ushabiki huu wa ligi ya uingereza ni too much sasa.hatari.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ushabiki huu wa ligi ya uingereza ni too much sasa.hatari....

Discussion in 'Sports' started by The Boss, Aug 29, 2011.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Nafahamu kuna watu wengi wana wehu wa mpira na ushabiki hauna logic

  but mimi mwenzenu naona tulipofika kama watanzania au waafrika ni too much

  tena ni hatari mno....LIGI YA UINGEREZA hii jamani.......siyo ya kwetu....

  unakutana na houseboy ambae hata shule yamsingi hakumaliza
  wala aikoneshwa ramani ya dunia akuoneshe england ilipo hawezi...but yuko so sad
  kwa sababu arsenal imefungwa.....wamama wauza sokoni wanazungumzia manchester united..

  watu hawajawahi hata kufika uwanja wa taifa but wanajua timu yote ya chelsea na wake wa wachezaji wa chelsea..

  yaani unakuta mkeo,mama yako mzazi,ndugu zako,rafiki zako,ofisini
  mitaani......wanazungumza mechi ya jana mpira......

  mbona zamani hatukuwa hivyoo??????

  hivi hili halina hasara ya aina yoyote ile kwetu?????????

  mimi naona sasa ni too much...
  mpaka vijijini watu wanasikitika kufungwa kwa arsenal?

  ikwiriri na tandahimba??????/jamaniii
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama mtu anapenda mpira acha awe shabiki wa mpira!!

  Kwani tatizo liko wapi?!Wengine wanapokua wanashabikia na kujua hayo yote wewe wanakupunguzia nini?!Binafsi sio shabiki wa mpira ila kusikia na kusoma watu wakiongelea kufungwa kwa timu yoyote ile hakunisumbui. Kwasababu tu kitu fulani siyo starehe yangu hakunipi mimi kibali cha kuchukia kuona mtu mwingine akikifurahia.. .ili mradi hainipunguzii kitu!‘
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  sijazungumza kama kero yangu binafsi
  na sijasema watu wasishabikie mpira....

  na nimeuliza hapo kama society hatupati hasara hapo?
  unafahamu lolote kuhusu assimilation ya culture thru vitu kama sports???????/
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa kama binafsi haijakukera...wala hujaona/hujui kama kuna athari/hasara yoyote kwa jamii inayoweza kutokana huo ushabiki iweje umeanza kwa kucondemn?!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  naona hunielewi kabisaaa
  nilichofanya hapa sio ku condemn
  but kutoa opinion na kuacjia wengine wazungumze
  nimeuliza swali hapo,je hakunahasara as societyt??????/
   
 6. B

  Balozi Chriss Senior Member

  #6
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante sana kwa thread yako.Mimi naomba sasa jamani tuipende soka yetu,kwani bila sisi haitaendelea.
   
 7. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Wamarekani weusi walipokuwa wakiteswa sana na wazungu huku wakinyimwa fursa za kielimu faraja yao ilikuwa sanaa {kuimba, kucheza, kuigiza n.k} ndio maana wanamichezo, wanamuziki wengi maarufu wamekuwa wenye asili ya Afrika.

  South Africa chini ya mkaburu walijifariji kwa nyimbo hivyo kuwafanya kuwa mahiri ktk eneo hilo.

  Watanzania wanabeba machungu mengi vifuani ni bora wakapokea maudhi/mazuri ya asiyewajua (arsenal/man u/ chelsea) kuliko mateso yaletwayo na chaguo la "mungu"!

  Boss tumeshauza kila kilicho chetu hivyo hiyo assimilation ya culture wala isikutishe maana hatuna tulichobakiza.
   
 8. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  ilaumiwe fat ya ndolanga na tff kwa kuua soka.
  Chaneta nao walaumiwe kwa kuuwa netball.
  Relwe gerezani nasikia umekuwa ukumbi wa disco
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Boss ana hoja ya msingi hapa...
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sikuelewi au hujielewi!!?!

  Maana ulishaanza kulalamika kwamba the whole thing is too much wakati binafsi haikukeri wala hujui kama kuna madhara yoyote kwa society!!Kwahiyo hata nikukuuliza kwanini unadhani/umesema ushabiki huo ni too much hutakuwa na jibu!!
   
 11. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,124
  Likes Received: 23,726
  Trophy Points: 280
  Relwe Gerezani nasikia mpaka kuna ka--swimming pool flani hivi~enzi zile bana netball ndio ilikuwa pahala pake. Mambo ya Jeshi star wakichuana na Mbweni JKT~.
   
