Nadhani hujui ndugu, kasome upya. Hata quran ni maneno ya Mwenyezi MUNGU ananena na sisi, kwani wewe huwa humsikii!! Ukisoma quran unadhani ni mashairi yale? Ni nani mtamkaji wa yale yaloandikwa?? Naomba ujue pia ibada pia ni mawasiliano baina ya mja na mola wake, inawezekana hujui na yawezekana imanj yako ni haba kiasi ambacho huoni hata majibu ya maombi yako. Ndugu, mtegemee Mwenyezi MUNGU utamsikia akisema na wewe binafsi. Maandiko yanasema "na waja wangu watakapokuuliza habari zangu; waambie, MIMI nipo karibu, ninasikia na ninajibu maombi ya mwombaji anaponiomba, basi na waniitikie mimi, na waniamini MIMI ili wapate kuongoka (quran 2:186)
Hebu niambie hiyo aya ni nani anaongea? Na anamwambia nani.
Mkuu nenda kasome sio unakariri.
Halafu, sisi tumeitwa ni umma bora; Hivi unajua kwanini tumeitwa hivyo?? Ni kwasababu tunafanya kazi waliyokuwa wakifanya mitume hapo awali, yaani kukumbushana mema na kukatazana mabaya. Je, Mja anayetenda kazi ya mitume Mwenyezi MUNGU hawezi kuwa karibu naye?? Jibu unalo.