ushabiki huu wa ligi ya uingereza ni too much sasa.hatari....

yaani kweli naitaji matibabu maalum kumbe ndo maana nilivotoa thread ya kutafuta rafiki nikasema lazima awe arsenal fan sijapata mtu eeh?
Nadhani rejao anafaaa kuwa rafiki yako kuanzia leo kwasababu naye ni gunners///
Hongereni sana mungu awabariki nakipigo hadi mwisho wa urafiki wenu.....teteheeee teheheeeeee.
Man.u bana tabia yao sio nzuri kabisaaaa.
 
Boss thanks una bonge la hoja hapa. Watu hawali wala kunywa kwa vile wazungu wamefungana hahaha wakati hii ya kwetu hata ushauri hatutoi watu wanasishia kuamini ndumba ili mpira ukuwe
 
Boss thanks una bonge la hoja hapa. Watu hawali wala kunywa kwa vile wazungu wamefungana hahaha wakati hii ya kwetu hata ushauri hatutoi watu wanasishia kuamini ndumba ili mpira ukuwe

umeona ehh?
 
Nafahamu kuna watu wengi wana wehu wa mpira na ushabiki hauna logic

but mimi mwenzenu naona tulipofika kama watanzania au waafrika ni too much

tena ni hatari mno....LIGI YA UINGEREZA hii jamani.......siyo ya kwetu....

unakutana na houseboy ambae hata shule yamsingi hakumaliza
wala aikoneshwa ramani ya dunia akuoneshe england ilipo hawezi...but yuko so sad
kwa sababu arsenal imefungwa.....wamama wauza sokoni wanazungumzia manchester united..

watu hawajawahi hata kufika uwanja wa taifa but wanajua timu yote ya chelsea na wake wa wachezaji wa chelsea..

yaani unakuta mkeo,mama yako mzazi,ndugu zako,rafiki zako,ofisini
mitaani......wanazungumza mechi ya jana mpira......

mbona zamani hatukuwa hivyoo??????

hivi hili halina hasara ya aina yoyote ile kwetu?????????

mimi naona sasa ni too much...
mpaka vijijini watu wanasikitika kufungwa kwa arsenal?

ikwiriri na tandahimba??????/jamaniii

Labda nikuulize wewe ni dini gani na kama umewahi kuwaona waanzilishi wa hizo dini au zilipoanzia???? Hili ni suala la nafsi na moyo wa mtu haijalishi ni ya Tanzania au UK, hata dini zetu hazijaanzia Tanzania, ila tunaamini, likewise na mpira, tunaona kwenye TV tunazipenda.
 
Boss hoja yako ni nzuri lakini kuna makandokando mengi sana yanatusonga....

Kwanza soka la ulaya unaliona kiurahisi na kulisikiliza kiurahisi kwa sababu linatangazwa sana, unawasikia sana akina Suarez kwa siku kuliko hawa akina Ngasa. Hasheem Thabeet anacheza kikapu marekani na ni mtanzania lakini vyombo vya habari vya bongo vinakaa hadi miezi 6 bila kuwa na habari yake hata moja. Kila siku vichwa vya habari ni Arsenal na manchester kwa kuwa ndio zinauza magazeti yao na tv + radio zinasikilizwa sana.
Leo hii mimi shabiki wa Yanga nikitaka kuvaa jezi ya timu yangu hakuna duka hata moja ambalo nikenda nikasema niuzieni official jezi ya yanga nitapata, licha ya potential kubwa ya clubs kutajirika kwa kujitangaza na kuuza bidhaa zao. Viongozi wa clubs za mpira ni kama wanasiasa. Kiongozi wa TFF hajui hata utamaduni wa timu ya yanga anang'ang'ania wavae nyekundu ambayo kimsingi kila shabiki wa simba atachukizwa na wana yanga kuvaa nyekundu, na utamaduni huu tumeuona toka utotoni. Wakati wa kombe la kagame hadi watangazaji wa super sport walishangaa kuona kuwa Tanzania kun fan base kubwa kiasi cha kujaza uwanja wa watu 60elfu, lakini hakuna anaetumia hii potential kuingizia fedha klabu, watu ni wezi tu, hawataki hata watu wakae uwanjani kwa nambari za viti ili kusiwe na takwimu za watu wangapi wameingia uwanjani wao waendelee kuchakachua. TFF wanapokea mamiliono toka kwa wadhamini lakini hawajawahi hata siku moja kutoa tangazo luningani la biashara kuitangaza mechi yoyote ya ligi kuu, wanachoangalia wao ni fursa zilizowazi na hawana ubunifu kutafuta fursa zingine kutangaza ligi na kuongeza mvuto na mashabiki, wanafanya kazi kwa mazoea na uchakachuaji. Mi nilishangaa sana watu wawili wa tasnia moja walipopata nafasi za kazi ktk TFF huku ikijulikana kabisa kuwa hawana jipya, hawana mbinu zozote za kibiashara zinazoendana na wakati huu kidunia, just wameenda pale kujiponya njaa na they are inspired na namna Mwakalebela alivyotajirika haraka

Mambo hayo na mengine mengi kama watu kuingiza siasa kwenye mpira ndio yanasababisha watu kuhamia ughaibuni ambako kwanza soka inavutia mno, kuna mbinu za ufundi zilizo wazi, tofauti na huku wanashindana kwenda kwa waganga wa kienyeji tu. Hakuna ladha ukienda uwanjani, wachezaji wavivu, hawawezi hata kicomplete five passes. Niende uwanjani kufanya nini kama Tegete anaingia kwenye basi kugombana ngumi na shabiki na inachukuliwa poa tu? Nitapendaje soka letu wakati wanaoliendesha hawalipendi?
 
hee! nyinyi vipi...?!!! wawapi nyinyi ..?! utapelekaje weekend bila kuangalia ligi ya uingereza

ARSENAL TILL I DIE
 
Hongera sana kaka kwa kuwa na hoja za kizalendo na zenye tija. Sio ushabiki wa soka tu hata
- imani (dini) watu wanashindia maeneo ya kuabudia wakisali au kuimbasiku nzima kisa eti wanamtukuza mungu!!!!!!!!
- ulevi wa teknolojia ( facebook mpaka darasani), simu mpaka bungeni mbunge akitoa hoja mjengoni!!!!!!!
- mtu mmmoja muuza chipsi ana simu sita kiganjani...... Duh.... Akili matope

sio kwamba ni dunia ya utandawazi...... Bali watanzania tumekuwa limbukeni sana, tumezibukia vitu hivi sanaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom