Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

Ushahidi wa CHADEMA kuinyima CCM usingizi ni huu..

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Kitengo cha propaganda cha CCM kimeonekana kufanya kazi yake barabara sasa hivi na idadi kubwa ya magazeti imekuwa ikipiga propaganda kubwa dhidi ya CHADEMA sasa hivi.Kutokana na hali hiyo inatakiwa kitengo cha uenezi CHADEMA kiwe macho saa zote chini ya John Mnyika na Tumaini Makene.Pia umuhimu wa CHADEMA kuwa na vyombo vyake vya habari unazidi kuongezeka.

Chini ni baadhi ya magazeti ya leo:
 
Wanapoteza muda wao tu.Propaganda za aina hii zimepitwa na wakati.
 
Ni kweli CHADEMA inabidi ije kivingine katika kupangua hoja dhaifu za CCM japo vigazeti vyenyewe usomekaji wake si mkubwa sana miongoni mwa jamii lakini si vya kukalia kimya.
 
Ni kweli CHADEMA inabidi ije kivingine katika kupangua hoja dhaifu za CCM japo vigazeti vyenyewe usomekaji wake si mkubwa sana miongoni mwa jamii lakini si vya kukalia kimya.
hakuna sababu ya kujibu huu upuuzi. just get focused on the main agenda. ufisadi,uwajibikaji,social welfare, period. kila utakapozungumzia haya na mengine ndio unavyoona mapunguvu makubwa ya ccm na uhitaji wa kuwaondoa unaongezeka zaidi.
 
Huo ni muendelezo wa ccm kuelekea kaburini! Tatizo magamba wanaona adui wao ni chadema! Wamemuacha adui yao mkuu ambaye ni ufisadi wanapigana na anae ona kuwa ufisadi ndio adui wa taifa hili. Wangejitahidi kumuuwa adui fisadi ndio waje waseme chadema inakufa! Pesa ziko uswis hawafanyi jitihada za kuzirejesha wao wana pambana na chadema wanaopiga kelele fedha hizo zirejeshwe. Ujinga mtupu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hii nguvu wangeitumia kurudisha pesa zetu zilizoko Uswiss na kuchukulia hatua MAFISADI hakika wangeeleweka.
 
Si mara ya kwanza tunaona magazeti yakitafuta namna ya kuimaliza CDM lakini siku zote ukweli unajulikana kuwa hizi ni mbinu chafu katika kupunguza kasi ya chama kuwafikia na kukubalika kwa wananchi.

 
.....naomba kuuliza swali hivi magazeti haya huwa yanauzwa au yanagawiwa bure ?? ni nani analipia gharama za uzalishaji na usambazaji wa magazeti haya kwa sababu nina wasiwasi isiwe kodi zetu ndio zinatumika kugharamia utumbo huu.
 
ni lazima tufahamu kwamba moja kati ya silaha kubwa ya maendeleo kiuchumi,kisiasa,kijamii,kitamaduni etc kwenye hii dunia ya leo ni media, ni lazima CDM nao kwa upande wao wajipange kukabiliana na huu mpango wa kuwapoteza au kuwaondoa kwenye hoja za msingi za kimaendeleo na kupigania rasilimali za nchi, wakaishia kufanya siasa za majitaka kupitia media
 
Ujinga wa watanzania walio wengi ndio mtaji wa magamba, hivyo si rahisi kwa mtu mwerevu yeyote kuyumbishwa na propaganda na siasa mufilisi kama hizi.
Bado hapa hatujaona jitiahada zozote za dhati zinazofanywa na serikali ya ccm za kumfanya mwananchi apate maisha bora isipokuwa jitihada wanazofanya sasa ni kupambana na CHADEMA na DR SLAA tu. huku watanzania wengi masikini huko vijijini wakiendelea kuishi kwa kula mlo mmoja kwa siku.
 
Bahati mbaya kwao ni kuwa hayo magazeti hayatawezesha mabadiliko yanayohitajika leo na wananchi (wapiga kura). Kusema CHADEMA inakufa hakupunguzi ukali wa maisha, hakuboreshi elimu wala kuboresha huduma za afya.

Waache waandike, na wakiona haitoshi waandike tena na tena. Mavi ya kuku!
 
.....naomba kuuliza swali hivi magazeti haya huwa yanauzwa au yanagawiwa bure ?? ni nani analipia gharama za uzalishaji na usambazaji wa magazeti haya kwa sababu nina wasiwasi isiwe kodi zetu ndio zinatumika kugharamia utumbo huu.
Kwahiyo wewe ulikuwa unategemea Magazeti haya hayatumii kodi yetu kujiendesha bila faida? anayekumbuka Arumeru hawezi kuingizwa mkenge na Propaganda uchwara, maana kule Arumeru hadi Wamasai wasiojuwa kusoma na kuandika walikuwa wanagaiwa bure magazeti ya Uhuru yaliyojaa Propaganda, lakini matokeo kila mtu anayajuwa kwenye sanduku la kura watu walifanya nini.
 
Ki ukweli ujinga wa wananchi wa tanzania ndi mtaji wa sisim......na kwa kujua hili sisim imeendelea kuwanyima wa tz elimu bora ili waendeleee kuwa wajinga na hivyo kuwa mtaji wao.
Mathalani .....watanzania wanaishi maisha duni huku pesa zao zikifichwa huku na kule mfano zilizoko uswisi lakini ajabu ni kuwa viongozi wa sisim hawafanyi jitihada za dhati kuzirejesha badala yake wao wakilala wakiamka wanafikiria waimbe wimbo gani kuhusu cdm!!!! Shem on them.
 
Magazeti yenyewe yanasomwa na ccm wenyewe, wenye akili timam huyaona kama uchafu tuu
 
Nina mapendekezo ya nini kifanyike kupitia idara ya propaganda ya cdm lakini hakika siwezi kuanika silaha za maangamizi hapa.
 
Mimi naona kitengo cha propaganda cha chadema ndicho kiko smart zaidi.,ndio na ni vizur ccm wakafikiria hivi hivi ya kwamba adui yao ni chadema,na kuacha kushughulikia mambo ya msingi,,
mwishowa siku sisi tutakuja kuwauliza tuh kuhusu utekelezaji wa ahadi zao na sio uadui wao na chadema
 
Back
Top Bottom