Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

Hivi wewe lini utaacha kumwandama manyerere? Kila mara ujinga wako unapotaka kuuonyesha lazima umtaje manyerere. ngoja aje akujibu maana huwa yumo humu.
Jacton Manyerere wewe ni mjinga kiuandishi umeleta mada ambayo umeunga vipisi vya habari hakuna mtiririko umekuwa mwanaume kama mabinti wa kupenda dezo dezo huna akili moja ya kuchuma mali yako mwenyewe kwa kutumia taaluma yako sifa yako moja wewe unatumika kama tambara la deki ili kupata fedha,fedha ni fedheha hata vyombo vya habari vilikuwa vikualika sana kama mwandishi aliyebobea siku hizi huna lolote unaachwa solemba
 
Lwesye.Tunashukuru sana kwakutufumbua macho.
 
Last edited by a moderator:
Kitengo cha propaganda cha CCM kimeonekana kufanya kazi yake barabara sasa hivi na idadi kubwa ya magazeti imekuwa ikipiga propaganda kubwa dhidi ya CHADEMA sasa hivi.Kutokana na hali hiyo inatakiwa kitengo cha uenezi CHADEMA kiwe macho saa zote chini ya John Mnyika na Tumaini Makene.Pia umuhimu wa CHADEMA kuwa na vyombo vyake vya habari unazidi kuongezeka.

Chini ni baadhi ya magazeti ya leo:

Ni kawaida shetani akizeeka hujifanya malaika,kinachofanyika ni ukosefu wa scientific strategy ambazo wangesoma nyakati wangetafuta mbadala wa propaganda za maji taka.Kila siku watasema lakini mwisho wa siku kaburi linawangoja
 
Siku zote nimepuuza kujiunga humu. Msimamo wangu umesababishwa, si tu ya maudhui murua ya mtandao huu, bali shida ya kujibizana na "mizimu". Kwa msaada, leo nimejitahidi kuingia, tena kwa jina langu halisi bila kujificha. Naishi Kwembe-Kati, na kwa kweli mimi ni mmoja wa wazee-ndiyo maana naitwa Mzee wa Kwembe-Kati. Nasema wazi, kila utakaposoma Mzee wa Kwembe-Kati, ujue ni mimi Manyerere Jackton. Simu yangu ni 0759 488 955. e-mail yangu ni manyererej@hotmail.com.

Nimesoma matusi mengi yanayonilenga. Lakini nashindwa kujibu kwa sababu sijui namjibu nani? Hii ndiyo faida na hasara ya kujibizana na "mizimu". Kudhalilishana, au kushushiana hadhi kwa sababu tu ya Jamhuri imeandika nini, nadhani si sahihi. Lazima tuwe na ustaarabu. Wanaoliandamana Gazeti Jamhuri, hasa la leo, wajaribu kuingia ndani, wasome yaliyomo, na waone msimamo wa Gazeti. Nawakaribisha tubishane hoja za msingi. Matusi, kejeli ay husda haviwezi kuisaidia jamii yetu. Wanaonifahamu vema wanajua sijawahi kuwa mnafiki wala mchumia tumbo. Kwangu mimi, Tanzania na Watanzania ni zaidi ya kila kitu.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
 
Wana CDM hizo propaganda zinazoenezwa na CCM through all channels at the disposal zisipuuzwe bali iwe ni changamoto . Iwe ni threat that CDM must transform into opportunity (s) kwa kuendelea kueneza elimu ya uraia. Tuwalenge hayo makundi ambayo hajui kusoma na kuandika au wanajua lakini uwezo wa kuchambua mambo ni mdogo. Hawa nao ni wapiga kura na mtaji mkubwa ambao unaweza kuyumbishwa na propaganda. Tuliona IGUNGA yaliyotokea kwa kutumia kapeini chafu. Halafu sio kila sehemu ya Tanzania ni Arumeru, au Tarime au Mwanza. Kuna wengine ambao hawatakagi source nyingine ya habari mbali na vijiweni. Huko utasikia yule alikuwa anafundisha chuo cha majaji, marais na exaggerations za kila aina. Kwa hiyo tuendelee na M4C kwa style zote kutgemea na wakati na mahala.

Mungu Inbariki Tanzania. Mungu inabariki CDM
 
Siku zote nimepuuza kujiunga humu. Msimamo wangu umesababishwa, si tu ya maudhui murua ya mtandao huu, bali shida ya kujibizana na "mizimu". Kwa msaada, leo nimejitahidi kuingia, tena kwa jina langu halisi bila kujificha. Naishi Kwembe-Kati, na kwa kweli mimi ni mmoja wa wazee-ndiyo maana naitwa Mzee wa Kwembe-Kati. Nasema wazi, kila utakaposoma Mzee wa Kwembe-Kati, ujue ni mimi Manyerere Jackton. Simu yangu ni 0759 488 955. e-mail yangu ni manyererej@hotmail.com.

Nimesoma matusi mengi yanayonilenga. Lakini nashindwa kujibu kwa sababu sijui namjibu nani? Hii ndiyo faida na hasara ya kujibizana na "mizimu". Kudhalilishana, au kushushiana hadhi kwa sababu tu ya Jamhuri imeandika nini, nadhani si sahihi. Lazima tuwe na ustaarabu. Wanaoliandamana Gazeti Jamhuri, hasa la leo, wajaribu kuingia ndani, wasome yaliyomo, na waone msimamo wa Gazeti. Nawakaribisha tubishane hoja za msingi. Matusi, kejeli ay husda haviwezi kuisaidia jamii yetu. Wanaonifahamu vema wanajua sijawahi kuwa mnafiki wala mchumia tumbo. Kwangu mimi, Tanzania na Watanzania ni zaidi ya kila kitu.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam

Mzee wa Kwembe.Twende hoja kwa hoja gazeti lako limeandika Zitto hashiriki M4C lakini alipofanya mahojiano na JF aliweka bayana yeye kapangiwa majukumu gani ndani ya M4C.Sasa gazeti lako bila aibu limesema Zitto amesusia M4C are you serious? Au umeprove nyie ni makanjanja?
 
Kosa jingine ni hili; usisome habari kama wanavyofanya ndugu zetu wanaosoma maneno mawili kwenye kifungu cha Biblia na kutoa tafsiri!! Soma maudhui ya habari uone. Sisi wapenda mageuzi tunapenda sana kuiona Chadema ikiwa imara kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu. Tena nimshukuru msomaji mmoja hapa aliyesaidia kueleza hata yaliyo kwenye maoni ya leo ya Jamhuri. Isitoshe, nimeandika makala kulaani Mwenyekiti Musukuma kuwatenga wananchi wa Kata waliomchagua diwani wa Chadema. Yote haya ni mapenzi yetu kwa upinzani maana tunajua faida zake kwa ustawi wa nchi yetu. Shida ninayopata hapa ni watu kuzomoka tu kusoma headline au mistari miwili mitatu, badala ya kusoma gazeti lote na kuona kilichomo. Bei ya Jamhuri ni Sh 500 tu, sidhani kama kuna sababu ya kujaa upepo kwa kuhukumu Gazeti ambalo umeamua kusoma headline au mstari mmoja tu!

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
 
Jacton Manyerere wewe ni mjinga kiuandishi umeleta mada ambayo umeunga vipisi vya habari hakuna mtiririko umekuwa mwanaume kama mabinti wa kupenda dezo dezo huna akili moja ya kuchuma mali yako mwenyewe kwa kutumia taaluma yako sifa yako moja wewe unatumika kama tambara la deki ili kupata fedha,fedha ni fedheha hata vyombo vya habari vilikuwa vikualika sana kama mwandishi aliyebobea siku hizi huna lolote unaachwa solemba

Hii ndiyo akili tunayotarajia ielete mabadliko ya kweli katika Taifa letu!! tuna kazi kweli kweli. Tujitahidi kujenga hoja bila matusi. Si kweli kwamba ukitaka kueleweka vizuri, basi lazima utukane. Tutumie hoja, hakuna aliye mkamilifu!

