha kuudhibitsha.hapa Twende kwa ushahidi tu
Ushahidi huwezi kuupata hapa ndugu yangu. Mimi binafsi nilikuwa wakala hapa dsm, nilipewa kazi ya ku-compile matokeo toka vituoni.
Kuna mambo kadhaa niliyagundua ambayo yalikuwa ya kutilia mashaka na umakini wa tume ya uchaguzi pamoja na wasimamizi kuanzia vituoni kura zilikopigwa na kuhesabiwa hadi kwenye ofisi za watendaji wa kata matokeo yalipokuwa yanatolewa na kubandikwa.
1. Kwanza ni fomu za kujaza matokeo ya kura za uraisi na ubunge hazikuwepo katika vituo vingi, hii ilipelekea matokeo hayo kuandikwa kwenye karatasi za kawaida, kitu ambacho sio tu kiyume na utaratibu lakini pia inatoa mwanya wa uchakachuaji.
2. Nakala nyingi za matokeo kwa vile vituo ambavyo vilibahatika kupata fomu halisi za kujaza matoeo zilikuwa zinaonekana kurudiwa kuandikwa(kugandamizia ukipenda) na nyingine zilikuwa zinasomeka kwa mbali, kitu ambacho kinaweza kutiliwa shaka kuhusu usahihi wa idadi ya kura alizopata mgombea.
3. Wakati wa kufanya majumuisho kwenye ofisi za watendaji wa kata, niligundua baadhi ya fomu za matokeo kuonekana zimechezewa kwa kufutwa futwa na kuandikwa upya, na tulipojaribu kuwahoji wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wakali sana na kutaka asiyeridhika aende mahakamani na wanajeshi walikuwepo hapo ofisini wao wakawa wanatoa vitisho badala ya kutolea ufafanuzi wasiwasi na mashaka tuliyokuwa nayo. Maeneo niliyokuwa mimi masanduku ya kura yalikuwa yanakusanywa na magari ya jeshi na wanajeshi wenyewe hilo nalo lilikuwa jambo la kujiuliza kulikoni wanajeshi kusimamia uchaguzi? au walikuwa wametumwa na shimbo?

Kwahali niliyoishuhudia siku ile, mtu asiyetaka kuamini na kukubali kwamba matokeo ya uchaguzi huu yamechakachuliwa kwa kiwango kikubwa sana, aidha ana maslahi kutokana na uchakachuaji uliofanyika ama la hajui kinachoendelea.
 