 12. kishoreda

  kishoreda Senior Member

  #12
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu The Boss hoja yako ni ya msingi sana na ni muhimu kabisa.Ila watu sio kama hawataki soka la hapa nyumbani suala hapa hadi miaka 50 ya uhuru tuna maendeleo gani katika suala zima la michezo hasa soka?Mm binafsi ni shabiki mzuri sana la soka la hapa bongo ila maumivu ninayoyapata ninapoenda kushabikia timu yangu ya Yanga au timu ya taifa inapocheza na timu yoyote ya nje ni bora nishabikie Man u ambayo haipiti msimu bila kunipa raha.Huu ni mfano tu kwa upande wangu naamini wapo wadau wengi ambao wako kama mm.m2 anadunduliza vijisenti vyake ili akaione timu yake ya taifa,Simba au Yanga akitoka kwenye mechi anajilaumu bora angeenda kunywea bar na kuongeza mapato ya serekali.Kiufupi Wa tz kama tumelogwa katika suala zima la michezo
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kuna washabiki wengi wa Man City Manchester kuliko wa Man United
  Wakazi wengi wa Newcastle wanashabikia Newcastle United....
  Birmingham kumejaa washabiki wa Villa, Birmingham City na Westbrom

  Kila mtu wa Wolverhampton anashabikia Wolves....

  Ni nini cha kujifunza hapo juu...!!??

  Loyalty... na mtu kupenda chake sio kuwa Glory Hunters.., tupende vya nje lakini vya nyumbani haviwezi kukua bila support yetu wenyewe na issue ya kusema kwamba kiwango ni kidogo isiwe sababu.

  Kuna tofauti kubwa ya Fan na Supporter..., hivyo basi hata kama wewe ni Fan wa timu ya nje (na unapenda mpira) basi si vibaya ukiwa Supporter wa home grown talent...
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo mkuu wewe ni Glory Hunter na sio shabiki wa mpira au timu na ina maana kwamba ungezaliwa enzi za 1970's ungekuwa mshabiki wa Liverpool na kwa maneno yako ni kwamba washabiki wote wa England wangekuwa wanashabikia United na timu kama Watford, Walsall na Charlton zisingepata mshabiki hata mmoja...

  Na kiwango kisiwe ni sababu, kwenye michezo kitu cha maana ni competition ndio maana hata mechi za watoto wa shule huwa zinavutia.. sababu ya competition kali.., hapa Bongo sababu kubwa ni kwamba watu wameamua kuachana na timu za nyumbani... sababu kama kuna upenzi na following kubwa hata ligi daraja la nne au mechi za mtaani bado zinaweza zikawa burudani tosha
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  WENYE toleo Na. 104 niliandika kuitahadharisha TBC kuhusu ubia wake na kampuni ya China katika mradi wake wa kuiondoa katika analogy na kuingia digital. Nilitahadharisha kwamba ubia na mwekezaji wa kigeni katika sekta nyeti kama hiyo unapaswa kufanywa kwa makini; vinginevyo tusishangae siku moja Wachina wakitamba na vipindi vyao katika TBC I na TBC Taifa.
  Japo niliiandika makala hiyo wiki mbili zilizopita, nimekuwa nikiendelea kupokea barua na ujumbe wa sms na barua pepe kuhusu suala hilo. Moja ya barua hizo nimeichapisha kwenye ukurasa wetu wa barua za wasomaji (uk 8).
  Nimeichapisha barua hiyo, kwa sababu mwandikaji ametoa mfano wa ile shaka niliyoizungumzia kwenye makala yangu hiyo. Msomaji huyo anakumbusha katika barua hiyo kwamba Wachina walijitolea kugharimia uanzishaji wa Televisheni ya Mlimani, na sasa vipindi vya Kichina vinatamba katika televisheni hiyo!
  Niliposema kwenye makala yangu ile kwamba ukishamruhusu ngamia akaingiza kichwa chake kwenye hema mwisho wa yote ataingiza pia kiwiliwili, nilikuwa naamanisha mambo kama hayo ya Wachina na Televisheni ya Mlimani. Hilo ni funzo kwa TBC.
  Hata hivyo, napenda leo kuuendeleza kidogo mjadala kuhusu suala hilo.
  Nimejaribu kudadisi ni kwa nini Serikali ya Rais Kikwete iliridhia TBC kuingia ubia na wageni (Wachina), nikaambiwa ni kwa sababu haina fedha za kubadili mfumo wake wa matangazo kutoka analogy kwenda digital kabla muda iliyopewa na vyombo vya kimataifa kukamilisha mabadiliko hayo, haujapita.
  Hoja ya kutoka kwenye analogy kwenda digital ni nzito, na kwa sababu mfumo wa analogy unazikwa kote duniani, hakuna mjadala katika suala hilo la mabadiliko.
  Lakini je, ni kweli kwamba Serikali ya Kikwete ilishindwa kupata fedha za kugharimia mabadiliko hayo TBC hadi kulazimika kuingia ubia na Wachina katika sekta nyeti kama hiyo?
  Sijui jibu lako msomaji ni lipi, lakini labda niweke wazi mapema mtazamo wangu kuhusu uwekezaji wa kigeni katika televisheni au redio nchini. Nimekuwa, kwa mfano, nikikerwa na redio nyingi za FM hapa nchini kuruhusu masafa yao kutumiwa na redio za kigeni kama vile BBC, Deutche Welle, VOA nk kurushia vipindi vyao (kana kwamba ni matawi yao hapa nchini) badala ya kutengeneza vya kwao.
  Si siri kwamba ni kwa njia hiyo tunalishwa kidogo kidogo utamaduni wa wazungu, na kidogo kidogo tunaanza kuusahau u-Afrika wetu na u-Tanzania wetu.
  Kwa mfano; badala ya kutangaziwa mechi za ligi yetu ya soka ya Tanzania, BBC Idhaa ya Kiswahili inatutangazia mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (mfano Burnley vs Wolves).
  Ni kwa njia hiyo, hivi sasa, hadi vijijini wanawajua kina Wayne Rooney kuliko wanavyowajua kina Mrisho Ngassa na Juma Kaseja wetu!
  Ni rahisi kuona, hata kijijini, kijana amevaa fulana yenye picha ya Wayne Rooney kuliko kumuona aliyevaa fulana yenye picha ya Kaseja. Na hata ukimletea fulana yenye picha ya kipa huyo wa Simba, hataithamini namna atakavyoithamini ile ya Rooney.
  Hapo ndipo vyombo vya mawasiliano vya wazungu vilipotufikisha. Tunaiabudu Premier League ya Uingereza kuliko tunavyoiabudu Ligi Kuu yetu.
  Majuzi tu hapa tulimshuhudia Rais wetu Kikwete akiharakisha mazungumzo yake na wananchi kwa njia ya simu, sms na barua pepe; eti ili Watanzania wawahi kuona kwenye televisheni mechi za ligi ya England!
  Kwa kauli yake ile kwamba "tumalize haraka wananchi waone mechi za England", ilikuwa ni wazi kwamba Kikwete ni mmoja wa waathirika wa ‘utamaduni' huo wa Uingereza tunaolishwa na Waingereza kupitia tv zetu.
  Naambiwa akiwa Uingereza, Kikwete aliwahi hata kwenda uwanjani kuangalia mechi ya Ligi Kuu ya England wakati hapa nyumbani hakuna kumbukumbu kwamba alipata kuhudhuria mechi yoyote ya Ligi Kuu yetu (sizungumzii Taifa Stars)! Kwa ufupi, sote ni waathirika wa ubeberu huu wa utamaduni (cultural imperialism).
  Tunavutwa kushabikia utamaduni wao na mambo yao mengine kwa sababu ya mambo tunayolishwa na vyombo vyao vya habari.
