Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

yani kama mama anayetarajia kuingia labour vile wanavyohangaika
 
Tatizo la Watanzania mnapenda sana kushambulia kitu kabla haya ya kujua cotent zilizo kwenye habari husika. Hebu msome hii habari ya Jamhuri kisha muone kama hakuna matatizo ndani ya Chadema. Walichofanya Jamhuri ni kuwasaidia wanachama na wapenda Chadema kwamba kuna matatizo ndani ya chama hiki kinachopendwa. Sasa mnapoambiwa ukweli mnarukia kulaani gazeti.

Someni hapa JAMHURI:




Chadema inakufa
*Mbowe, Dk. Slaa, Zitto, Shibuda hawapikiki
*Marando awatuhumu CCM, Usalama wa Taifa
*Heche, Waitara, Shonza hawazungumzi pamoja
*Kinana atema cheche aeleza anachokifanya sasa

Na Christopher Gamaina na Edmund Mihale, Dar es Salaam

Hali ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni mbaya na tayari kumeanza kuwapo hofu ya chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini, kufa.

Hofu hiyo inayokana, pamoja na mambo mengine, kuibuka kwa makundi yanayohasimiana, yanayoundwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho.

Katika fukuto hilo, JAMHURI imefanikiwa kupata habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi, zinazohusu kuwapo mkakati madhubuti wa kuwafukuza baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Duru za uchunguzi zinaonesha kuwa walengwa wakuu kwenye mpango huo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda. Pamoja nao, walengwa wengine ni wafuasi wa wanasiasa hao.

Moja ya sababu zinazotajwa kuchochea au kuibua makundi makuu matatu ndani ya Chadema, ni mbio za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015. Makundi yanayotajwa, na ambayo yameanza kujitokeza hadharani yamejiegemeza kwa viongozi watatu maarufu - Zitto, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa.

Zitto anatajwa kama mmoja wa vinara wa migogoro ndani ya Chadema, akidaiwa kutumia umaarufu wake kama kinga ya kufanya lolote analotaka akiamini kuwa “Chadema bila Zitto, haipo”.

Pia urafiki wake wa karibu na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, na viongozi wengine waandamizi wa CCM umekuwa ukiwatia shaka baadhi ya wanachama, wafuasi na viongozi wa Chadema.

Tayari Zitto ameshatangaza hadharani nia yake ya kuiwakilisha Chadema kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015, na kwa sasa anaendesha kampeni ya umri wa wagombea urais kupunguzwa na ikiwezekana iwe miaka 35. Mwaka 2015, Zitto atakuwa anatimiza umri wa miaka 39.

Hii si mara ya kwanza kuibuka kwa makundi ndani ya Chadema, kwani miaka kadhaa iliyopita Zitto na Mbowe walisuguana kutokana na uamuzi wa Zitto wa kutangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa. Mzozo huo ulimalizwa kwa busara ya wazee na wanachama waandamizi ndani ya chama hicho, kwa Zitto kukubali kuondoa jina lake mbele ya waandishi wa habari.

Hata kurudi kwake kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Chadema kulitokana na busara za wazee, kwani Mbowe hakumtaka kabisa Zitto aendelee kuwa na madaraka ya juu katika chama.

Katika hotuba yake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema, Mbowe hakuficha kutamka wazi kuwa alinyanyaswa vya kutosha, na kwamba baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti, alikuwa na uamuzi wa kuamua nani awe nani ndani ya chama hicho.

Aidha, aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ambaye alionekana kutofautiana na Mbowe, alikufa katika ajali ya gari ambayo mazingira yake bado yanahojiwa na wafuasi wake. Wangwe anakumbukwa kwa kuwa mstari wa mbele kudai wigo mpana wa demokrasia ndani ya chama hicho.

Mtafaruku ndani ya Chadema umeenea hadi kwa Mratibu wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwita Waitara, ambaye kwa sasa haelewani kabisa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVITA), John Heche.

Ugomvi wa wanasiasa hao vijana, ulianza wakati wa kura za maoni za kumpata mwanachama wa Chadema kwa ajili ya kuiwakilisha katika uchaguzi wa ubunge Jimbo la Tarime mkoani Mara. Waitara alimshinda Heche, ingawa naye baadaye aliangushwa na mgombea wa CCM, Nyambari Nyangwine.

