Ushahidi Huu: Jinsi Bunge linavyotumia madaraka yake kuliibia Taifa via Tume ya Utumishi ya Bunge

Nyongeza ya posho ilikuwa ni mulungura ili mswada wa katiba upite chapuchapu!!
 
nataka kuwa mbunge nikapate posho wadau naombeni strategies, esp mzee mwanakijiji mchango wako ktk hizo jitihada zangu za kuwania ubunge ni muhimu sana, tehe tehee tehee afu nikifanikiwa nitawatoa wadau au sio
Nipeni kura zenyu banaa..
 
VGL usipingane na aliesema watanzania ni mabwege,maana kwa tukio kama hili subiri uone kama hatutaishia kujadiliana humu jkwaani na kesho ikiibuka hoja nyingine hii itakuwa imepata natural death na hakuna kitakachofuata,hebu jiulize hili la kugongana kauli kwa watendaji limeshafanyika mara ngapi na juzi Kashilah na Spika wamegongana kauli sasa nani mkweli kama Dr Kashililah kaundanganya umma wa watanzania anachukuliwa hatua gani,na kama mapendekezo hayo yalikuwa hayajatiwa mkono na JK nini kilifanyika na hatua gani zitachukuliwa? na hili la mifumo ya ulipananji ni kweli linashida lakini nani mwenye kulikemea na kulibadilisha au kufanyiwa marekebisho?wakati wenye kuisimamia serikali nao ndo hivyo tena,ndo maana naunga mkono hoja ya mchangiaji kuwa watanzania ni mabwege,maana tunaouwezo wa kuyarekebisha haya kwa kukataa,lakini humuhumu kuna watu kuna watu watapinga na vile nao ni sehemu ya ufisadi unaofanyika
 
Jamani mwenye nakala ya hii sheria ya 2008 naomba mnitumie. Nimeitafuta kila mahali without success.
 
Madiwani nao wataka posho yao iongezwe toka sh 120 000 kwa mwezi wanayolipwa sasa ukizingatia wao wanafanya kazi kuliko wabunge
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Wabunge ya 1997 (siina uhakika kama imewahi kufanyiwa marekebisho)

Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge: (WAJUMBE WOTE NI WABUNGE)

(a) the Speaker, who shall be the Chairman,
(b) the Deputy Speaker, who shall be the Vice- Chairman;
(c) The Minister responsible for Parliamentary Affairs;
(d) five other members appointed by the National Assembly from amongst its Members.
(3) The Clerk shall be the Secretary of the Commission and shall be responsible for securing or facilitating the implementation of
all the decisions of the Commission

Wafanyakazi wengine wa Tume mishahara yao na marupurupu yao yanatakiwa yaendane na yale ya Tume ya Utumishi wa Umma - ukiondoa Katibu wa Tume

Ibara ya 7:

(2) In the performance of its
functions under this section, the Commission shall
ensure that the complementing, grading and pay of
staff in the Service are kept broadly in line with
those in the Civil Service, and that so far as
consistent with the requirements set by the
National Assembly, the other conditions of staff in
the Service are also kept broadly in line with those
in the Civil Service.
(3) The Commission shall ensure that,
the pensions and other similar terminal benefits of
staff in the service are kept in line with the
provisions of the main pension scheme of the Civil
Service, but shall not do so in the case of staff for
whom provision for such benefits was made under
another statutory scheme before they entered
service in the National Assembly.

Maamuzi yao yanaamuliwa na Bunge (mapendezo toka kwa wabunge yanaulizwa wabunge wote!) na wakipitisha fedha ni lazima zilipwe mara moja kwenye mfuko wa Bunge

Ibara ya 11: The moneys required from time to time for the purposes of this Act shall, when the estimates have
been approved by Parliament, be paid by the Treasury from the Consolidated Fund into the National Assembly Fund.

Ibara ya 12: Tume inaweza kubadilisha mapendekezo ya makadiridio yatakayoletwa na Katibu wa Bunge

Mgogoro na Ibara ya 13?

The Commission shall from time to time, Prepare and recommend to the President the rates of salaries, allowances and other remuneration to be paid to Members of Parliament.