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
 
Kosa jingine ni hili; usisome habari kama wanavyofanya ndugu zetu wanaosoma maneno mawili kwenye kifungu cha Biblia na kutoa tafsiri!! Soma maudhui ya habari uone. Sisi wapenda mageuzi tunapenda sana kuiona Chadema ikiwa imara kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu. Tena nimshukuru msomaji mmoja hapa aliyesaidia kueleza hata yaliyo kwenye maoni ya leo ya Jamhuri. Isitoshe, nimeandika makala kulaani Mwenyekiti Musukuma kuwatenga wananchi wa Kata waliomchagua diwani wa Chadema. Yote haya ni mapenzi yetu kwa upinzani maana tunajua faida zake kwa ustawi wa nchi yetu. Shida ninayopata hapa ni watu kuzomoka tu kusoma headline au mistari miwili mitatu, badala ya kusoma gazeti lote na kuona kilichomo. Bei ya Jamhuri ni Sh 500 tu, sidhani kama kuna sababu ya kujaa upepo kwa kuhukumu Gazeti ambalo umeamua kusoma headline au mstari mmoja tu!

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam

Manyerere,

Nimecheka sana hilo jibu lako.Hiyo habari ina maudhui gani? Habari ya kuungaunga eti tangu Zitto amegombea uenyekiti na Mbowe? Utasemaje maudhui wakati Zitto ametoa majibu yote hapa JF katika mahojiano? Wewe umetumia maneno ya mitaani unaacha majibu ya Zitto mwenyewe huo ni uandishi?

John Heche kugombea jimbo na Waitara ndiyo kitu kikubwa cha Chadema kufa?

John Heche kugombana na Shonza ndiyo iwe sababu ya kupamba gazeti lako lote juu kuwa Chadema inakufa? You are Joking.

Halafu kwa ustadi mkubwa ukaonyesha Chadema inaangamia eti kwa vile Kinana amekuwa Katibu mkuu.Very Funny...
 
Mkuu Manyerere

Jamhuri lilikuwa ni gazeti langu pendwa after Mwanahalisi.Lakini baada ya kuona ile habari yenu ya leo nimeamini wote mko kwenye Payroll.Mtu ambaye hajanunuliwa hawezi kuandika habari ya uongo na ya kijinga kama ile.
 
Ndugu yangu, ukimpenda mwenye chongo utasema ana kengeza tu! Sote tunayapenda mabadiliko. Kuto hadhari ya jambo ni kitu muhimu sana. Hatutaki tena tuingine kwenye adha na hasara kubwa sana kidemokrasia iliyotupata kwa kusambaratika kwa NCCR-Mageuzi. Nashukuru kwamba hii Part I imewagusa watu, lakini naamini waandishi wetu walioandika habari hii wanajiandaa kuja Part II. Hii yote, bila shaka, itakuwa imelenga kuvunja nguvu zote za kishetani zinazotaka kukiangamiza Chama hiki ambacho kimejitokeza kuwa tumaini la Watanzania wengi. Kama mmoja alivyosema hapa, kujua tatizo ni moja ya hatua za kulitatua. Chadema lazima wawe kitu kimoja. CUF vivyo hivyo. Ukweli mwingine unakuwa mchungu, lakini ni lazima tuukubali. Tofauti na Chadema, CCM imeshakuwa taasisi-bila kujali ubovu na udhaifu wao. Chadema bado ipo kwenye safari ya kujijenga kuwa taasisi, hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa misuguano yote isiyo na maana inadhibitiwa haraka bila kuleta madhara.

Ndugu yangu FMpiganaji, wala usikate tamaa. Ndani ya hili Gazeti la leo kuna makala nyingi na nzito sana zinazolenga kujenga ustawi wa Chadema. Wala usikatishwe tamaa. Pengine mapenzi yako kwa Chadema ni makubwa sana sana kiasi kwamba hutaki iguswe. Endelea kuisoma Jamhuri, utafaidi mengi-ushauri, maonyo, mafunzo na changamoto za huko tunakopaswa kuelekea.
 
