Ushahidi: Kikwete anakumbatia watoa/wala rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushahidi: Kikwete anakumbatia watoa/wala rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 255Texter, Sep 22, 2010.

 1. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa siku nyingi wananchi wa Tanzania tumekuwa tukisikia madai kwamba Rais wa nchi ni mtetezi au ni swahiba au anakumbatia watu wanasadikika kuhusika na vitendo vya rushwa, lakini madai hayo yamekuwa yakikanushwa na watu mbali mbali katika serikali na ndani ya CCM.

  Lakini hivi karibuni tumeona kwa uthibitisho, vitendo ambavyo vinaashiria bila kupingwa kwamba kiongozi huyu wa CCM ambaye anataka aongezewe muda mwingine wa miaka mitano ya uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kigeugeu inapokuja swala la kuonesha msimamo dhidi ya vitendo vya rushwa na wahusika wa vitendo hivyo. Uthibitisho wa picha na taarifa za wanahabari zimeonesha jinsi JK alivyowapigia chepuo tena bila aibu, wahusika wa vitendo vya rushwa kama Bw. Basil Mramba na Bw. Edward Lowassa, huku akimsafisha bila wasiwasi Bw. Lowassa toka ile kashfa ya Richmond.

  Sasa, cha ajabu kupita vyote, ni pale JK ambaye ni mwenyekiti wa CCM na ndiye aliyeongoza vikao vya NEC-CCM ambayo alitoa 'hukumu' dhidi ya watu mbalimbali akiwamo Bw. Frederick Mwakalebela ambaye alienguliwa toka nafasi ya kugombea ubunge wa Iringa mjini kwa madai kwamba alihusika katika rushwa. Bw. Mwakalebela hivi sasa anakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na vitendo vya rushwa, mashtaka ambayo pia yanamkabili na mkewe.

  Cha kustaajabisha ni kwamba huyu huyu mtuhumiwa wa rushwa ambaye CCM amemhukumu na kumuondoa kabisa katika nafasi ya kugombea ubunge, leo amekuwa ni mtu wa kukumbatiwa na JK.

  Ingawa mimi na wewe ambao tunaamini utawala wa sheria na haki ya kila binadamu, Bw. Mwakalebela tunamchukulia kwamba hana hatia hadi hapo itakapothibitishwa na mahakama kwamba kweli alihusika na vitendo vya rushwa na kuhukumiwa. Hivyo, mimi binafsi simhukumu. Ila NEC-CCM na huyu JK tayari walisha muona huyu bwana hafai, kwamba ni mtoa rushwa na ndiyo maana wakamuengua. Sasa huu unafiki wa JK kumkumbatia mtoa rushwa unaashiria nini? Je, ni mwendelezo wa kile kitabia cha JK cha kujichanganya na watoa rushwa? Au hii ndiyo inaashiria kwamba kesi ya Mwakalebela itapigwa zengwe na jamaa ataachiwa huru, kwa sababu ni "mwenzetu" ?

  Waingereza wanasema - picture speaks louder than words.

  Rais mkumbatia watoa rushwa(according to NEC-CCM).


  mwakale-1.jpg

  mwakale-2.jpg
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ya Mwakalebela ni ajali ya kisiasa tu.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Anatayarishiwa wilaya kuwa DC
   
