Kwanza kabisa ningependa kutoa taarifa sikuwepo hapa Jamvini kujibu bandiko hili kwa sababu ya tatizo la kukatika hovyo hovyo kwa umeme nikaamuwa kwenda Gym.Kwanza nikueleze ndugu yangu, acha matusi kwa sababu nikisema wewe ni nani na upo wapi, utapata mpasuko wa roho. Ukiendelea nitakupigia simu. Tuache hayo.
Kwanza huna hakika kama niliandika au nilihojiwa Star TV. Nakumbuka siku moja kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2010, nilihojiwa Star TV. Nikatamka wazi kuwa Musoma Mjini Chadema, chini ya mdogo wangu Vincent inashinda uchaguzi. Nikasema wazi kuwa Mathayo hana chake pale kwa sababu nimehudhuria mikutano na kujionea hali ya mambo. Nikaapa kwamba kama kweli CCM watashinda, basi tangu siku hiyo nitakubali kuwa CCM ni wezi wa kura waliokubuhu. Nakala ya mahojiano hayo ipo Star TV na kwa kweli watu wengi walinipigia simu wakihoji ni kwa namna gani najiaminisha Chadema watashinda. Kumbuka, Chadema, wakiwakilishwa na Vincent walishinda. Tena Musoma Mjini likawa jimbo la kwanza Tanzania kutangazwa matokeo.
Uzushi na uzandiki si asili yangu. Umetaja Mwitongo, sijui ni Mwitongo ya Butiama au Mwitongo wa Rwanda, maana Mwitongo maana yake ni mahameni. Nililo na hakika nalo ni kwamba ukizidisha matusi, sitosita kukuweka hadharani. Sitaki tufike huko, isipokuwa ikilazimu tu.
Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
Wala huna sababu ya kuangaika, Jackton Manyerere povu lilikuwa linamtoka ili bwana wake Rostam Azizi apate vitalu vingi vya uwindaji na vyenye wanyama wengi kupitia kampuni ambayo Rostam Aziz aliinunuwa inaitwa Miombo Safaris ambayo ilikuwa inamilikiwa na Mitchele pamoja na Wazungu wenzanke, ipo pale Masaki karibu na Mambo Club.Manyerere, leo umeingia choo cha jinsia tofauti na ya kwako, .....Hivi wewe unataka kujenga tena na hii ni mbinu ya kutishia na kuomba bati? ..... Hakika nitakufunua juu ya uzandiki wako na jinsi unavyoandika kutishia watu ili upate fedha .....uliandika sana kuhusu tasnia ya utalii wakati ukiwa habari cooperation na gazeti la mtanzania , mwisho wa siku unaenda kudai kuwa kibanda chako kinahitaji mabati na ikatumwa fedha kwenye akaunti yako .......hapa leo mnataka nini? Balile ya kwake ni kuanzia Hull, wakurugenzi wengine leo nawaacha huru.
Ntakuja jioni ya leo kwa saa za huku niliko kuwavua hawa jamaa wawili nguo hadharani na kuweka kivuli cha mabati , nawapa masaa yaliyobakia muombe radhi........
Kwanza kabisa ningependa kutoa taarifa sikuwepo hapa Jamvini kujibu bandiko hili kwa sababu ya tatizo la kukatika hovyo hovyo kwa umeme nikaamuwa kwenda Gym.
Back to the point, Matola is no body in this country na bandiko lako hili limejidhirisha jinsi unavyoweweseka kwa mimi kukuumbuwa kwa kujaribu kuwadanganya Watanzania kwa kudhani wote ni wavivu wa kufikiri na ni wepesi kusahau.
Mimi ndiye Matola halisi mwenye ID hii nakupa ruksa rasmi nitaje sasa hivi mimi ni nani na nina maslahi gani kwenye Media, Chadema, NGO na wanaharakati wengine zaidi ya mimi kuwa Mtanzania wa kawaida ambaye napigania Better Life for all and for puppets of CCM like you Jackton Manyerere.
Nimekupa muda wa kunitaja mpaka kesho asubuhi kabla sijafunguwa file lako rasmi ili nikuache uchi hapa hapa kwenye hii thread ndani ya JF. twende kazi sasa.
Manyerere, leo umeingia choo cha jinsia tofauti na ya kwako, .....Hivi wewe unataka kujenga tena na hii ni mbinu ya kutishia na kuomba bati? ..... Hakika nitakufunua juu ya uzandiki wako na jinsi unavyoandika kutishia watu ili upate fedha .....uliandika sana kuhusu tasnia ya utalii wakati ukiwa habari cooperation na gazeti la mtanzania , mwisho wa siku unaenda kudai kuwa kibanda chako kinahitaji mabati na ikatumwa fedha kwenye akaunti yako .......hapa leo mnataka nini? Balile ya kwake ni kuanzia Hull, wakurugenzi wengine leo nawaacha huru.
Ntakuja jioni ya leo kwa saa za huku niliko kuwavua hawa jamaa wawili nguo hadharani na kuweka kivuli cha mabati , nawapa masaa yaliyobakia muombe radhi........
Ni kweli kabisa kwamba nikiwa habari corporation, nimeandika sana habari za tasnia ya uwindaji wa kitalii. Lakini si hapo tu, tangu nikiwa Tanzania Daima, na sasa Jamhuri. Nimekuwa mmoja kati ya wengi sana waliofanikisha kuwapo kwa Sheria mpya na5 ya Wanyamapori ya mwaka 2010.
Nakiri kwamba nimejenga nyumba, na kwa kweli ningependa nijenge nyingine nyingi kadri inavyowezekana. Tamaa ya mtu mwenye akili ni kuwa na maendeleo, lakini maendeleo halali.
Nakiri kwamba nimesaidiwa sana kwenye ujenzi na mambo mengine muhimu yanayonihusu. Nimepata msaada kutoka kwa marafiki zangu wengi sana wa ndani na nje ya nchi. Nimepata msaada kutoka kwa marafiki wangu wengi walioko Iringa, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Nairobi, Washington, Cairo na sehemu mbalimbali. Ninachokanusha ni kwamba nimewahi kupata fedha kwa njia za vitisho. Hilo nalikanusha kwa nguvu zote.
Kusaidiwa kwangu kunatokana na utashi tu. Wenye akili timamu huomba kitu cha kuwafaa maishani, lakini wenye akili zilizo na mazonge wataishia kuomba michango ya harusi, kipaimara, jando, kitchen p; na kadhalika. Mimi siwezi kuomba hivyo vitu.
Kuwekewa fedha benki, haikutokea mara moja, mbili wala 10! ni mara nyingi sana nawekewa. Sababu za kufanya hivyo zipo wazi-nazo ni kulingana na mahitaji ya leo ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Kusafiri kwenda kupokea msaada kutoka kwa rafiki, hasa wakati huu wa ujambazi, ni hatari zaidi. Mbali na benki, kuna misaada naipokea kupitia M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money; na kadhalika. Weledi wangu wa kupima msaada wa kuomba umenisaidia leo kuwa na maisha ya kati. Si tajiri, na si masikini! Siombi chakula, bali mimi huomba mbegu! Hilo halina kificho na kwa kweli naona fahari. Naona fahari kwa sababu hakuna binadamu aliyeweza kufanikiwa yeye mwenyewe bila kusaidiwa. Narejea kusema kuwa sijapata kuomba msaada kwa vitisho; na ndiyo maana wapo walionisaidia kwa kutaka kunizima, lakini bado nikasimama kwenye maadili kupambana nao kwa ajili ya masilahi ya nchi yetu. Karibu sana.