ushabiki huu wa ligi ya uingereza ni too much sasa.hatari....

sijazungumza kama kero yangu binafsi
na sijasema watu wasishabikie mpira....

na nimeuliza hapo kama society hatupati hasara hapo?
unafahamu lolote kuhusu assimilation ya culture thru vitu kama sports???????/
Athari zipo mkuu jana tulipokuwa tunaangalia mechi pembeni yangu walikaa mme-arsenal na mkewe-man u na wamevaa jezi kabisa,halftime magoli yakiwa 3-1 njemba ikamtelekeza mkewe wa ndoa pale na kuondoka zake bila hata ya kumuaga,maskini mke wa watu baada ya dakika 15 kuona kimya akasimama na kuondoka na teksi,sasa hapa utasema hamna athari kweli ? huko nyumbani kulikuwa na amani kweli ?

Mi sipendi ushabiki. Timu itakayoshinda ndio yangu. Sishangilii hadi mpira uishe nijue nani kashinda.
Kuanzia leo sweety we ni Yanga kwa hapa Bongo na Arsenal kwa Uingereza sawa eeh!

WENYE toleo Na. 104 niliandika kuitahadharisha TBC kuhusu ubia wake na kampuni ya China katika mradi wake wa kuiondoa katika analogy na kuingia digital. Nilitahadharisha kwamba ubia na mwekezaji wa kigeni katika sekta nyeti kama hiyo unapaswa kufanywa kwa makini; vinginevyo tusishangae siku moja Wachina wakitamba na vipindi vyao katika TBC I na TBC Taifa.
Japo niliiandika makala hiyo wiki mbili zilizopita, nimekuwa nikiendelea kupokea barua na ujumbe wa sms na barua pepe kuhusu suala hilo. Moja ya barua hizo nimeichapisha kwenye ukurasa wetu wa barua za wasomaji (uk 8).
Nimeichapisha barua hiyo, kwa sababu mwandikaji ametoa mfano wa ile shaka niliyoizungumzia kwenye makala yangu hiyo. Msomaji huyo anakumbusha katika barua hiyo kwamba Wachina walijitolea kugharimia uanzishaji wa Televisheni ya Mlimani, na sasa vipindi vya Kichina vinatamba katika televisheni hiyo!
Niliposema kwenye makala yangu ile kwamba ukishamruhusu ngamia akaingiza kichwa chake kwenye hema mwisho wa yote ataingiza pia kiwiliwili, nilikuwa naamanisha mambo kama hayo ya Wachina na Televisheni ya Mlimani. Hilo ni funzo kwa TBC.
Hata hivyo, napenda leo kuuendeleza kidogo mjadala kuhusu suala hilo.
Nimejaribu kudadisi ni kwa nini Serikali ya Rais Kikwete iliridhia TBC kuingia ubia na wageni (Wachina), nikaambiwa ni kwa sababu haina fedha za kubadili mfumo wake wa matangazo kutoka analogy kwenda digital kabla muda iliyopewa na vyombo vya kimataifa kukamilisha mabadiliko hayo, haujapita.
Hoja ya kutoka kwenye analogy kwenda digital ni nzito, na kwa sababu mfumo wa analogy unazikwa kote duniani, hakuna mjadala katika suala hilo la mabadiliko.
Lakini je, ni kweli kwamba Serikali ya Kikwete ilishindwa kupata fedha za kugharimia mabadiliko hayo TBC hadi kulazimika kuingia ubia na Wachina katika sekta nyeti kama hiyo?