Watapambana sana lakini hawatashinda,mwisho wa siku watanzania watadai Yale maisha bora waliyoahidiwa.....Nepi na mr elephant mkiongozwa na Mzee chichidodo kazi mnayo
 
Ndugu yangu, ukimpenda mwenye chongo utasema ana kengeza tu! Sote tunayapenda mabadiliko. Kuto hadhari ya jambo ni kitu muhimu sana. Hatutaki tena tuingine kwenye adha na hasara kubwa sana kidemokrasia iliyotupata kwa kusambaratika kwa NCCR-Mageuzi. Nashukuru kwamba hii Part I imewagusa watu, lakini naamini waandishi wetu walioandika habari hii wanajiandaa kuja Part II. Hii yote, bila shaka, itakuwa imelenga kuvunja nguvu zote za kishetani zinazotaka kukiangamiza Chama hiki ambacho kimejitokeza kuwa tumaini la Watanzania wengi. Kama mmoja alivyosema hapa, kujua tatizo ni moja ya hatua za kulitatua. Chadema lazima wawe kitu kimoja. CUF vivyo hivyo. Ukweli mwingine unakuwa mchungu, lakini ni lazima tuukubali. Tofauti na Chadema, CCM imeshakuwa taasisi-bila kujali ubovu na udhaifu wao. Chadema bado ipo kwenye safari ya kujijenga kuwa taasisi, hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa misuguano yote isiyo na maana inadhibitiwa haraka bila kuleta madhara.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam

Nimekuuliza maswali ma3 na hujanijibu hata moja bali umeleta tu Riwaya za siku zote zinazozungumzwa kwenye mikutano ya CCM.Na ili kukamilisha mradi wa CCM ukaona hiyo habari yako uikamilishe kwa kumhoji Kinana eti azungumzie mgogoro ndani ya Chadema...

Lakini mnapaswa kufahamu watanzania wa sasa siyo wa miaka ya nyuma.Habari yenu haina viwango vyovyote vya kuitwa habari.Ni vyema mkajifunza uandishi wa gazeti kama Raia Mwema.

Mliona ni Rahisi zaidi kwenda Lumumba kumhoji Kinana habari za Chadema badala ya kumfuata Dr Slaa Kinondoni kumhoji.

Naona habari ya leo imewafurahisha sana na ndiyo maana ukasema unakuja na Part 2,nawashauri isiwe Part 2 tu bali njooni na mpaka Part 5.Lakini mjue kwamba watu wengi wamewaweka kundi moja na magazeti ya Uhuru Publication.
 
Usiwe mkali, nakumbuka wakati fulani mwanahalisi walimwandika zitto kina ninyi mkaibuka na kusema Kubenea kanunuliwa na CCM! Tuyaache hayo. Jamhuri litaendelea kuwa Gazeti lisilofungamana na upande wowote. Tena basi, usiwe na hasira, maana hasira hazisaidii. Kubali tu kwamba tunapaswa kui-shape Chadema ili itekeleze maudhui ya kuanzishwa kwake.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
 
Sasa itabidi tuanze kusoma magazeti ya Kenya, Tanzania hatuna waandishi labda tuanze kuajili waandishi wa kigeni.

Manyerere Jackton last election alitamka wazi wao wanaiunga Mkono CCM kwanza atueleze ni lini alitangaza kuacha kuinga mkono ndio tuongee hoja kwa hoja, otherwise ni porojo tupu.

Do not trust empty stomach.
 
Ndugu zangu, heshima ya JF inashuka kwa uzushi na mambo ya kutunga ya aina hii. Last election anayoisema huyu ndugu sikupata na wala sijawahi kuandika au kutamka popote kwamba naiunga mkono CCM. Kama ushahidi wa hilo upo, nakubali nisutwe na laana ya unafiki wangu iniangukie. Sijawahi kufanya kitu cha aina hiyo. Wanaonijua, wanaelewa ninachokisema. Narudia, kama kweli upo ushahidi wangu wa maandishi (maana magazeti yanatunzwa), nisutwe. Sijawahi kufanya kazi ya kuifia CCM. Lakini ni ajabu, ukiwa na CCM wanasema mimi ni mpinzani, ukiwa upinzani unaambiwa CCM. Sioni ubaya wa haya, hasa ikizingatiwa kuwa I'm after my country!

manyerere Jackton

Kwembe-Kati
Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom