Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

Ndugu zangu, heshima ya JF inashuka kwa uzushi na mambo ya kutunga ya aina hii. Last election anayoisema huyu ndugu sikupata na wala sijawahi kuandika au kutamka popote kwamba naiunga mkono CCM. Kama ushahidi wa hilo upo, nakubali nisutwe na laana ya unafiki wangu iniangukie. Sijawahi kufanya kitu cha aina hiyo. Wanaonijua, wanaelewa ninachokisema. Narudia, kama kweli upo ushahidi wangu wa maandishi (maana magazeti yanatunzwa), nisutwe. Sijawahi kufanya kazi ya kuifia CCM. Lakini ni ajabu, ukiwa na CCM wanasema mimi ni mpinzani, ukiwa upinzani unaambiwa CCM. Sioni ubaya wa haya, hasa ikizingatiwa kuwa I'm after my country!

manyerere Jackton

Kwembe-Kati
Dar es Salaam
Wewe Manyerere ni Mnafki mkubwa, unakumbuka vyema hiki kitu au msimamo huu haukuandikwa kwenye magazeti bali ulikuwa unahojiwa na Star Tv kama sikosei, na ukatoa msimamo wa Gazeti lenu kwamba mnamuunga mkono JK na CCM.

JF kuna kila aina ya wataalam wa kufanya searching kwa taarifa wanazohitaji, naomba wanajamvi kama kuna mtu mwenye uwezo wa kutafuta Interview alizowahi kufanya huyu Manyerere mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu video clip mtaipata.

Hapa anachojaribu kuskip Manyerere ni kujionesha kwamba ni mtu huru wakati si kweli, na habari hii niya malipo maalum kwa kazi aliyoifanya.

Nakala kwa Mwitongo.
 
Kwanza nikueleze ndugu yangu, acha matusi kwa sababu nikisema wewe ni nani na upo wapi, utapata mpasuko wa roho. Ukiendelea nitakupigia simu. Tuache hayo.

Kwanza huna hakika kama niliandika au nilihojiwa Star TV. Nakumbuka siku moja kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2010, nilihojiwa Star TV. Nikatamka wazi kuwa Musoma Mjini Chadema, chini ya mdogo wangu Vincent inashinda uchaguzi. Nikasema wazi kuwa Mathayo hana chake pale kwa sababu nimehudhuria mikutano na kujionea hali ya mambo. Nikaapa kwamba kama kweli CCM watashinda, basi tangu siku hiyo nitakubali kuwa CCM ni wezi wa kura waliokubuhu. Nakala ya mahojiano hayo ipo Star TV na kwa kweli watu wengi walinipigia simu wakihoji ni kwa namna gani najiaminisha Chadema watashinda. Kumbuka, Chadema, wakiwakilishwa na Vincent walishinda. Tena Musoma Mjini likawa jimbo la kwanza Tanzania kutangazwa matokeo.

Uzushi na uzandiki si asili yangu. Umetaja Mwitongo, sijui ni Mwitongo ya Butiama au Mwitongo wa Rwanda, maana Mwitongo maana yake ni mahameni. Nililo na hakika nalo ni kwamba ukizidisha matusi, sitosita kukuweka hadharani. Sitaki tufike huko, isipokuwa ikilazimu tu.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
 
quote_icon.png
By Molemo

Mzee wa Kwembe.Twende hoja kwa hoja gazeti lako limeandika Zitto hashiriki M4C lakini alipofanya mahojiano na JF aliweka bayana yeye kapangiwa majukumu gani ndani ya M4C.Sasa gazeti lako bila aibu limesema Zitto amesusia M4C are you serious? Au umeprove nyie ni makanjanja?
Kosa jingine ni hili; usisome habari kama wanavyofanya ndugu zetu wanaosoma maneno mawili kwenye kifungu cha Biblia na kutoa tafsiri!! Soma maudhui ya habari uone. .........