Tangu wakati huo, Waitara na Hache hawapikiki chungu kimoja. Uhasama huo umeshika kasi baada ya Heche kwenda Tarime hivi karibuni na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo.

Ugomvi ndani ya Bavicha umezidi kuwa mkali, kwani Heche pia haelewani kabisa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Julian Shonza. Ugomvi wao ulipamba moto baada ya Shibuda kutangaza kuwania urais kupitia Chadema akiwa katika mkutano wa CCM.

Baada Shibuda kutangaza nia hiyo, Heche alimkosoa kwa kusema alifanya makosa kutangaza nia akiwa katika jukwaa lisilostahili. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Shonza alijitokeza hadharani na kumpinga Heche, akisema Shibuda alikuwa na haki ya kufanya hivyo. Hadi sasa wanasiasa hao vijana hawaelewani.

Wakati hali ya mambo ikizidi kuwa mbaya ndani ya Chadema, viongozi wake waandamizi wanajitahidi kuficha ukweli wa mambo.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando, katika mahojiano yake na JAMHURI, amejitahidi kuwa na kauli kali za kushutumu waandishi wa habari na kusema kwamba chama hicho hakina mgogoro wowote wa kiuongozi.

Amekwenda mbali zaidi kwa kusema baadhi ya magazeti na vyombo vya habari vinatumiwa na CCM kwa ajili ya kuivuruga Chadema.
“Kama unapenda kuandika, andika, lakini mimi najua hakuna migogoro wala makundi matatu wala matano ndani ya Chadema, kama unataka kuandika andika hayo uliyoambiwa. Unapoendelea kuhoji hayo unafanya kazi ya CCM na Usalama wa Taifa,” amesema ambaye amewahi kufanya kazi ya ushushushu katika Usalama wa Taifa.

Pia Marando ana historia ya kuwa kwenye migogoro, kwani akiwa NCCR-Mageuzi (chama alichokiasisi) aligombana na hatimaye kushindwa na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Augustine Mrema. Alikihama chama hicho na kujiunga Chadema.

Wakati Marando akisema hivyo, uhasama miongoni mwa viongozi wa chama hicho unaonekana wazi hata kwenye Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ambako baadhi ya viongozi, akiwamo Zitto, wamejitenga kabisa. Mwanasiasa huyo hahudhurii mikutano wala hafla za uchangishaji fedha zenye lengo la kufanikisha mpango huo. Wakati wa Operesheni Sangara, wakati ambao Chadema haikuwa na mpasuko mkubwa, Zitto alishiriki mikutano mingi na sehemu mbalimbali nchini.

Pia kuna habari za uhakika kwamba Zitto amekuwa akisafiri nje ya nchi bila ruhusa au kutoa taarifa kwa uongozi wa juu wa chama chake. Si hivyo tu, bali kuna baadhi ya vikao vya chama vinavyohitaji msimamo wa pamoja ambavyo amekuwa hahudhurii.

Waitara, Heche wazungumza

Kwa upande wake, Heche anajitahidi kumung’unya maneno kwa kusema hakuna makundi yanayohasimiana ndani ya Chadema, na kwamba chama hicho hakiamini katika kufukuzana, bali katika kujenga chama kwa kufuata misingi ya Katiba, miongozo na kanuni.
“Chadema ina kanuni, misingi na miongozo, iwapo mtu atakosea basi anatakiwa kufukuzwa kwa kufuata kanuni hizo na si vinginevyo,” amesema Heche.

Kwa upande wake, Waitara anasema hajisikii vizuri kuona Heche amekwenda Tarime kutangaza nia ya kuwania ubunge, ilhali akitambua yeye (Waitara) bado ana mtaji wa wapigakura waliomuunga mkono katika kinyang’anyiro cha ubunge jimboni humo mwaka 2010.

“Katika hali ya kisiasa, kibinadamu, lazima ujisikie vibaya, tena ni mtu (Heche) ambaye nilipogombea hakuniunga mkono, mimi ninaona ni kama inatangazwa vita ambayo inabidi itumike busara kuimaliza, lakini mtu huwezi kuwa mnafiki lazima ujisikie vibaya.

“Katika hali ya kawaida kitendo cha kwenda kutangaza kwamba anagombea na mimi nilikuwa mgombea pale… Mwaka 2010 baada ya Heche kushindwa kwenye kura aliondoka kuja Dar es Salaam kujiunga kwenye timu ya Dk. Slaa akamsaidia kufanya kampeni, lakini hata ndugu yake kama Mwenyekiti wa Bavicha Tarime aliondoka kabisa Tarime.

“Kwa ujumla watu wa Heche waliokuwa wanamuunga mkono hawakunisaidia kampeni, kwa hivyo kilichofanyika watu waliingia kwa maana ya kusema Chadema, siyo mtu… tukapambana mpaka tukafikia tulipofikia, matokeo yake hilo lilileta mgawanyiko yakatokea matokeo ambayo yalitokea, tukapoteza jimbo.

“Kwa hiyo, huo ndiyo ukweli, kwamba wao tulipokwenda kwenye mchakato wa kura za maoni baada ya kushindwa, hawakuniunga mkono… hata familia ya akina Heche haikuniunga mkono kabisa na sina hakika kama walinipigia kura.

“Ukweli ni kwamba watu wangu wametangaza kwamba lazima watanisapoti kwa nguvu zote…lakini nilishasema mimi sina tatizo tukienda kwenye mchakato wa chama, kama kitamteua mtu ambaye wataona kwamba anafaa mimi nitafanya kazi ya chama.
“Lakini ninachokifahamu ni kwamba kwa sababu niligombea 2010 tukapambana na watu wa Tarime bado wananiunga mkono, nina mtaji pale, mimi nadhani bado nitapambana,” anasema.

Waitara ameomba mara kadhaa kukutana na Heche kujadili kuhusu kugombea ubunge wa Tarime, lakini bado juhudi hizo hazijazaa matunda na kwamba hata uongozi wa juu Chadema haujaonyesha nia ya kuingilia kati suala hilo.

“Mimi na yeye (Heche) tunazungumza mambo ya kawaida sana, hatujawahi kukaa tuzungumzie mustakabali wa Tarime, na hilo jambo amejaribu kulikwepa muda mrefu sana, na mimi nimeomba mara nyingi kwamba hata chama kiingilie kati tujadiliane, nimeomba viongozi wengi, nimemuomba Dk. Slaa.

“Lakini kama waliniteua kugombea, lakini kuna mtu anatangaza katika utaratibu usio wa kawaida, ametangaza mapema. Kwa hiyo, binafsi nisingetaka hayo mapambano yaendelee kuwapo,” amesema Waitara.

Kwa upande wake, Heche amesema hana ugomvi na Waitara kwa kuwa kila wakati wamekuwa wakikutana na kusalimiana vizuri.
Kuhusu kutomsaidia katika kampeni za mwaka 2010, Heche anasema hakufanya hivyo kwa vile alichaguliwa na uongozi wa Taifa wa Chadema kuwa kiongozi wa msafara wa kampeni za kitaifa za chama hicho.

“Kwa sasa Chadema hatuzungumzi mambo ya mwaka 2010, kwa sasa tunazungumzia kuchukua dola mwaka 2015, wakati Waitara anagombea mimi nilichaguliwa na uongozi wa juu kuwa kiongozi wa msafara wa mgombea urais wa Chadema.

“Hata hivyo, Chadema inao wanachama wengi na si mimi tu ambaye wanatakiwa kufanya kazi ya chama, si mimi tu niliyetakiwa kubaki mkoani Mara na kumpigia kampeni mgombea huyo. Hata hivyo, nilimtambulisha Nyamongo na Sirari (miji iliyopo Tarime).
“Hata mwaka 2015 uongozi wa juu wa chama ukinichagua kuongoza msafara wa kampeni, na kama sigombei ngazi yoyote ya uongozi wa chama nitafanya hivyo,” amesema.

Kinana azungumza
Uongozi mpya wa CCM umetajwa kama moja ya sababu zinazoifanya Chadema ianze kuyumba. Chini ya Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, CCM imeanza kujijenga upya kwa wanachama wake na wananchi kwa lengo la kurejesha imani iliyokuwa imeporomoka mno.
Kinana, ameiambia JAMHURI kwamba ugomvi ndani ya Chadema ni wao wenyewe, na kwamba CCM haihusiki kwa namna yoyote kuibua au kukuza mgogoro.

Amesema tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, amefanya mikutano sehemu mbalimbali nchini, na kwamba hajawahi hata siku moja kuzungumza masuala ya Chadema na vyama vingine kwenye mikutano wanayofanya.

“Sina muda wala nafasi ya kuzungumza mambo ya wapinzani, tangu niteuliwe kuwa Katibu Mkuu nimefanya mikutano 23, hakuna mahali nilipotaja chama cha siasa. Kazi yangu ni kunadi Ilani ya CCM, kukabiliana na matatizo ya wananchi. Matatizo tunayoyakabili kupitia Ilani yetu yanatosha kabisa, sina wala hatuna sababu ya kujadili wapinzani. Kama wao wana matatizo yao, hayo ni yao. Wasituhusishe.

“Narudia tena, sisi kazi yetu ni utekelezaji Ilani yetu, kupambana na matatizo ya wananchi na kuimarisha chama chetu, basi. Wasitafute mchawi, hatuna muda wa kujadili mambo yao,” amesema Kinana.

Wimbi la viongozi kuihama Chadema
Chadema inakabiliwa na changamoto nyingine ya kuwatimua baadhi ya viongozi na wanachama. Madiwani kadhaa wa Arusha na Mwanza wamefukuzwa kwa tuhuma mbalimbali zikiwamo za usaliti. Hatua hiyo imekuwa ikungwa mkono na wafuasi wengi wa Chadema, lakini imekuwa kete kwa CCM kuwapata wanachama hao.

Wiki iliyopita, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mbeya ambaye amesimamishwa, Edo Mwamalala, alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusema kwamba Dk. Slaa ni mamluki namba moja wa CCM, kutokana na kumiliki kadi ya chama hicho.

Viongiozi wengine wa Chadema wakiwamo Mbowe, Dk. Slaa, Zitto na John Mnyika (Mkurugenzi wa Habari na Uenezi) hawakupatikana kuzungumzia sakata la mgogoro ndani ya chama hicho.
 
watanzania wameelimika sasa hivi hizo propaganda ni kazi bure.
 
watanzania wameelimika sasa hivi hizo propaganda ni kazi bure.

Walioelimika ni wachache sana. Kweli, ukitaka kumficha Mwafrika kitu, kiweke kwenye maandishi. Unapinga kuwa Chadema hakuna mgpgoro? Mbona hapa hapa JF kuna uzi unaohusu migogoro ndani ya BAVICHA? Mbona kila leo kunaelezwa vurugu za Shibunda ndani ya CDM? Je, Mbowe na Slaa wanapikika chungu kimoja? Yote haya yapo, lakini kwa ujinga wa kutotaka kuyasoma, mnakimbilia kulishutumu Gazeti. Kukiri tatizo ni moja ya njia za kuelekea kulitatua! Tukubali kwamba tuna matatizo ndani ya chama, then kuanzia hapo tuone namna ya kusonga mbele. Kujitawaza kwa majani ya mgomba hakusaidii kuijenga Chadema.
 
ni vigumu sana kwa sasa ccm kukubalika na kinazidi kupoteza mwelekeo kadri wanavyopigana na slaa. watz hawataki kusikia malumbano ila wanataka kujua maisha yao ya sasa na baadae yanarekebika vipi
 
Maana nzuri ya neno PROPOGANDA ni uongo ..na uongo siku zote adui yake ni ukweli acha waendeleze uongo wao na CHADEMA waendeleze ukweli mwisho wa siku .. ukweli utakuweka huru bwana.
 