Sijui jibu lako msomaji ni lipi, lakini labda niweke wazi mapema mtazamo wangu kuhusu uwekezaji wa kigeni katika televisheni au redio nchini. Nimekuwa, kwa mfano, nikikerwa na redio nyingi za FM hapa nchini kuruhusu masafa yao kutumiwa na redio za kigeni kama vile BBC, Deutche Welle, VOA nk kurushia vipindi vyao (kana kwamba ni matawi yao hapa nchini) badala ya kutengeneza vya kwao.
Si siri kwamba ni kwa njia hiyo tunalishwa kidogo kidogo utamaduni wa wazungu, na kidogo kidogo tunaanza kuusahau u-Afrika wetu na u-Tanzania wetu.
Kwa mfano; badala ya kutangaziwa mechi za ligi yetu ya soka ya Tanzania, BBC Idhaa ya Kiswahili inatutangazia mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (mfano Burnley vs Wolves).
Ni kwa njia hiyo, hivi sasa, hadi vijijini wanawajua kina Wayne Rooney kuliko wanavyowajua kina Mrisho Ngassa na Juma Kaseja wetu!
Ni rahisi kuona, hata kijijini, kijana amevaa fulana yenye picha ya Wayne Rooney kuliko kumuona aliyevaa fulana yenye picha ya Kaseja. Na hata ukimletea fulana yenye picha ya kipa huyo wa Simba, hataithamini namna atakavyoithamini ile ya Rooney.
Hapo ndipo vyombo vya mawasiliano vya wazungu vilipotufikisha. Tunaiabudu Premier League ya Uingereza kuliko tunavyoiabudu Ligi Kuu yetu.
Majuzi tu hapa tulimshuhudia Rais wetu Kikwete akiharakisha mazungumzo yake na wananchi kwa njia ya simu, sms na barua pepe; eti ili Watanzania wawahi kuona kwenye televisheni mechi za ligi ya England!
Kwa kauli yake ile kwamba “tumalize haraka wananchi waone mechi za England”, ilikuwa ni wazi kwamba Kikwete ni mmoja wa waathirika wa ‘utamaduni’ huo wa Uingereza tunaolishwa na Waingereza kupitia tv zetu.
Naambiwa akiwa Uingereza, Kikwete aliwahi hata kwenda uwanjani kuangalia mechi ya Ligi Kuu ya England wakati hapa nyumbani hakuna kumbukumbu kwamba alipata kuhudhuria mechi yoyote ya Ligi Kuu yetu (sizungumzii Taifa Stars)! Kwa ufupi, sote ni waathirika wa ubeberu huu wa utamaduni (cultural imperialism).
Tunavutwa kushabikia utamaduni wao na mambo yao mengine kwa sababu ya mambo tunayolishwa na vyombo vyao vya habari.
Tumefikishwa mahali ambapo Barclays Bank (benki ya Uingereza) inapanga kulileta kombe la Premier League ya Uingereza na kulitembeza hapa nchini; ilhali tawi la Barclays Bank la hapa Tanzania halijawahi kulitembeza kwa wananchi kombe letu la Ligi Kuu!
Na kwa sababu mabosi wa vituo vyetu vya tv wanataka kutoana roho kugombea haki ya kuonyesha mechi hizo za Ligi Kuu ya England, tumeaminishwa kwamba ligi yetu haina maana na si muhimu.
Hiyo ndiyo nguvu ya vyombo vya habari; nguvu ambayo imetufanya tupoteze identity yetu kama Waafrika na kama Watanzania. Nguvu ambayo imetufanya tusijiamini mbele ya wazungu; kiasi kwamba akijitokeza Dk. James Watson na kusema kwamba bongo za watu weusi zina walakini, sisi wenyewe weusi tunaamini hivyo kwa sababu tulishamalizwa mapema kisaikolojia na vyombo vyao vya habari vinavyotuzunguka.
Kulia ni Waingereza na BBC yao, kushoto ni Wamarekani na VOA yao, nyuma ni Wajerumani na Deutche Welle yao, mbele ini Wachina na Radio Beijing nk.
Upande mwingine pia zipo televisheni za kigeni, filamu za kigeni, vitabu vya kigeni, magazeti ya kigeni, internet nk. Kila kona tunalishwa tamaduni zao; kiasi kwamba tunaelekea kupoteza kabisa identity yetu kama Waafrika.
Najua suala hili si rahisi kulielezea likaeleweka vyema; lakini nawashawishi wasomaji wangu wamsome John Tomlison katika Cultural Imperialism: A critical introduction ili wafumbuke macho.
Nihitimishe kwa kusema kwamba si nia yangu kuwahamasisha Watanzania kuacha kutazama CNN, BBC au kusikiliza Deutche Velle au kuangalia filamu za Holywood au mechi za soka za England au kusoma vitabu vyao vya riwaya. La hasha.
Ninachosema ni kwamba tuyafanye yote hayo tukiwa tunatambua kwamba vyote hivyo ni wakala wa utamaduni wa wazungu. Tukitambua hivyo, angalau tutajihami kwa kukataa kukubali ndani ya vichwa na ndani ya nafsi zetu kwamba sisi si lolote wala chochote mbele ya wazungu.
Angalau UNESCO miaka ile ya 80 ilijitahidi kutusaidia kujihami hivyo ilipopigania kuanzishwa kwa mfumo mpya wa habari duniani (New International Information Order). UNESCO ilitaka kuwe na mtiririko sawia wa habari (na utamaduni) baina ya nchi tajiri na masikini duniani. Yaani iwe two way traffic.
Lojiki ya UNESCO ilikuwa kwamba kama (kwa mfano) wazungu wanataka kutuonyesha utamaduni wao kupitia vichekesho vya Mr. Bean, basi nasi tunapaswa kuwaonyesha utamaduni wetu kupitia vichekesho vya kina orijino komedi.
Kwa maneno mengine, kama wao wana kina Van Damme na kina Julia Roberts wao, basi nasi tuna kina Steven Manumba wetu!
Lakini nini kilitokea? Kilichotokea ni kwamba Marekani na Uingereza viliupiga vita mpango huo wa UNESCO hata kufikia hatua ya kujitoa uanachama katika shirika hilo la Umoja wa Mataifa. Walirejea tu na kuendelea kulifadhili baada ya UNESCO kusalimu amri kwa kuutosa mpango huo.
Leo hii, ukiangalia wazungu wanavyohaha kununua mamilioni ya hekta za ardhi barani Afrika (ikiwemo Tanzania), jinsi pia wanavyohaha kuturushia tamaduni zao (kupitia vyombo nilivyovitaja mwanzoni) na namna tunavyozidaka haraka tamaduni hizo (rejea kupapatikia Valentine Day, Fiesta, baba na mama na watoto ndani ya swimming pool moja wakiwa na vichupi, Big Brother nk), huwezi kukataa kwamba ukoloni mkongwe unarejea tena kwa kasi nchini!
Najua wako watakaosema kwamba haya niliyoyajadili yamepitwa na wakati katika zama hizi za utandawazi ambapo dunia imekuwa kijiji kimoja. Jibu langu kwao ni kwamba hata katika utandawazi huu, Waafrika wamo kwenye receiving end tu kwa sababu mfumo wenyewe ni wa one way traffic iwe ni kwenye biashara au utamaduni.
Tafakari
hs3.gif