Swali kuhusu Ibara ya 11, 12 na ile ya 13? Je Rais anahitaji kuridhia ongezo la mishahara ya wabunge kwa mujibu wa sheria? Napendekeza kwamba (kwa maoni yangu) RAis anapewa taarifa tu; sheria haimtaki kuridhia kwani uamuzi wa mwisho wa makadirio na maamuzi ya kulipa wabunge yanafanywa na Tume hiyo. Sheria haimtaki rais kuridhia mapendekezo hayo au chombo kingine chochote. Tunaweza kujadiliana juu ya use ya neno "recommend" but in light of Article 11 Spika Makinda yuko sahihi.

Kulinganisha na TUme nyingine za Utumishi?

NImejaribu kulinganisha japo kwa haraka haraka na tume nyingine za utumishi ili kuona kama kinachofanywa na Wabunge kinafanywa na tume hizo nyingine (walitungiwa sheria na Bunge!). Je, tume ya utumishi ya Walimu au ya Mahakama na hata tume ya Utumishi wa Umma ziko huru kama tume ya Utumishi wa Bunge kufanya wapendavyo kuhusu fedha za Watanzania? Where did we go wrong?

Mzee Mwanakijiji, taratibu za matumizi ya fedha za umma kwa mujibu wa katiba ni hizi

MFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHA
ZA JAMHURI YA MUUNGANO
Mfuko Mkuu wa
Hazina ya
Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib.
135.-(1) Fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbali
kwa ajili ya matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
isipokuwa fedha za aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya
ibara hii, zitawekwa katika mfuko mmoja maalum ambao utaitwa
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
(2) Fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na Sheria
kwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe katika
mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum.
Masharti ya
kutoa fedha za
matumizi kutoka
mfuko
Mkuu wa Hazina
ya Serikali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
136.-(1) Fedha hazitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina
ya Serikali kwa ajili ya matumizi ila kwa mujibu wa masharti
yafuatayo:-
(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo
yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iwe
imetolewa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote;
(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo
yameidhinishwa ama na sheria ya Matumizi ya
Serikali iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheria
iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 140
ya Katiba hii.
(2) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa serikali,
ukiachilia mbali Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, hazitatolewa
kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi
hayo yawe yameidhinishwa na sheria.
(3) Fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali
hazitatolewa kutoka Mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka
matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali na pia kwa sharti kwamba fedha
hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajili
hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
98
Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya
fedha zilizomo
katika Mfuko
Mkuu wa Hazina
ya Serikali Sheria
ya 1984 Na.15
ib.43
137.-(1) Rais atatoa maagizo kwa watu wanaohusika
kwamba watengeneze na kuwasilisha kwenye Bunge katika kila
mwaka wa fedha wa Serikali, makadirio ya mapato na matumizi
ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kipindi cha
mwaka wa fedha unaofuata.
(2) Baada ya Bunge kuyakubali makadirio ya matumizi
(mbali na matumizi ambayo yameidhinishwa ama na Katiba hii
au sheria nyingine yoyote kuwa yatokane na fedha zilizomo
katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali) kutawasilishwa
kwenye Bunge Muswada ambao utaitwa Muswada wa Sheria ya
Matumizi ya fedha za Serikali, kwa ajili ya kuidhinisha matumizi
ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, na fedha
hizo zitatolewa kulipa gharama za shughuli mbalimbali za
Serikali zinazohusika na makadirio hayo.
(3) Ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekana
kwamba:
Fedha za matumizi zilizoidhinishwa na sheria ya
matumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya shughuli fulani
hazitoshi au kwamba imekuwa lazima kulipa gharama za
shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu
wa sheria; au
Kuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli
fulani kwa kiasi kinachozidi kiwango cha matumizi
yaliyoidhinishwa na sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali
kuhusu shughuli hiyo au kwamba fedha zimetumiwa kulipia
gharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi
kwa mujibu wa Sheria, kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio
ya matumizi ya nyongeza au, kadri itakavyokuwa, maelezo ya
matumizi ya ziada, na baada ya Bunge kuyakubali hayo
Makadirio ya matumizi ya nyongeza au maelezo ya matumizi ya
ziada, kutawasilishwa kwenye Bunge Muswada wa Sheria ya
Matumizi ya fedha za Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi
ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na fedha
hizo zitatumiwa kulipia gharama za shughuli zinazohusika na
hayo makadirio au maelezo.

JEE MATUMIZI HAYO YA POSHO, YALIFUATA UTARATIBU HUU?. Kama sivyo ni ukiukwaji wa katiba, wahusika wakuu lazima waende na maji!.

Ili fredha za umma zitumike, ni lazima CAG aidhinishe kama inavyoelezwa hapa!

Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za
Serikali wa
Jamhuri ya
Muungano
Sheria za 1979
Na.14 ib.11
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
143.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na
jukumu juu ya mambo yafuatayo:
(a) kuhakikisha kwamba fedha zozote
zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa
na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 136 ya Katiba hii, na iwapo atatosheka
kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo,
basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;
(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi
yake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo
katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au fedha
ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, na ambazo zimetumika,
zimetumiwa kwa ajili ya shughuli zilizo husika na
matumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayo
yamefanywa kwa kufuata

nimezungumza na CAG, hajaidhinisha matumizi hayo!.

Pasco
 
.............
nimezungumza na CAG, hajaidhinisha matumizi hayo!.

Pasco

CAG tena aidhinishe!!! . Ebu fafanua pascal. Mi nilidhani CAG ni mtu anayekuja baada ya matukio kumbe anatakiwa kudihinisha ?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu ibara ya 13 haina mgogoro hata kidogo..The Commission shall from time to time, Prepare and recommend to the President the rates of salaries, allowances and other remuneration to be paid to Members of Parliament.

Mimi sielewi mnavyopitisha matumizi ya fedha lakini mara zote vikao hupitisha matumizi na yanapokwenda kwa mkuuu wa kaya anaweza kutumia veto yake kupinga matumizi hayo na ndio maana wametumia neno recommend to.. Kupita kwa jambo lolote haina maana hazina amabyo iko chini yake watoe hela kwa sababu bunge limepitisha..Hata muswada wa sheria umepitishwa na baraza na hata bunge zima lakini bado mkuu wa kaya ndiye mwamuzi wa mwisho.

Mara nyingi mkuu wa kaya huwa kisha jua kinaendelea nini bungeni. Kama Bunge linajichukulia jukumu la kuweka viwango vyake na hakuna final say hapa mkuu wangu tutakuwa tunafanya madudu matupu. Just imagine kama JK asingelikwamisha hili ndio ilikuwa inatoka hivyo na yeye aseme nini? Ati ahusiki akitegemea wananchi mtamuelewa!

Sema tu kwamba mfumo wa Utawala wetu ni mbaya sana tunatakiwa kuwa na rais ambaye ni ceremonial tu, mambo yote waziri mkuu ambaye huenda Bungeni. kazi kubwa ya rais ni kuitisha Uchaguzi, kuapisha na kumkabidhi Waziri mkuu wadhifa huo. Maadam huyu hana mahusiano na chama na pekee ndiye mwenye uwezo wa kumsimaisha Waziri mkuu ama kusikiliza malalamiko ya upande wowote hata kama ni minority anaweza kuitisha uchaguzi mpya. Waziri mkuu anakuwa hana power juu yake Kiutawala..
 
JEE MATUMIZI HAYO YA POSHO, YALIFUATA UTARATIBU HUU? Kama sivyo ni ukiukwaji wa katiba, wahusika wakuu lazima waende na maji!.

Mkuu Pasco,

Nina ambaye atawapeleka na maji? Huyu JK ambaye mpaka leo bado hajasema kitu kuhusu Jairo na wenzake waliokutwa na makosa kwenye sakata la Jairo?

Bunge lilimchunguza Jairo alipotuhumiwa kukusanya hela nje ya utaratibu unaotakiwa. Je, kwenye hili sakata ni nani ambaye anatakiwa kulichunguza Bunge? If found guilty, mwenye makosa ni nani? Nani mwenye final say kati ya Spika wa Bunge na Katibu wa Bunge when it comes kwenye maswala ya matumizi ya fedha?
 
CAG tena aidhinishe!!! . Ebu fafanua pascal. Mi nilidhani CAG ni mtu anayekuja baada ya matukio kumbe anatakiwa kudihinisha ?

Mkuu Mtazamaji,

Kwa uelewa wangu ni kwamba baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa fedha, nakala ya bajeti hiyo hupelekwa kwa CAG kwa ajili ya udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha za seerikali, kwamba matumizi ya fedha za serikali yatakuwa kama ilivyoainishwa kwenye bajeti iliyopitishwa na bunge. Pia matumizi ya fedha hizo yatafuata taratibu zinazohusika katika matumizi yake.