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
7,698
Likes
187
Points
160
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
7,698 187 160
Humu katika JF kuna baadhi walikuwa mawakala wa vyama wakati wa mchakato wa kura.nimefanikiwa kuona nakala za matokeo walizopewa mawakala baada ya kuzisaini.Matokeo yalibandikwa pia kwenye vituo(kwa sehemu nyingi)Na wakati wa kujumlisha matokeo ya Rais,Wabunge kutoka kwenye vituo ulifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya chini ya WAWAKILISHI wa Vyama na wadau wengine na walipewa nakala za matokeo kwa nafasi ya Ubunge na Rais kisha nyingine kutumwa NEC makao makuu.Sasa kuna suala kuwa NEC taifa inabadilisha takwimu tofauti na halisi kutoka majimboni(Inawezekana)Hapa tuwekane sawa kuhusu suala hili la kubadilisha matokeo alyosema Dk Slaa.Kwa kuwa Vyama vina Nakala za matokeo kwa ngazi ya jimbo ,ebu watio mfano mmoja kwa kuskan zile nakala za matokeo ya jimbo fulani ambazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo ya NEC kisha waziweke hapa JF .Tusiongelee tu kwamba kule Moshi kituo kimoja kilibadilishwa takwimu bila udhibitisho wa kutoshaInawezekana kabisa Wizi wa kura ulikuwepo na Kipenzi chetu DK Slaa akawa ameibiwa kura LAKINI ushahidi unaotolewa na Dk Slaa,Marando na wana JF haina uzito wa kutosha kuudhibitsha.hapa Twende kwa ushahidi tu
Rutunga,
Najua argument yako inako base, kwa kufikiria jinsi taratibu zilivyo unadhani kuchakachuliwa kwa kura ni vigumu.
Nimekuwa nikifuatilia mchakato mzima wa kura mwaka huu 2010. Baada ya zoezi la kupiga kura. Kura zinahesabiwa mbele ya mawakala. Kwa kuanzia zilikuwa zinahesabiwa kura za rais kisha mbunge kisha Diwani. Baada ya kupata matokeo na mawakala wote kuridhika, msimamizi wa kituo utoa form namba 20,21,22 (kama sijasahau) ambazo ni za matokeo na ujaza matokeo. Moja ikiwa ya rais nyingine ya mbunge nyingine ya udiwani. mawakala wote husaini fomu hizi kukubali matokeo kama wamelidhika na mwenendo wa uchaguzi kuwa kila kitu ni sawa. Kisha kila wakala upewa nakala moja kutoka katika kila form hizo. Orginal copy ubaki ndani ya kitabu kwa ajili ya kupelekwa kwa mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo. Nakala moja ya matokeo ya Ubunge na nyingine ya udiwani ubandikwa nje ya kituo kwa ajili ya watu kujua matokeo lakini ya urais haibandikwi.
Mawakala huwa ni mbadala wa wagombea kwa hiyo uwapelekea wagombea nakala ya matokeo yote ya urais, ubunge na udiwani kwenye ofisi za vyama ili wajue matokeo hatakama hayajatangazwa. Hivyo wagombea huwa wameshafahamu nini wamepata hata kabla msimamizi hajatangaza.
Lakini pia mkurugenzi huwa anatumia form hizo hizo akishirikiana na mawakala wa vyama au wagombea ku sum up hesabu ya vituo vyote na kuja na jibu la nani atangazwe kama mshindi.
Dr Slaa kama mgombea anajua wazi ni kwa nini analalamikia uchakachuaji kama fomu alizo nazo zinaonyesha kitu tofauti na tume! Nina amini kwa sasa hata yeye anajumlisha kivyake na anaona upungufu na tofauti iliyopo na tume.
Jambo lingine ni kwamba nilimsikia Rajab Kiravu siku moja kabla ya 31.10 akiojiwa na TBC na akijibu tuhuma hizi hizi za sasa alisema tume itakaa na vyama kuona kama wanakubaliana kuhusu hesabu hizi kabla ya kutangaza, sasa nisichojua ni kama matangazo haya wamekubaliana na vyama kuwa yako sahihi? au wameamua watangaze wapendavyo? Ninaamini there is something wrong here na tume inatakiwa ijiweke sawa kujibu hoja badala ya kudhani sauti yao ndio itakuwa ya mwisho. Wanaturudisha kwenye enzi za Zanzibar na wanaweka maisha yetu hatarini. Wanatangaza mambo yasiyo sawa wakitegemea nini? kwa nini wanalazimisha tukubali matokeo yasiyo sahihi? kwa nini wao wasiwe tayari kutangaza matokeo yaliyo sahihi kama wana hakika wanataka tukubali kushindwa?
Hakuna ambaye anakataa kukubali kushindwa hapa. Issue ni kwamba je wako tayari tukae tuwaonyeshe ukweli?
Dr Slaa atakuja na ushahidi mzuri baadaye kwa sasa ushahidi mdogo tu alioutoa unaonyesha kuna udanganyifu na amefanya hivyo ku intervene ili tume isiendelee kutangaza longo longo lakini kuna mengi zaidi.

Hii hapa ni habari iliyo hapa hapa JF

1. Dk Slaa aelezea jinsi CCM ilivyochakachua Uchaguzi Mkuu

Slaa aitaka NEC isitishe matokeo.*Adai yanayotangazwa ni tofauti na kura za vituoni.
*Asema yameandaliwa makusudi kumbeba mgombea wa CCM.
*NEC yasema kama ana ushahidi awasilishe vielelezo.

Na Tumaini Makene
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa amesema zimefanyika njama kuhujumu matokeo ya uchaguzi mkuu
hasa katika nafasi ya urais ili kumbeba mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na chama chake, Rais Jakaya Kikwete.

Kutokana na hali hiyo ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo unaoendelea kwa kuwa yanatofautiana na idadi halisi ya kura zilizohesabiwa vituoni, kisha irudie uchaguzi wote katika nafasi ya urais.

Dkt. Slaa aliongeza kuwa chama chake kina ushahidi, na mwingine kinaendeleea kuufanyia kazi, unaoonesha namna ambavyo matokeo yanayotangazwa na NEC ni tofauti na yale yaliyopatikana vituoni baada ya upigaji kura.

Mbali ya nafasi ya urais, mgombea urais huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, alisema kuwa uchaguzi unapaswa kurudiwa katika nafasi ya ubunge katika majimbo ambako matokeo yake yameonekana kuwa na utata mkubwa, akitolea mfano wa Jimbo la Segerea na maeneo mengine nchini.

Dkt. Slaa aliyasema hayo jana Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisisitiza kauli yake ya mara kwa mara kuwa hawezi kuzungumza bila kuwa na ushahidi au kufanya utafiti, akionesha namna ambavyo chama chake kimefanyiwa kile alichodai kuwa ni hujuma, kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi.

"Tumeamua kuzungumzia mwenendo wa mambo haya sasa kwa sababu tunajua tofauti na udiwani au ubunge ambapo unaweza ku-challenge (kupinga) ushindi mahakamani, urais huwezi, hata kama matokeo yatakuwa na dosari, huwezi kwenda mahakamani wala kuhoji popote, hivyo lazima tuseme sasa...tunapenda kutoa tahadhari kwa vyombo vya ulinzi na usalama na NEC yenyewe kuna mambo yametushtua sana, taratibu zimekiukwa sana.

"Kwanza walianza kisaikolojia, mnakumbuka gazeti la serikali lilisema Slaa hawezi kuwa rais, akaja mnadhimu mkuu wa jeshi naye akasema yake, mkuu wa polisi naye hivyo hivyo, wakisisitiza tukubali matokeo, wanasaikolojia tukawa tunajiuliza ni kitu gani kinaandaliwa, sisi tulisema mapema matokeo tutayakubali iwapo mchezo ukifuata taratibu," alisema Dkt. Slaa na kuongeza.

"Nitazungumzia zaidi upande wa urais, tangu matokeo yaanze kutolewa kulikuwa na mkakati maalumu, NEC ikawa haitangazi matokeo ya maeneo yale ambayo tuna nguvu, si kitu kidogo hicho, walianza Zanzibar yakamalizika majimbo yote, wakaja maeneo mengine ya bara...ilikuwa inajengwa dhana kisaikolojia kuwa CHADEMA iko huko mwishoni na ni ya kushindwa tu, sisi tukaanza kukusanya data huko chini kukoje."

Huku akitoa mifano ya baadhi ya vituo katika majimbo kama vile Same Mashariki, Mheza, Segerea, Hai, Kiteto, Kibakwe, Kyela, Morogoro Mjini na mahali pengine, Dkt. Slaa alisema kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi, ili kutimiza kile alichodai ni 'kucheza na namba za matokeo na saikolojia za watu', kazi ambayo, inaonekana imefanywa kitaalamu na watu makini.

Akitumia maeneo hayo kama sampuli ya nchi nzima, Dkt. Slaa alidai kuna mahali kura zimepinduliwa kwa ama kuongezwa au kupunguzwa kwa pande zote mbili za CCM na CHADEMA, kukosekana kwa fomu za matokeo, kuwepo kwa vituo bandia vya kupigia kura, kutangazwa kwa matokeo ya urais na ubunge bila kuwa yamejumlishwa, wala masanduku ya kura kuwepo eneo la kujumlishia.

Alitaja baadhi ya mambo aliyoita hujuma, kuwa ni kutokuonekana kwa matokeo ya baadhi ya vituo mpaka wakati wa hesabu za mwisho na matokeo kutangazwa, (mathalani Kata ya Kiwalani, Tabata na Vingunguti huko Segerea). Pia wasimamizi wa vituo kuondoka na fomu za matokeo badala ya kukusanywa mbele ya mawakala, kutoshirikisha mawakala wakati wa kujumlisha.

"Sasa tunataka kuwauliza NEC kama maeneo mengine fomu hazikuwepo, au masanduku yalikuwa hayajafika eneo la kujumlishia wilayani, wamepata wapi hesabu za kutangaza matokeo ya kitaifa? Wanacheza na matokeo na saikolojia za watu...kwa mfano huko Same katika moja ya vituo, Kikwete alipata kura 92, Slaa alipata kura 69, lakini wao wakatangaza Kikwete 123 na Slaa 33.

"Wakaweka kituo hewa, wakacheza na namba, katika kituo halali, Kikwete akapata kura 190, Slaa kura 26, lakini zikazidishwa mara mbili zionekane ni za kituo kimoja, huko Mheza CCM walipata 92, CHADEMA 57 na CUF 71, lakini walipotangaza wakasema CCM 359, CHADEMA, 15 na CUF 23.

"Huko Geita matokeo halisi katika kata 20 yanaonesha kuwa CCM walipata 30,960, CHADEMA kura 15,736 lakini ilivyotangazwa na NEC taarifa zikakinzana, wakazipunguza na kuweka CCM 17,792, CHADEMA 3,789...hii maana yake nini, unacheza na namba kwa sababu zile za mwanzo ukisema Dkt. Slaa ana kura elfu kumi na tano ataonekana ni tishio lakini ukisema anazo elfu tatu, unamwonesha kuwa ni mtu wa kushindwa.

"Sina neno jingine la kuita kitendo hiki, bali huu ni wizi mkubwa. Matokeo yanayotangazwa na NEC si yale yaliyopatikana vituoni, tunapigiwa simu na watu wetu wakishangaa hiki ni kitu gani, mahali pengine matokeo yametangazwa bila kuwepo kwa fomu za uchaguzi au za matokeo, mahali pengine watu wetu hawajashirikishwa katika zoezi la kuhesabu au kujumlisha kura, kisha wanaambiwa kuwa mambo yamekamilika.

"Hatujalala tunafanyia kazi mambo haya ili hasa tujue maana yake, ninao uzoefu wa wizi wa kura unaofanywa na CCM huko Karatu...tumeagiza ushahidi zaidi uletwe kutoka huko vituoni, mwingine bado tunaofanyia kazi...tunashangazwa hata na asilimia za waliopiga kura, zingine zinafika hata asilimia elfu mbili au zaidi.

"Baada ya kuona mwelekeo huo, ninaomba NEC, tena natumia polite language (lugha ya upole), naiomba NEC...kama kweli tunaitakia mema nchi hii, kama kweli tuna utashi mwema na nchi hii, NEC ifute matokeo yote ya urais na kura zirudiwe upya...hatuwezi kukubali matokeo yaliyopikwa na usalama wa taifa, matokeo haya si ya kura za wananchi," alisema Dkt. Slaa na kuongeza;

"Tunataka mkuu wa usalama wa taifa ajiuzulu, hatukumuajiri awe usalama wa chama kimoja, jumuiya ya kimataifa waweke taarifa zao hadharani kama walivyoanza leo katika vyombo vya habari, taasisi za serikali kama TEMCO, nasikia hawa wamezuiwa kutoa matokeo yao ya uangalizi, tunataka zitoe taarifa zao, wasaidie nchi, si Kikwete wala CCM."

Dkt. Slaa alisema kuwa dosari nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu wa Jumapili iliyopita, kwa kiasi kikubwa zimetokana na maelekezo, akitolea mfano wa barua mbili zilizokamatwa hivi karibuni huko Mwanza, zikielekeza kuondolewa kwa majina ya vijana ili wasipigie upinzani, kuchelewesha utoaji matokeo, kutumia vijana wa green guards, matumizi ya nguvu ya polisi kutisha watu.

"Watanzania wakiishiwa uzalendo na uvumilivu kisha kuamua kuingia mitaani kama tulivyoona huko Geita, Shinyanga, Mwanza na kwingineko nani atakayebaki au kulaumiwa? Kikwete alisema vurugu zikianza wapinzani watapanda ndege kuondoka nchini, kumbe alijua anataka kufanya uchakachuaji huu waliofanya," alisema Dkt. Slaa." Mwanasheria wa CHADEMA, Mabere Marando amewasilisha rasmi NEC barua ya kupinga matokeo.

Hatua zilizochukuliwa/tutakazochukua ni:

1. Kwenda NEC - (barua imewasilishwa jana)
2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi
3. Tunakwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea kwa kuwaonyesha ushahidi kamili.
4. Dk. Slaa amepanga kuwakilisha ushahidi MZITO unaoonyesha uchakachuaji mkubwa wa kura za Urais ulivyofanyika. Ushahidi huo ni pamoja na matokeo halisi ya vituoni yenye saini za mawakala ambayo yanapishana na yale ya NEC.

Marando alisema hadi juzi Jumatatu matokeo ambayo tayari walikuwa wamekusanya kutoka katika maeneo mbalimbali ya Nchi, yanaonyesha Mgombea Urais wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa anaongoza kwa wastani wa asilimia 61.6%."
"
 
Mzee wa Rula

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
8,181
Likes
113
Points
160
Mzee wa Rula

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
8,181 113 160
Hivi ni kwa nini hawabandiki fomu ya matokeo ya urais kama wafanyavyo kwenye ubunge na udiwani????
 
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
7,698
Likes
187
Points
160
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
7,698 187 160
Hivi ni kwa nini hawabandiki fomu ya matokeo ya urais kama wafanyavyo kwenye ubunge na udiwani????
Ili wachakachue na hakuna wa kuwa fanya lolote hata mahakama!
 
Forum statistics

Threads 1,235,082
Members 474,351
Posts 29,211,571