Nyeusi: mkuu toleo la kitu gani, gazeti? jarida? au?
Nimependa sana uliyoyaandika hapo juu..hiki ni chakula cha fikra...
Lakini hapo kwenye maandishi mekundu umeniacha kidogo..huyo mwandishi ni mzungu au? Kama ndio argument yako ya msingi inakua inakosa credibility kwani huyu mzungu hawezi kumfumbua macho muafrika au mtanzania kwa kiwango ambacho umejaribu kukieleza...kuna school of thought moja inaitwa post colonial theory; hii ipo katika masuala ya siasa za ekolojia..msingi wa skuli hiyo ni kuandikwa historia na mambo ya Afrika na waafrika wenyewe..rewriting history throught the minds of the colonised..naomba ufafanuzi.

naona hunielewi kabisaaa

nilichofanya hapa sio ku condemn

but kutoa opinion na kuacjia wengine wazungumze

nimeuliza swali hapo,je hakunahasara as societyt??????/

kwa kauli na mtazamo wako ninahakika wewe nawe ni shabiki wa arsenal, pole sana!

Nyeusi: mkuu toleo la kitu gani, gazeti? jarida? au?
Nimependa sana uliyoyaandika hapo juu..hiki ni chakula cha fikra...
Lakini hapo kwenye maandishi mekundu umeniacha kidogo..huyo mwandishi ni mzungu au? Kama ndio argument yako ya msingi inakua inakosa credibility kwani huyu mzungu hawezi kumfumbua macho muafrika au mtanzania kwa kiwango ambacho umejaribu kukieleza...kuna school of thought moja inaitwa post colonial theory; hii ipo katika masuala ya siasa za ekolojia..msingi wa skuli hiyo ni kuandikwa historia na mambo ya Afrika na waafrika wenyewe..rewriting history throught the minds of the colonised..naomba ufafanuzi.

mkuu sory kwa kutomtaja muandishi hapo
siyo article yangu
raia mwema,johnson mbwambo...

unasahau matatizo kwa kuwaongezea pesa waingereza?

hivi unajua kila mtanzania anaetazama ligi ya uingereza anawalipa waingereza?????

pesa????????

najua boss,,,ila watz wanaondoa stress

Weekend bila Premier league haiendi kabisa!
kwanza ligi ya uingereza umeturahisishia njia ya kupata VIZA kutoka kwa wake zetu bila maswali mengi!

Sasa kama binafsi haijakukera...wala hujaona/hujui kama kuna athari/hasara yoyote kwa jamii inayoweza kutokana huo ushabiki iweje umeanza kwa kucondemn?!
Nshajua we shabiki wa Asenali
pole bibie!!!!!!!!!!

Media inaseaidia sana katika kufanya watu wapende kitu. Media za wingereza zimesaidai sana kuteka washabiki wa mpira na sa hivi karibia dunia nzima inatizama EPL, mi nakumbuka kuna wakati ITV ilikua inaonyesha sana ligi ya NBA, kama sikusei ilikua katitkati ya miaka ya Tisini na vijana wengi hasa wa sekondari walipenda mpira. kwa hiyo kama Media zetu zitajika sana sana katika kushabikia ligi ya kwetu pamoja na watu kupenda ligi za nje bado kuna uwezekano mkubwa kwa watu kuendelea kuzipenda ligi za kwetu. sasa hivi karibia kila mkoa una redio kwa hiyo kama hizi redio zikitumika vizuri kuhamasisha watu wa eneo hilo kuipenda timu yao hapo nadhani tutaanza kujenga "loyality" kama vile ilivyo wingereza yaani kila watu wa mji fulani wanapenda timu ya mji wao regardless kua hiyo timu inafanya vizuri au haifanyi vizuri.
kuna wakati pia kipindi cha ITV cha michezo cha jumapili kilikua kina promote sana mchezo wa ngumi yaani kila jumapili Izack Gamba lazima azungumzie mapambano ya ngumu na hii ikasababisha watu kuanza kuupenda mchezo wa ngumi na kwenye mapambano watu walikua wanafurika sana.

Premier imesheheni the best players kutoka pembe zote za dunia,kutokana na hili quality ya premier football ni ya kiwango cha juu hivo kuvutia mashbiki wengi.
Kuhusu cultura assimilation versus kupenda cha kwetu "tukubali ya ishe" American cultural conquest ni dhahiri. Shuhudia American cultural influence maishani mwetu: cocacola,gillete,hiphop and jazz,proudly wear levi and strauss jeans. American cultural carpet bombing is victorious halina ubishi. Chinua Achebe said we have had a different past, strictly speaking we will have same future. I do agree.

hata hivyo wizara ya afya imetoa onyo kali sana kuhusu mashabiki wa arsenal.
yaani kweli naitaji matibabu maalum kumbe ndo maana nilivotoa thread ya kutafuta rafiki nikasema lazima awe arsenal fan sijapata mtu eeh?

Similar Discussions

Back
Top Bottom