So, kwenye hii issue, ule waraka ambao JK anatakiwa kuiandikia ofisi ya Bunge kuridhia kwamba amekubaliana na ombi la nyongeza ya posho, lazima uende kwa CAG, siyo kwa ajili ya approval, bali kwa ajili ya ukaguzi hapo baadaye pindi timu ya CAG itakapokwenda kukagua hesabu za Bunge. Huo waraka lazima uwe na tarehe ili kuonyesha kwamba nyongeza imeanza kutumika lini na kama ilianza kabla ya tarehe ya kuandikwa waraka huo, then waraka lazima useme wazi kwamba nyongeza hii imeanza kutumika tangu tarehe fulani.

Kwa hiyo CAG huwa hafanyi approval (idhinisha), bali hupelekewa kwa ajili ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali. Bajeti ikishapitishwa na Bunge hakuna anayeweza kuisimamisha.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Wabunge ya 1997 (siina uhakika kama imewahi kufanyiwa marekebisho)

Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge: (WAJUMBE WOTE NI WABUNGE)

(a) the Speaker, who shall be the Chairman,
(b) the Deputy Speaker, who shall be the Vice- Chairman;
(c) The Minister responsible for Parliamentary Affairs;
(d) five other members appointed by the National Assembly from amongst its Members.
(3) The Clerk shall be the Secretary of the Commission and shall be responsible for securing or facilitating the implementation of
all the decisions of the Commission

Wafanyakazi wengine wa Tume mishahara yao na marupurupu yao yanatakiwa yaendane na yale ya Tume ya Utumishi wa Umma - ukiondoa Katibu wa Tume

Ibara ya 7:

(2) In the performance of its
functions under this section, the Commission shall
ensure that the complementing, grading and pay of
staff in the Service are kept broadly in line with
those in the Civil Service, and that so far as
consistent with the requirements set by the
National Assembly, the other conditions of staff in
the Service are also kept broadly in line with those
in the Civil Service.
(3) The Commission shall ensure that,
the pensions and other similar terminal benefits of
staff in the service are kept in line with the
provisions of the main pension scheme of the Civil
Service, but shall not do so in the case of staff for
whom provision for such benefits was made under
another statutory scheme before they entered
service in the National Assembly.

Maamuzi yao yanaamuliwa na Bunge (mapendezo toka kwa wabunge yanaulizwa wabunge wote!) na wakipitisha fedha ni lazima zilipwe mara moja kwenye mfuko wa Bunge

Ibara ya 11: The moneys required from time to time for the purposes of this Act shall, when the estimates have
been approved by Parliament, be paid by the Treasury from the Consolidated Fund into the National Assembly Fund.

Ibara ya 12: Tume inaweza kubadilisha mapendekezo ya makadiridio yatakayoletwa na Katibu wa Bunge

Mgogoro na Ibara ya 13?

The Commission shall from time to time, Prepare and recommend to the President the rates of salaries, allowances and other remuneration to be paid to Members of Parliament.

Swali kuhusu Ibara ya 11, 12 na ile ya 13? Je Rais anahitaji kuridhia ongezo la mishahara ya wabunge kwa mujibu wa sheria? Napendekeza kwamba (kwa maoni yangu) RAis anapewa taarifa tu; sheria haimtaki kuridhia kwani uamuzi wa mwisho wa makadirio na maamuzi ya kulipa wabunge yanafanywa na Tume hiyo. Sheria haimtaki rais kuridhia mapendekezo hayo au chombo kingine chochote. Tunaweza kujadiliana juu ya use ya neno "recommend" but in light of Article 11 Spika Makinda yuko sahihi.

Kulinganisha na TUme nyingine za Utumishi?

NImejaribu kulinganisha japo kwa haraka haraka na tume nyingine za utumishi ili kuona kama kinachofanywa na Wabunge kinafanywa na tume hizo nyingine (walitungiwa sheria na Bunge!). Je, tume ya utumishi ya Walimu au ya Mahakama na hata tume ya Utumishi wa Umma ziko huru kama tume ya Utumishi wa Bunge kufanya wapendavyo kuhusu fedha za Watanzania? Where did we go wrong?

Mwanakijiji, unachozungumza ni sahihi. Lakini sina hakika kuwa kuna tofauti kati ya Rais na Bunge, kama sijakosea rais ni sehemu ya bunge, na yeye ndiye mwenye madaraka juu ya bunge anaweza kulivunja kama anavyopenda na kupitisha miswada na sheria zinazoamuliwa na bunge. [achana na ujinga kuhusu separation of powers tunajua kabisa kuwa ipo kwenye makaratasi haipo kivitendo]. Sina hakika kama rais pia anapokea mshahara wa wabunge, lakini kuna uwezekano kuwa ana haki hiyo, kwa hiyo yeye pia ana interest.

Tunatakiwa kujiuliza maswali mengi tu kuhusu bunge. nani anatunga sheria na taratibu za kulidhibiti bunge? huyu anayezitunga ana interest gani na ubunge, wabunge ba bunge. Ukiangalia unaweza kuona kuwa zimetungwa na mtu mmoja kwa interests za chama kimoja. Hii ni moja ya tatizo kubwa tulilo nalo ambalo tunalikalia kimya.
 
Mwanakijiji

Sheria imefanyiwa marekebisho, na inaonyesha kwamba sheria hiyo uliyoinukuu ilishafutwa na kuandikwa upya. Fanya rejea kwa kutumia The National Assembly (Administration) Act ya mwaka 2008.

Hii ndio niliyoitumia katika: JOHN MNYIKA: Msimamo wangu juu ya suala zima la Posho!

Ukirejea sheria husika na maoni yangu utaona kwamba wote wawili Spika na Katibu wa Bunge wamefanya makosa; pamoja na mapendekezo ya tume ya utumishi wa ubunge; wabunge hawana mamlaka ya kujipangia posho zao. Wala hakuna siku wabunge tulikaa kwa umoja wetu na 'kujipandishia' posho. Posho hizi zimeongezwa kinyemela na kikundi kidogo cha watu katika uongozi wa Bunge, walipobaini kwamba wamekiuka sheria wakaacha kuendelea kuzilipa. Ukiondoa habari za magazetini kuwa posho hizo zimeingizwa kwenye akaunti za wabunge kwa siku tatu tu, binafsi nafuatilia kupata taarifa rasmi za kibunge kujua zimeingizwa lini, siku, ngapi, kiasi gani na kwa sababu gani. Hatimaye tutafanya maamuzi ya hatua za ziada za kuchukua juu ya jambo hili.

JJ

Heshima kwako na jana kama ulivyokuwa na Dkt Lwaikama nadhani ni wakati muhimu wa kuwa chombo huru cha kuratibu maslahi ya watumishi wa umma.
 
Ni swala ambalo lipo wazi sana kwamba inavyoonekana Spika wa Bunge ndiye aliyepitisha hii issue ya kuongeza posho kivyake kwa sababu wangekuwa wote basi Dr. Kashililah asingeliweza kuja front na kupinga kuwa posho hazijaongezwa wakati zimeongezwa. Hii inadhihirsha wazi kuwa kulikuwa na mgongano wa kimaslahi na utendaji kati ya vigogo hawa na kutaka kuoneshana ubabe wa madaraka yao ndo maana fedha ikawekwa kimya kimya na kwa siri na mmoja anakanusha leo kesho yake mwingine aliyeidhinisha kwa minajiri yake binafsi anathibisha kuwa ni kweli fedha za posho za vikao zimeongezwa.

Shida iliyopo katika uongozi wa nchi hii ni kuongoza kwa usemi wa bora liende pasipo kuzingatia sheria zinazotoa mwongozo wa madaraka na majukumu husika kwa kila kiongozi.
 
Mzee Mwanakijiji!
Katika hali Kama hii Bunge haliwezi kuwa na maslahi ya dhati ya kufanya mchakato wa Katiba Mpya
Ukichunguza kila kitu kimakaa hovyo. Narudia mpaka Watz watakapoamua kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu ya umma peoples power ndipo tutapata ukombozi wa kweli. Kuchambua tukio moja moja haitutoi hapa tulipo tunatakiwa ujasiri always take the bull at the horns vinginevyo imekula kwetu.
 
Back
Top Bottom