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam

Bado haujamjibu Molemo. Kwani kumfafanulia Molemo hoja yake inahitaji sentensi ngapi ! Jibu hoja yake.
 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya kwao ni kuwa hayo magazeti hayatawezesha mabadiliko yanayohitajika leo na wananchi (wapiga kura). Kusema CHADEMA inakufa hakupunguzi ukali wa maisha, hakuboreshi elimu wala kuboresha huduma za afya.

Waache waandike, na wakiona haitoshi waandike tena na tena. Mavi ya kuku!

Kweli mkuu! CCM wanalenga kwenye wrong target, hawajamuona adui yao bado. Wanatapatapa tu kama mfa maji, mara akamate gogo, mara ubua hata unyoya anakamata akiamini unaweza kumuokoa... Mwisho lazima watoweke ila kwa kuwa CCM ni dubwana kubwa kama mbuyu kwenye shamba la migomba, unapoanguka baadhi ya migomba haiwezi kusalimika. Kitengo cha uenezi cdm kiangalie namna ya kupunguza madhara yanayotokana na propaganda izi chafu na kukabiliana nazo sawa sawa!
 
Nimefurahi mzee wa Kwembe -Kati- Manyerere Jacton anakuja kujibu hoja hapa hivi ndio inavyofaa wote tunajenga nyumba moja tusigombee fito,Manyerer katika uandishi wako ungetupa na majibu ya wahusika kwa maana ya maoni yao tungekufurahi zaidi wasomaji lakini kwa sababu unataka kuwafurahisha watu fulani wewe uliona ni bora utoe hiyo heading ukijua utakuwa umetimiza lengo
 
Ujinga wa watanzania walio wengi ndio mtaji wa magamba, hivyo si rahisi kwa mtu mwerevu yeyote kuyumbishwa na propaganda na siasa mufilisi kama hizi.
Bado hapa hatujaona jitiahada zozote za dhati zinazofanywa na serikali ya ccm za kumfanya mwananchi apate maisha bora isipokuwa jitihada wanazofanya sasa ni kupambana na CHADEMA na DR SLAA tu. huku watanzania wengi masikini huko vijijini wakiendelea kuishi kwa kula mlo mmoja kwa siku.

siku zote mfa maji haachi kutapatapa.Cha msingi hapa sio hupoteza muda kwa kulumbana nao ila kuendelea kusambaza sera za CDM kwa wananchi, Viongozi wake wote wa juu waendelee kutangza sera kila kona.
 
Siku zote nimepuuza kujiunga humu. Msimamo wangu umesababishwa, si tu ya maudhui murua ya mtandao huu, bali shida ya kujibizana na "mizimu". Kwa msaada, leo nimejitahidi kuingia, tena kwa jina langu halisi bila kujificha. Naishi Kwembe-Kati, na kwa kweli mimi ni mmoja wa wazee-ndiyo maana naitwa Mzee wa Kwembe-Kati. Nasema wazi, kila utakaposoma Mzee wa Kwembe-Kati, ujue ni mimi Manyerere Jackton. Simu yangu ni 0759 488 955. e-mail yangu ni manyererej@hotmail.com.

Nimesoma matusi mengi yanayonilenga. Lakini nashindwa kujibu kwa sababu sijui namjibu nani? Hii ndiyo faida na hasara ya kujibizana na "mizimu". Kudhalilishana, au kushushiana hadhi kwa sababu tu ya Jamhuri imeandika nini, nadhani si sahihi. Lazima tuwe na ustaarabu. Wanaoliandamana Gazeti Jamhuri, hasa la leo, wajaribu kuingia ndani, wasome yaliyomo, na waone msimamo wa Gazeti. Nawakaribisha tubishane hoja za msingi. Matusi, kejeli ay husda haviwezi kuisaidia jamii yetu. Wanaonifahamu vema wanajua sijawahi kuwa mnafiki wala mchumia tumbo. Kwangu mimi, Tanzania na Watanzania ni zaidi ya kila kitu.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam

Manyerere
Nilikuwa nadhani Jamhuri ni gazeti huru la habari.Kumbe nilipotea sana.Sijawahi kuona mtu unaandika habari ya kukandamiza mtu halafu unaenda kuomba maoni ya hiyo habari kwa adui yake huyo mtu.
Wewe bila aibu umeandika habari ya kuivuruga CDM kwa makusudi huku ukijua malengo yako mwenyewe ya kuandika hiyo habari halafu bila aibu unakimbilia ofisini kwa Kinana kuomba maoni yake.Hapo umejidhihirisha unavyotumika na ulivyo mtupu.
Halafu ulivyo mnafiki na muongo umemhoji Marando huku ukihitimisha eti Marando alimkimbia Mrema NCCR wakati hata mtoto mdogo anaelewa Mrema ndiye aliyemwachia Marando NCCR akaenda TLP.
Uandishi wa aina yako ni aibu na unajidhalilisha sana.Ile imani ndogo mliyoanza nayo kwenye gazeti lenu imepotea kabisa.Utaombea sana na kuandika chochote kwa malipo ili kusambaratisha CDM lakini nakuhakikishia Mungu akiamua kuilinda hamtafanikiwa.
Walau magazeti yaliyo huru sasa hivi ni Raia Mwema,Mwananchi na Nipashe.Tuombe Mungu shetani asijipenyeze na huko.
 
hayo magazeti nyumbani kwangu nanunua kwa ajili ya kuwashia moto...
 
Kwanza nikueleze ndugu yangu, acha matusi kwa sababu nikisema wewe ni nani na upo wapi, utapata mpasuko wa roho. Ukiendelea nitakupigia simu. Tuache hayo.

Kwanza huna hakika kama niliandika au nilihojiwa Star TV. Nakumbuka siku moja kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2010, nilihojiwa Star TV. Nikatamka wazi kuwa Musoma Mjini Chadema, chini ya mdogo wangu Vincent inashinda uchaguzi. Nikasema wazi kuwa Mathayo hana chake pale kwa sababu nimehudhuria mikutano na kujionea hali ya mambo. Nikaapa kwamba kama kweli CCM watashinda, basi tangu siku hiyo nitakubali kuwa CCM ni wezi wa kura waliokubuhu. Nakala ya mahojiano hayo ipo Star TV na kwa kweli watu wengi walinipigia simu wakihoji ni kwa namna gani najiaminisha Chadema watashinda. Kumbuka, Chadema, wakiwakilishwa na Vincent walishinda. Tena Musoma Mjini likawa jimbo la kwanza Tanzania kutangazwa matokeo.

Uzushi na uzandiki si asili yangu. Umetaja Mwitongo, sijui ni Mwitongo ya Butiama au Mwitongo wa Rwanda, maana Mwitongo maana yake ni mahameni. Nililo na hakika nalo ni kwamba ukizidisha matusi, sitosita kukuweka hadharani. Sitaki tufike huko, isipokuwa ikilazimu tu.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam
we manyerere sijui.... umeiingia choo cha kike...tushajua njama zenu nyie...msitukute sie vilaza... CHADEMA SIO YA WAJINGA....pelekeni pumba zenu mahala pengine....nashukuru... sijakutukana mahala popote...natumaini umenielewa...eti eeeh???
 
Kwanza
nikueleze ndugu yangu, acha matusi kwa sababu nikisema wewe ni nani na
upo wapi, utapata mpasuko wa roho. Ukiendelea nitakupigia simu. Tuache
hayo.

Kwanza huna hakika kama niliandika au nilihojiwa Star TV. Nakumbuka siku
moja kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2010, nilihojiwa Star TV. Nikatamka
wazi kuwa Musoma Mjini Chadema, chini ya mdogo wangu Vincent inashinda
uchaguzi. Nikasema wazi kuwa Mathayo hana chake pale kwa sababu
nimehudhuria mikutano na kujionea hali ya mambo. Nikaapa kwamba kama
kweli CCM watashinda, basi tangu siku hiyo nitakubali kuwa CCM ni wezi
wa kura waliokubuhu. Nakala ya mahojiano hayo ipo Star TV na kwa kweli
watu wengi walinipigia simu wakihoji ni kwa namna gani najiaminisha
Chadema watashinda. Kumbuka, Chadema, wakiwakilishwa na Vincent
walishinda. Tena Musoma Mjini likawa jimbo la kwanza Tanzania kutangazwa
matokeo.