 4. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo CCM inatuchanganya na kutuona hatuna akili kabisa.chenge ana tuhuma nzito kuhusu rada na madudu mengine lakini yupo kwenye kamati ya maadili ya chama.Mramba ana case mahakamani,aliyempeleka mahakamani anasimama na kumnadi.Naamini JK anajua makosa yao vizuri ila hana ujasiri wa kuwatema na naamini kuna njia nyingine anayotaka kutumia kuwatelekeza lakini kwa gharama za walipa kodi kwani kuna chaguzi ndogo zitakuja kwa uzembe wake.
  Nimesoma humu ndani ya kuwa Bashe nae ameteuliwa kuwa kampeni manager wa chaguo la Bi Mkubwa (WAMA), ni vituko.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu 255 kama ulikuwa kichwani kwangu, I was thinking on the same page!!!!!!!!!!! Yaani huyu JK busara ni sufuri kabisa!!!!!!!
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ana uchu mkubwa sana wa madaraka!!!!!!
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Halafu eti unategemea mahakama itakuwa huru kwenye kesi hiyo kwa mazingira kama haya. Damn! hapa ndiyo umuhimu wa debate unapokuja haya yalikuwa ni maswali ambayo angeulizwa tuusikie umakini wake. But this guy will be there in the records as the worst presdaa ever!!!!
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni pigo kubwa kwa Hoseah!!! Anangoja nini kujiuzulu? Lakini kwa kuwa naye ni kibaraka, sidhani kama analielewa vyema hili.
   
 9. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kiwango cha nchi yetu viongozi kutowajibika kwa wananchi ni cha kutisha, na sijui mwisho wake utakuwa lini.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimependa sana jinsi 255Texter ulivyoiweka mada hii ikiwa na ushahidi RED HANDED! Kuna haja ya ushahidi gani mwingine? Oktober 31 haiko mbali!

   
 11. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mwakalebela hapa amekumabtiwaje sasa? Kwani amerudishiwa tena nafasi ya ugombea? Au kule kukumbatiana wakati wa kusalimiana na kwenyewe hakutakiwi?
   
 12. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  He is desparate to win the election again.

  Kama anaona una umuhimu wowote katika yeye kushinda atakuhitaji hata kama wewe ni mla rushwa, mwizi, jambazi, au muuwaji.

  He is so desperate
   
 13. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani CCM ina double standards..kama we ni mtu wao kwa maana uko katika mtandao wa JK au mwanae au kuna kigogo wa ndani ya CCM anakulinda basi maamuzi yao juu yako ni tofauti na mwana CCM mwingine raia tuu alietokea kupendwa na wananchi bila kuwa na mtu wa kumlinda ndani ya CCM. Ndo maana kina Mramba,RA na EL wataendelea kupeta na wengine wakiangukia pua na kubaki kusubiri fadhila za u-DC!
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hata kama ningekuwa mimi ningemkumbatia. This is politics, kuwa na kesi mahakamani si kuwa ndo umekuwa ugomvi, hayo niyakawaida. well done.
   
 15. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Binafsi naona bora kidogo ya Mwakalebela, lakini kuwapitisha Lowassa, Chenge na Mramba halafu anaenda kupigia kampeni ni utani wa hali ya juu na kuonyesha kwamba serikali ya JK si makini na anafanya mchezo wa kuigiza na hayuko serious. anawaona watz kama vichanga.
  Mtu yeyote mwenye akili timamu wakiwemo wasaidizi wake including kitchen cabinet wanashangaa, mfano Mramba serilkali ya JK inamshitaki kwa rushwa halafu anaenda jukwaa anasema mchagueni huyo ndiye kiongozi safi anayefaa, simweli naona ni kama ametutukana watanzania kupita kiasi ni bora afute hizo kesi tujUe moja kuliko VIINI MACHO VYA NAMNA HII
   
 16. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  JK Ni Msanii Mnataka atoe Singo ngapi kama hizo ndo Muamini!:playball:
   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Chama Cha Mafisadi, Chama Cha Majambazi, Chama Cha Mabazazi, Chama Cha Mijitu... orodha iendelee!
   
 18. T

  Tanzania Senior Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo si CCM, Ni watanzania. Tusipoamua tukaenda vijijini na kuwaelemisha watanzania tutaendelea kuimba CCM inatuchanganya.
   
 19. M

  Mutu JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  this is real what happening now to mkwere
   
 20. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nafikiri yeye pia ni mtoa na mpokea rushwa, niyo maana anawakumbatia wenzake. Tofauti hapa ni kwamba yeye ndiye aliyeshika mpini hivyo kwa sasa hakuna wa kumchukulia hatua, labda akimaliza uongozi wake, utasikia mengi tu.
   
Loading...