Huo ni muendelezo wa ccm kuelekea kaburini! Tatizo magamba wanaona adui wao ni chadema! Wamemuacha adui yao mkuu ambaye ni ufisadi wanapigana na anae ona kuwa ufisadi ndio adui wa taifa hili. Wangejitahidi kumuuwa adui fisadi ndio waje waseme chadema inakufa! Pesa ziko uswis hawafanyi jitihada za kuzirejesha wao wana pambana na chadema wanaopiga kelele fedha hizo zirejeshwe. Ujinga mtupu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
mkuu hapo kwenye bolded red;adui wa ccm sio ufisadi!ufisadi na ccm are inseparable,yani ukitaja ufisadi umetaja ccm wote,.kwa hiyo adui wao ni yule anayepambana na ufisadi sababu ukipambana na ufisadi umepambana na ccm yote kuanzia mwenyekiti hadi vuvzela nepi
 
Wanataka kuaminisha jamii kwamba hata chadema nako kuna migogoro siyo CCM tuu,watengeneza propaganda watatumia magazeti uchwara ya Jamhuri ya waandishi kama Balile,Jackton Manyerere ambao maisha yao yote wamekataa kufikilisha akili zao na kuwa watumwa wa kubwa,hawana jipya watazunguka katika kuandika ujinga ,hakuna mtu atawajibu viongozi hao wataendelea kujenga chama
wameshindwa kupenya ndani hata hawajui watumie mbinu gani kuvuruga chama kabla ya 2014 uchaguzi wa serikali za mitaa wanajua kabisa kimbunga chao ni kuanzia wakati huo
Jamhuri na Tazama yanasomwa na nani magazeti yanalipiwa na kodi zetu yenyewe tuyaruhusu yavuruge demokrasia thubutu
@ Mwitongo wewe ni Jackton Manyerere embu safisha akili yako mbaya
 
  1. Acha CCM wamalizane wenyewe. Jamhuri ni mali ya Lowasa na Habari leo wanatumia hela za watanzania kueneza chuki dhidi ya watanzania. CCM na serikali yake ndio wanazidi kujichimbia kaburi lakini wa.tz wawe makini na maadui wao hawa CCM na serikali yao
 
Walioelimika ni wachache sana. Kweli, ukitaka kumficha Mwafrika kitu, kiweke kwenye maandishi. Unapinga kuwa Chadema hakuna mgpgoro? Mbona hapa hapa JF kuna uzi unaohusu migogoro ndani ya BAVICHA? Mbona kila leo kunaelezwa vurugu za Shibunda ndani ya CDM? Je, Mbowe na Slaa wanapikika chungu kimoja? Yote haya yapo, lakini kwa ujinga wa kutotaka kuyasoma, mnakimbilia kulishutumu Gazeti. Kukiri tatizo ni moja ya njia za kuelekea kulitatua! Tukubali kwamba tuna matatizo ndani ya chama, then kuanzia hapo tuone namna ya kusonga mbele. Kujitawaza kwa majani ya mgomba hakusaidii kuijenga Chadema.
All in all wewe huna udhu wala credibility ya kuishauri chochote Chadema kwa sababu nakumbuka vizuri wakati upo Gazeti lile la Fisadi papa ulideclare kabisa Interest kwamba msimamo wa Gazeti lenu mnaiunga mkono CCM. Sasa leo upo Gazeti la Jamhuri umebadilika kipi? wewe si ndiye yule yule?
 
Hivi ccm ina maana mmeshindwa kabisa kupandisha chati chama chenu hadi kionekane bila kutaka kupoteza chadema? Najua chadema kimewafunika lakini mnaweza kufanya miujiza mkaibukia juu badala ya haya mnayoyafanya. Kwa hiyo Watanzania hawana jipya la kutegemea kutoka kwenu. Na kwa kujua hamna jipya, mnatafuta namna ya kuchanachana CDM ili muonekane japo katika kiwango chenu kinachonuka.

Mmeshindwa. La msingi mkubali kwamba chama chenu kimekufa na hamna namna ya kukifufua. Vinginevyo mnazidi kuwashangaza wa Tanzania vile mnavyohangaika na CDM.
 
Wapenzi wa CCM wana matatizo kwelikweli!

kila move yao tunayo wajinga wakubwa wanaenda kununua kadi za cdm na kuzipiga picha tuletee kwenye vichwa vya magazeti kana kwamba wanavuna makamanda ili waupotoshe uma! Kwa taarifa yao agenda zao za dom na vikao vyote vya siri vya kuipunguza chadema kasi vigota mwamba!
Tukumbuke waziri mkuu Pinda iliwahi kusema "chadema inainyima usingizi serikali" mpaka kufikia hatua hii kwa kiongozi wakitaifa serikalini na chamani(ccm) ni dhahiri wamelitingishwa kweli !
NCCR,CUF na TLP walimalizwa nguvu enzi ya mangula na kinana na watz walikuwa hawajakaa sawa na elimu ya kiraia sasa kumekucha na wameamua kuwarudisha ili waje michezo ilee ,lakini wameanza kula moto! Na kama Mungu ameamua mageuzi,hata wangeweza kurudisha enzi nyuma haitawezekana!
Tumeona picha ya matukio yanayoendelea ! Lakini 2015 dunia inakwenda kushuhudia mageuzi makubwa tz!!
 
Mwitongo-Inaonyesha Mwitongo wewe ndiye mwandishi wa hii habari.Umejionyesha jinsi ulivyo kanjanja.Unaungaunga habari za Chadema za tangu uchaguzi wa chama miaka 4 iliyopita ili kuhalalisha kitumbua chako.Mtu yeyote aliyesoma hii habari atalipuuza hili gazeti milele.Eti Chadema itakufa kwa sababu Heche na Waitara wanagombea jimbo la Tarime.Hakika mmejionyesha ni watu wa aina gani.Ni afadhali kusoma magazeti ya udaku kuliko Jamhuri.
Mngekuwa na hata chembe ya akili mngetafuta yale mahojiano ya Zitto na JF aliweka wazi mgawanyo wa kazi katika M4C..Mmeonyesha mlivyo vipofu.
 
Last edited by a moderator:
Mwitongo-Inaonyesha Mwitongo wewe ndiye mwandishi wa hii habari.Umejionyesha jinsi ulivyo kanjanja.Unaungaunga habari za Chadema za tangu uchaguzi wa chama miaka 4 iliyopita ili kuhalalisha kitumbua chako.Mtu yeyote aliyesoma hii habari atalipuuza hili gazeti milele.Eti Chadema itakufa kwa sababu Heche na Waitara wanagombea jimbo la Tarime.Hakika mmejionyesha ni watu wa aina gani.Ni afadhali kusoma magazeti ya udaku kuliko Jamhuri.
Mngekuwa na hata chembe ya akili mngetafuta yale mahojiano ya Zitto na JF aliweka wazi mgawanyo wa kazi katika M4C..Mmeonyesha mlivyo vipofu......
 
Last edited by a moderator:
Walioelimika ni wachache sana. Kweli, ukitaka kumficha Mwafrika kitu, kiweke kwenye maandishi. Unapinga kuwa Chadema hakuna mgpgoro? Mbona hapa hapa JF kuna uzi unaohusu migogoro ndani ya BAVICHA? Mbona kila leo kunaelezwa vurugu za Shibunda ndani ya CDM? Je, Mbowe na Slaa wanapikika chungu kimoja? Yote haya yapo, lakini kwa ujinga wa kutotaka kuyasoma, mnakimbilia kulishutumu Gazeti. Kukiri tatizo ni moja ya njia za kuelekea kulitatua! Tukubali kwamba tuna matatizo ndani ya chama, then kuanzia hapo tuone namna ya kusonga mbele. Kujitawaza kwa majani ya mgomba hakusaidii kuijenga Chadema.

@ Mwitongo-Usijidhalilishe kama mtetea anayetaka kutaga...Tueleze wanajamvi...Mbowe na Dr Slaa hawapikiki kivipi chungu kimoja?
 
Wanataka kuaminisha jamii kwamba hata chadema nako kuna migogoro siyo CCM tuu,watengeneza propaganda watatumia magazeti uchwara ya Jamhuri ya waandishi kama Balile,Jackton Manyerere ambao maisha yao yote wamekataa kufikilisha akili zao na kuwa watumwa wa kubwa,hawana jipya watazunguka katika kuandika ujinga ,hakuna mtu atawajibu viongozi hao wataendelea kujenga chama
wameshindwa kupenya ndani hata hawajui watumie mbinu gani kuvuruga chama kabla ya 2014 uchaguzi wa serikali za mitaa wanajua kabisa kimbunga chao ni kuanzia wakati huo
Jamhuri na Tazama yanasomwa na nani magazeti yanalipiwa na kodi zetu yenyewe tuyaruhusu yavuruge demokrasia thubutu
@ Mwitongo wewe ni Jackton Manyerere embu safisha akili yako mbaya

Hivi wewe lini utaacha kumwandama manyerere? Kila mara ujinga wako unapotaka kuuonyesha lazima umtaje manyerere. ngoja aje akujibu maana huwa yumo humu.
 
Huo ni muendelezo wa ccm kuelekea kaburini! Tatizo magamba wanaona adui wao ni chadema! Wamemuacha adui yao mkuu ambaye ni ufisadi wanapigana na anae ona kuwa ufisadi ndio adui wa taifa hili. Wangejitahidi kumuuwa adui fisadi ndio waje waseme chadema inakufa! Pesa ziko uswis hawafanyi jitihada za kuzirejesha wao wana pambana na chadema wanaopiga kelele fedha hizo zirejeshwe. Ujinga mtupu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ni kweli tupu kaka CHADEMA haipaswi kutumia nguvu kubwa kujibu hoja mufilisi za ccm, bali inapaswa kuendeleza mikakati yake ya kuuelimisha umma wa waTanzania umuhimu wa kuiondoa ccm madarakani kwa manufaa ya taifa hili navizazi vijavyo.
Hizi propaganda zao zitumike kuimaliza kabisa ccm kule kwa wananchi.....
Wananchi waelezwe wazi namna fedha zao zinavyotumiwa vibaya kueneza propaganda chafu ilhali wanayaacha masuala ya msingI
Waelezwe kuwa ccm imeacha kwa makusudi kupambana na umaskini , kuboresha huduma za jamii, kuboesha kilimo, kupambana na rushwa na ufisadi, badala yake wanatumia pesa za umma na baadhi ya vyombo vya habari vya umma kupambana na CHADEMA ambayo inaishinikiza serikali ya CCM kuboresha maisha yao (wananchi).....HIVYO WATAMBUE KUWA CCM NDIO ADUI NAMBA MOJA WA USTAWI WA MAISHA YAO NA TAIFA LAO KWA UJUMLA.
HARAKATI ZA UKOMBOZI ZIENDELEE!
 
Wanachama, Viongozi na Wapenzi wa CHADEMA kuanza kupaza sauti huku wakivinyoshea vyama vingine vya siasa na kusema ndivyo vinavyochochea misuguano na makundi ndani ya chama chao ni kujaribu kuukimbia ukweli na hii ni dalili ya kulikimbia tatizo while feeling sorry for themselves. Historia inaonyesha kwa kufanya hivyo huku chama kikiwa hakina nguzo imara (political maturity) inakuwa ni chanzo cha sarambatiko kama ilivyotokea kwa NCCR-Mageuzi after 1994.

Historia inaonyesha kuwa, chama kinapoanza au kunapokuwa na mtaji wa kisiasa katika nchi ya kidemokrasia kinakuwa ni kama mzoga wa mnyama unaovutia na kukaribisha nzi, simba, mbwa mwitu, fisi na ndege kupigana vikumbo ili kupata angalau kidogo kinachopatikana kwa manufaa yao binafsi na dalili hizi zimeanza kujidhihilisha katika jukwaa la kisiasa nchini. Kwa wanaojua historia, mambo kama haya ni kawaida kutokea katika chama lakini vile vile yakiruhusiwa bila mpangilio huku chama kikiwa hakina pia nguzo imara ya kukabiliana na external pressure yanaweza kukiathiri hata kufikia hatua kukisarambatisha.

CHADEMA kama chama kilikuwa bado hakijakuwa tried & tested pamoja na kwamba kuna baadhi ya viongozi wake wameisha onja joto kali la kisiasa. Kama kuna viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA walikuwa wanafikilia kuwa CHADEMA is immune and everything is fine and rosy bado wanaota ndoto za mchana.

Kwa haya yanayoanza kutokea wafahamu kama ni utangulizi wa safari ndefu na ngumu ya kisiasa ndani ya chama. Hekima na busara za viongozi na wanachama wake ndiyo kitakachokinasua kutoka kwenye tanuru la moto mkali wa kisiasa ili kiwe tayari kupewa nchi kuiongoza otherwise, it'll be just another history nchini kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi.

Jaziba, matuzi, lawama, kejeri na kunyosha vidole hakuondoi ukweli halisia bali kinaongeza tatizo halisia ambapo matokeo yake sina haja kuyasema.
 
Back
Top Bottom