Wazungu wengi leo ndio wanaoongoza katika kumwabudu Yesu Kristo kwa roho na kweli. Wahubiri mashuhuri duniani, pamoja na waimbaji maarufu wa nyimbo za injili, ni kutoka mataifa ya Magharibi. Hili linaonyesha jinsi Injili ilivyopokelewa kwa dhati katika jamii zao.
Mfano hai ni aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump. Pamoja na kuwa kiongozi wa taifa tajiri duniani, alimtambua Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Mara kadhaa ameonekana akiwa amepiga goti kumuomba Mungu kwa unyenyekevu mkubwa. Hili linaonesha kuwa hata katika nafasi za juu za mamlaka, Yesu Kristo anapewa heshima. Ukiichukua dola ya Marekani (dollar bill) ya thamani yoyote, utaona imeandikwa maneno haya: "In God We Trust". Taifa tajiri linatambua kuwa chanzo cha mafanikio yao ni Mungu.
Kwa hiyo ndugu yangu, usidanganyike. Yesu Kristo ndiye njia, kweli, na uzima. Ndiye Mkombozi wa wanadamu wote. Amegusa na kubadilisha maisha ya watu wengi sana duniani kutoka maisha ya dhambi na giza, hadi kuwa watu wa nuru, maadili, na matumaini. Ametuletea amani, upendo, msamaha, na uzima wa milele.
Kwa upande mwingine, dini nyingi za jadi za Kiafrika zimekosa vigezo muhimu vya kuonesha ufunuo wa Mungu wa kweli aliyeziumba mbingu na nchi. Ustaarabu wa Mbinguni unajengwa juu ya maadili kama amani, upendo, furaha, uvumilivu, ustahimilivu, na utakatifu. Lakini katika baadhi ya mila na tamaduni za kidini za Kiafrika, kuna mambo kama kurogana, visasi, na woga usio wa kiroho. Haya yote yanapingana na tabia ya Mungu wa kweli.
Yesu Kristo ndiye nuru ya ulimwengu. Kumfuata Yeye ni kuchagua maisha ya uzima wa sasa na wa milele.
View attachment 3324102
View attachment 3324114