  Tumefikishwa mahali ambapo Barclays Bank (benki ya Uingereza) inapanga kulileta kombe la Premier League ya Uingereza na kulitembeza hapa nchini; ilhali tawi la Barclays Bank la hapa Tanzania halijawahi kulitembeza kwa wananchi kombe letu la Ligi Kuu!
  Na kwa sababu mabosi wa vituo vyetu vya tv wanataka kutoana roho kugombea haki ya kuonyesha mechi hizo za Ligi Kuu ya England, tumeaminishwa kwamba ligi yetu haina maana na si muhimu.
  Hiyo ndiyo nguvu ya vyombo vya habari; nguvu ambayo imetufanya tupoteze identity yetu kama Waafrika na kama Watanzania. Nguvu ambayo imetufanya tusijiamini mbele ya wazungu; kiasi kwamba akijitokeza Dk. James Watson na kusema kwamba bongo za watu weusi zina walakini, sisi wenyewe weusi tunaamini hivyo kwa sababu tulishamalizwa mapema kisaikolojia na vyombo vyao vya habari vinavyotuzunguka.
  Kulia ni Waingereza na BBC yao, kushoto ni Wamarekani na VOA yao, nyuma ni Wajerumani na Deutche Welle yao, mbele ini Wachina na Radio Beijing nk.
  Upande mwingine pia zipo televisheni za kigeni, filamu za kigeni, vitabu vya kigeni, magazeti ya kigeni, internet nk. Kila kona tunalishwa tamaduni zao; kiasi kwamba tunaelekea kupoteza kabisa identity yetu kama Waafrika.
  Najua suala hili si rahisi kulielezea likaeleweka vyema; lakini nawashawishi wasomaji wangu wamsome John Tomlison katika Cultural Imperialism: A critical introduction ili wafumbuke macho.
  Nihitimishe kwa kusema kwamba si nia yangu kuwahamasisha Watanzania kuacha kutazama CNN, BBC au kusikiliza Deutche Velle au kuangalia filamu za Holywood au mechi za soka za England au kusoma vitabu vyao vya riwaya. La hasha.
  Ninachosema ni kwamba tuyafanye yote hayo tukiwa tunatambua kwamba vyote hivyo ni wakala wa utamaduni wa wazungu. Tukitambua hivyo, angalau tutajihami kwa kukataa kukubali ndani ya vichwa na ndani ya nafsi zetu kwamba sisi si lolote wala chochote mbele ya wazungu.
  Angalau UNESCO miaka ile ya 80 ilijitahidi kutusaidia kujihami hivyo ilipopigania kuanzishwa kwa mfumo mpya wa habari duniani (New International Information Order). UNESCO ilitaka kuwe na mtiririko sawia wa habari (na utamaduni) baina ya nchi tajiri na masikini duniani. Yaani iwe two way traffic.
  Lojiki ya UNESCO ilikuwa kwamba kama (kwa mfano) wazungu wanataka kutuonyesha utamaduni wao kupitia vichekesho vya Mr. Bean, basi nasi tunapaswa kuwaonyesha utamaduni wetu kupitia vichekesho vya kina orijino komedi.
  Kwa maneno mengine, kama wao wana kina Van Damme na kina Julia Roberts wao, basi nasi tuna kina Steven Manumba wetu!
  Lakini nini kilitokea? Kilichotokea ni kwamba Marekani na Uingereza viliupiga vita mpango huo wa UNESCO hata kufikia hatua ya kujitoa uanachama katika shirika hilo la Umoja wa Mataifa. Walirejea tu na kuendelea kulifadhili baada ya UNESCO kusalimu amri kwa kuutosa mpango huo.
  Leo hii, ukiangalia wazungu wanavyohaha kununua mamilioni ya hekta za ardhi barani Afrika (ikiwemo Tanzania), jinsi pia wanavyohaha kuturushia tamaduni zao (kupitia vyombo nilivyovitaja mwanzoni) na namna tunavyozidaka haraka tamaduni hizo (rejea kupapatikia Valentine Day, Fiesta, baba na mama na watoto ndani ya swimming pool moja wakiwa na vichupi, Big Brother nk), huwezi kukataa kwamba ukoloni mkongwe unarejea tena kwa kasi nchini!
  Najua wako watakaosema kwamba haya niliyoyajadili yamepitwa na wakati katika zama hizi za utandawazi ambapo dunia imekuwa kijiji kimoja. Jibu langu kwao ni kwamba hata katika utandawazi huu, Waafrika wamo kwenye receiving end tu kwa sababu mfumo wenyewe ni wa one way traffic iwe ni kwenye biashara au utamaduni.
  Tafakari
  [​IMG]
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  huwezi kunielewa
  walionielewa so far wameelewe ninachozungumza

  again narudia,sizungumzii kero ya kwangu individual.....
  weather hasara sijazitaja au la haliondoi pointi hapa
   
 17. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mi sipendi ushabiki. Timu itakayoshinda ndio yangu. Sishangilii hadi mpira uishe nijue nani kashinda.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  inasaidia wasahau matatzo yao kwa muda
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  inawezekana umasikini na hali ya kutojithamini imeongeza
  glory hunter weengi mno tanzania
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  unasahau matatizo kwa kuwaongezea pesa waingereza?
  hivi unajua kila mtanzania anaetazama ligi ya uingereza anawalipa waingereza?????
  pesa????????
   
Loading...