Uzushi na uzandiki si asili yangu. Umetaja Mwitongo, sijui ni Mwitongo
ya Butiama au Mwitongo wa Rwanda, maana Mwitongo maana yake ni mahameni.
Nililo na hakika nalo ni kwamba ukizidisha matusi, sitosita kukuweka
hadharani. Sitaki tufike huko, isipokuwa ikilazimu tu.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
Dar es Salaam

Mkuu muweke mbona yeye kakutaja
 
we manyerere sijui.... umeiingia choo cha kike...tushajua njama zenu nyie...msitukute sie vilaza... CHADEMA SIO YA WAJINGA....pelekeni pumba zenu mahala pengine....nashukuru... sijakutukana mahala popote...natumaini umenielewa...eti eeeh???

Hakuna njama zozote katika habari hii. Muhimu, na pengine someni maoni ya mhariri, ni kuipa hadhari Chadema ili iwe imara zaidi kwa ajili ya ustawi wa demokrasia nchini mwetu. Kila mwenye akili angependa kuona Chadema inakuwa imara zaidi na zaidi.

Manyerere Jackton
Kwembe-Kati
 
Mkuu muweke mbona yeye kakutaja

JF naamini ni uwanja wa hoja, na si kuonyeshana umahiri wa kuumbuana. Fikiria, mtu akikusingizia kwamba wewe ni shoga, na wewe ukamjibu, "mbona na wewe ni shoga"-tofauti yenu itakuwa ipi? Hapa tujadili hoja, lakini nimesema hakuna wa kujificha hapa. Tunafanya heshima tu. Tuna mambo muhimu sana ya kitaifa ya kujadili.

Manyerere Jackton
 
kimsingi ni kwamba vyama vikongwe barani afrika kikiwemo ccm vinatakiwa kuondoka na kupisha mawazo mbadala yenye muelekeo wa sasa uchukue nafasi ,hakuna haja ya kupoteza muda na magazeti haya kwa kulinda watu wasiolindika ,badala yake magazeti haya yatumike kueleza ukweli wa fedha zilizo fichwa uswisi na jinsi walivyozipata hawa viongozi ,waeleze kero za maji kwa wananchi ,kero za ada za wanafunzi na kero nyingine nyingi .
 
Magazeti yote hayo yalishaacha 'ETHICS' za uandishi na kibaya zaidi yanalindwa na Habari Maelezo. Habari ni ile iliyotoka source zenye ukweli na uwazi siyo za kutoka upande mmoja tena ni mawazo ya mwandishi au kikundi. Juma lililopita kuna mawandishi mmoja aliandika juu ya Wenje, nikadhani kuna habari kumbe upuuzi mtupu.! Makala yote haina hata chanzo cha taarifa. Media kama hizi zizakununua kabisa, hazijenge TAIFA. Yatawakuta kama yaliyompata wale waliokuwa wanaandika habari za uongo dhidi ya SUMAYE, alipowakaba koo ikabidi kuomba msamaha tena kwa kupiga magoti.
 
Mi sina wasi wasi napropaganda za magamba maana mwananchi waleo ni mwelewa hadanganyiki anapima kauli yamaisha bora niipi sukari kilo moja kutoka elf kwenda elf mbili miatano namkate kutoka mia nane kwenda elfu mbili .
 
Bado haujamjibu Molemo. Kwani kumfafanulia Molemo hoja yake inahitaji sentensi ngapi ! Jibu hoja yake.

Mkuu Mpiga Kelele.Hana cha kunijibu na mtu yeyote aliyefuatilia hii thread tangu mwanzo ameelewa mchezo wote ulivyochezwa Lumumba.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom