Ushahidi Huu: Jinsi Bunge linavyotumia madaraka yake kuliibia Taifa via Tume ya Utumishi ya Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushahidi Huu: Jinsi Bunge linavyotumia madaraka yake kuliibia Taifa via Tume ya Utumishi ya Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 13, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Wabunge ya 1997 (siina uhakika kama imewahi kufanyiwa marekebisho)

  Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge: (WAJUMBE WOTE NI WABUNGE)

  (a) the Speaker, who shall be the Chairman,
  (b) the Deputy Speaker, who shall be the Vice- Chairman;
  (c) The Minister responsible for Parliamentary Affairs;
  (d) five other members appointed by the National Assembly from amongst its Members.
  (3) The Clerk shall be the Secretary of the Commission and shall be responsible for securing or facilitating the implementation of
  all the decisions of the Commission

  Wafanyakazi wengine wa Tume mishahara yao na marupurupu yao yanatakiwa yaendane na yale ya Tume ya Utumishi wa Umma - ukiondoa Katibu wa Tume

  Ibara ya 7:

  (2) In the performance of its
  functions under this section, the Commission shall
  ensure that the complementing, grading and pay of
  staff in the Service are kept broadly in line with
  those in the Civil Service, and that so far as
  consistent with the requirements set by the
  National Assembly, the other conditions of staff in
  the Service are also kept broadly in line with those
  in the Civil Service.
  (3) The Commission shall ensure that,
  the pensions and other similar terminal benefits of
  staff in the service are kept in line with the
  provisions of the main pension scheme of the Civil
  Service, but shall not do so in the case of staff for
  whom provision for such benefits was made under
  another statutory scheme before they entered
  service in the National Assembly.


  Maamuzi yao yanaamuliwa na Bunge (mapendezo toka kwa wabunge yanaulizwa wabunge wote!) na wakipitisha fedha ni lazima zilipwe mara moja kwenye mfuko wa Bunge

  Ibara ya 11: The moneys required from time to time for the purposes of this Act shall, when the estimates have
  been approved by Parliament, be paid by the Treasury from the Consolidated Fund into the National Assembly Fund.


  Ibara ya 12: Tume inaweza kubadilisha mapendekezo ya makadiridio yatakayoletwa na Katibu wa Bunge  Mgogoro na Ibara ya 13?


  The Commission shall from time to time, Prepare and recommend to the President the rates of salaries, allowances and other remuneration to be paid to Members of Parliament.

  Swali kuhusu Ibara ya 11, 12 na ile ya 13? Je Rais anahitaji kuridhia ongezo la mishahara ya wabunge kwa mujibu wa sheria? Napendekeza kwamba (kwa maoni yangu) RAis anapewa taarifa tu; sheria haimtaki kuridhia kwani uamuzi wa mwisho wa makadirio na maamuzi ya kulipa wabunge yanafanywa na Tume hiyo. Sheria haimtaki rais kuridhia mapendekezo hayo au chombo kingine chochote. Tunaweza kujadiliana juu ya use ya neno "recommend" but in light of Article 11 Spika Makinda yuko sahihi.


  Kulinganisha na TUme nyingine za Utumishi?

  NImejaribu kulinganisha japo kwa haraka haraka na tume nyingine za utumishi ili kuona kama kinachofanywa na Wabunge kinafanywa na tume hizo nyingine (walitungiwa sheria na Bunge!). Je, tume ya utumishi ya Walimu au ya Mahakama na hata tume ya Utumishi wa Umma ziko huru kama tume ya Utumishi wa Bunge kufanya wapendavyo kuhusu fedha za Watanzania? Where did we go wrong?
   
 2. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Phrase "recommend" obligates none to bunge to accept what the pres. may have said about demands of bunge,thus bunge ni wezi.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Unapendekeza nini?
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani raisi anahitajika kuridhia ongezeko la mishahara ya wabunge kwa mujibu wa sheria. Vinginevyo hakungekuwa na hiyo ibara ya 13.
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni pale tulipolitosa azimio la Arusha. Kabla, mbunge alitumia gari la serikali, dereva wa serikali, na hata alipobadilishiwa gari, lile la zamani liliendelea kutumiwa na idara zingine za serikali. Upuuzi wote huu wa mikopo ya magari, posho ya mafuta, posho ya vikao nk ni mazao ya utawala wa Mwinyi.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  In theory it looks ok but the horror emerges when you put faces:

  (a) the Speaker, who shall be the Chairman, - Anna Makinda
  (b) the Deputy Speaker, who shall be the Vice- Chairman; - John Ndugai
  (c) The Minister responsible for Parliamentary Affairs; - Lukuvi
  (d) five other members appointed by the National Assembly from amongst its Members. - ?
  (3) The Clerk shall be the Secretary of the Commission.... Dr Kashilila

  Ukiwa na mfumo madhaifu ya watu sio shida sana, na ndio maana ni muhimu kabisa kuwa na sheria itakayo deal na mapungufu ya kiungozi.
   
 7. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji

  Sheria imefanyiwa marekebisho, na inaonyesha kwamba sheria hiyo uliyoinukuu ilishafutwa na kuandikwa upya. Fanya rejea kwa kutumia The National Assembly (Administration) Act ya mwaka 2008.

  Hii ndio niliyoitumia katika: JOHN MNYIKA: Msimamo wangu juu ya suala zima la Posho!

  Ukirejea sheria husika na maoni yangu utaona kwamba wote wawili Spika na Katibu wa Bunge wamefanya makosa; pamoja na mapendekezo ya tume ya utumishi wa ubunge; wabunge hawana mamlaka ya kujipangia posho zao. Wala hakuna siku wabunge tulikaa kwa umoja wetu na 'kujipandishia' posho. Posho hizi zimeongezwa kinyemela na kikundi kidogo cha watu katika uongozi wa Bunge, walipobaini kwamba wamekiuka sheria wakaacha kuendelea kuzilipa. Ukiondoa habari za magazetini kuwa posho hizo zimeingizwa kwenye akaunti za wabunge kwa siku tatu tu, binafsi nafuatilia kupata taarifa rasmi za kibunge kujua zimeingizwa lini, siku, ngapi, kiasi gani na kwa sababu gani. Hatimaye tutafanya maamuzi ya hatua za ziada za kuchukua juu ya jambo hili.

  JJ
   
 8. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo bunge lina uwezo hata wa kudharau bajeti ya Taifa mwaka wa fedha? Ina maana kwao ongezeko zaidi ya wao wenyewe kukubaliana hakuna vigezo au scrutiny nyingine

  Kama bunge linakuwa mfano wa kupachika expenditure za ziada mwezi November litasimamijaje na kukemea serikali kutokuheshimu au kutofuata bajeti.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Na kikwete huyu wa maisha bora sasa kazidisha mara dufu..........na kikwete hii ni janja yake ili wabunge wasiendelee lumuumbua kwa ufisadi wake anaofanya yeye binafsi, mke wake kupitia taaisis feki, na watoto wake kupitia majengo elfu wanayomiliki tofauti na vipato vyao au vya baba yao....................

  Walibya wangekuwa ndiyo watz sijui wangefanyeje na viomgozi wao.........ndio maana ghadafi hawakutaka hata afike mbele ya sheria kwani wanajua sheria zipo tu na pengine zingezeza kupindishwa.......hapa kwetu pamoja na madudu na upumbavu wote huu wa rais na watendaji anaowateua bado tunacheka nae na tunamwacha achekecheke hovyo.............
  Twendeni wote barabarani kesho km nyie wajanja na mnaamini kweli mnaibiwa............."tz viongozi wahuni lakini wananchi ni mabweghe na mtu km kikwete anatumia san ubweghe wa watz kufanya atakavyo..............
  1.anagawa tuzo kwa wasiostahili na kwa maslahi yake binafsi ili hoja nzito dhidfi yake na serikali yake zisiruhusiwe na anna makinda (rushwa ya nishani)....
  2. Anasamehe mafisadi kila siku huku akipeleka mahakamani mafisadi bila kuwa na ushahidi ili wasikamatwe.......
  3. Anawachochea watz kwa itikadi za kidini.kikwete mdini hatari sana na kuna moto wa kidini ataulipua akikaribia mwishoni mwa ngwe yake hii ..............
  4. Kikwete fisadi namba moja kwa mujibu wa lowasa na hosea kule weak leaks
  5.hataki kuwahukulia hatua wateule wake pamoja na makosa ya wazi mbele ya jamii................sijui kikwete afanye nini aili asihukumiwe na watz hapo baadaye
  6. Anaikana waziwazi falsafa yake ya maisha bora kwa kila mtz...(hili ni tusi jingine kwa watz)


  "twendeni barabarani sasa au km vipi tuwaite walibya wenye maisha magumu watusaidie kuwaongoa wabunge wa ccm wabinafsi hawa na spika uchwara na rais dhaifu na goigoi kikwete"

   
 10. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Pure patriotism. Tunahitaji wabunge wa aina yako ili kuiondoa nchi hii mikononi mwa utumwa wa Pharoah (CCM)
   
 11. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Sasa mkuu,hapo wamaanisha kunawaliyopata au ambao awakuingiziwa posho,Je mh.we umeingiziwa sh.ngapi.?
   
 12. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nilimsikia mama Ananiel Nkya siku moja akielezea logic ya "Mlinzi kupanga na mwizi kuja kumuibia mwenye mali alafu mwenye mali akashistuka"
  Kweli kuna haja ya kusimama kwanza na kuangalia tutokako then kujiuliza hili swali lako Mzee Mwanakijiji:
  Where did we go wrong?

  Kuendelea kwenda mbele ni makosa makubwa maana tunaendelea kopotea
   
 13. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  JK inaonekana aliahidi maisha bora kwa wabunge tu na kwa kweli kafanikiwa, hawa wabunge wengi wanafiki tu wanajifanya wanapinga ongezeko la posho wakati zinawatamkia bora ya Shibuda yeye sio mnafiki. Siku moja nilimsikia Makinda anaongea via Capital radio eti wabunge wengi wapya wanajuta kuingia mjengoni coz maslahi ni duni yule mama ni msengenyaji yaani 200,000 kwa siku nikidogo? wakati huo ni mshahara wa mtu ambao kaufanyia kazi siku 30. Kwa hiyo maisha ni magumu dodoma tu na ni kwa wabunge tu?
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Miaka hamsini ya uhuru uliopitiliza hata kutukanana wenyewe kwa wenyewe ukiachilia mbali kumtukana Rais na watendaji wake. "Watanzania ni mabwege". Hapa unamaanisha akiwemo Baba yako, Mama yako, Dada zako na ukoo wako mzima. Watake radhi hao ndugu zako wasije wakakulaani, sisi wengine tumepokea kama lilivyo.
   
 15. d

  dada jane JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 16. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mnyika ina maana wewe hujaingiziwa hata centi? Antalya bank statement yako iwe online au kwenye hard copy na ujibi maswali unayojiuliza hapo juu!!
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mfumo mzima wa mishahara, posho mbalimbali na mafao ndani ya mihimili yote mitatu ni ya kuangalia upya. Nahisi Wabunge wanaonewa sana katika hili. Hakuna anayefahamu Majaji wanalipanaje mishahara, posho na mafao wakistaafu. Vivyo hivyo kwenye muhimili wa DOLA ambako kuna majeshi yetu ya ulinzi na usalama, kuna wanasiasa, kuna watendaji wakuu serikalini, watumishi waandamizi, mashirika na taasisi za UMMA.
  Sasa hivi akili na mawazo yetu tumeeelekeza mno kwa wabunge. Kwa nini? Hebu mtu ajaribu kutuwekea hapa anavyolipwa Jenerali wa Jeshi, Kamishna wa Polisi, CEO wa NHC, EWURA, TPDC,..., Jaji wa Mahakama ya Rufaa, mahakama kuu, AG, DPP, CAG, Gavana wa BOT,... Tunawaonea WAbunge. Wateule wa mtu mmoja tu anayeitwa Rais ni balaa. Na hapohapo ufisadi unaendelea kama kawa!
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,636
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana nasemaga hapa tulipofika bora kiwake tu, huu ushakuwa upuuzi sasa, ina maana ugumu wa maisha ni kwa wabunge tu, watu wa kada zingine tumekuwa mawe? Kama noma na iwe noma.
   
 19. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, salute!
  Unaweza usiamini ila leo nimeamka na mawazo juu ya Bunge letu tukufu. Nimejiuliza maswali ambayo mengine yametajwa ktk thread nyingine kuhusu Ombwe...
  Asante kwa kuleta hoja hii. Nimetafakari sana juu ya kinachoendelea ktk Bunge letu tukufu hasa baada ya Tume kusema wanasubiri maamuzi ya Rais.
  Nimejiuliza yafuatayo;
  1. Kwa kauli ya Kashililah kuwa hela hazijaanza kulipwa ina maana katudanganya watanzania mchana kweupe au niaje?
  2. Ina maana akiitisha hiyo press conference hakuwasiliana na Madam Speaker?
  3. Nini kilitokea kati yake na Spika) baada ya yeye kuitisha press conference hiyo ambayo Spika alitofautiana nayo (vurumai au mpango wa kusawazisha)
  4. Ni nani anamuwajibisha Katibu kwa kusema 'uongo' kwa mujibu wa Spika... Huyu alisema posho hazijapanda huyu akasema zimepanda
  5. Hii Tume ndiyo inasimamiwa na Spika km Mwenyekiti. Tume hii imesema inasubiri maamuzi ya Rais. Spika huyuhuyu alisema posho zomepanda, Spika huyu huyu anasema wanasubiri maamuzi ya Rais...inakuwaje hapo? Ina maana rahisi kuwa alikurupuka na kama posho zimetolewa na kwa kuzingatia msisitizo alioutoa juu ya posho - with or without President accent, then that's serious abuse of power...
  6. Kama haikutosha, Nape akatoa kauli ( ambayo naamini ndiyo msimamo wa Chama) unaokinzana na wa Spika wa Nchi. Kauli ya Nape inamkataza Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama kutia sahihi mapendekezo hayo. Nitashangaa yakitiwa sahihi.

  Mhe Rais nasikia unapitaga huku JF. Usiishie tu kutia au kutotia saini. Maswali haya pamoja na mengine yanashangaza na yanatia wananchi hasira sana. Do you have to keep silent up to now? When is this saga going to end?

  Alilofanya Kashililah lina tofauti gani na la Jairo la kuidhinisha malipo yasiyo na msingi? Heri kwa Jairo kulikuwa na inflation ya prices, forging...ila kwa Kashililah kuna kulipa fedha kwa matumizi yasiyo halali, ya haramu kwa maana nyingine. This is a serious offence in public office.
  Au ndo itaundwa tume ya Bunge kufanya uchunguzi? Hiyo tume itaundwa na nani? Tutamuaminije Utouh kuchunguza jambo hili?
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mnyika asante; ngoja niipitie hii (maana nilikuwa na wasiwasi na sheria zote ziliandikwa chini ya Mkapa especially kati ya 1995 na 2000). Natumaini hii ya sasa itakuwa imebadilishwa hivyo.
   
Loading...