shalet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 3,441
- 3,613
Habari wakuu,
Jana wakati naangalia Star Tv kipindi cha mahuburi ya huyu jamaa Malisa nilishangazwa na jambo moja ambalo yeye analiita muujiza wa kuwaingizia watu pesa kwenye akaunti zao kama ni mpesa tigopesa au airtell money.
Sina shaka na uwezo wa kufikiri wa waumini wa makanisa ya miujiza kuwa ni mdogo ndio maana wanatapeliwa ila kinachonisikitisha ni huyu nabii kuhisi kuna wajinga hata nje ya kanisa lake anaweza kuwadanganya kwa miujiza feki ya kuwawekea watu kwenye pesa na kuna wajinga kama watatu walikimbilia mbele kwenda kushuhudia kuwa wamewekewa pesa na malaika kimiujiza ila hawakuonyesha ushahidi wowote katika kitu kinachoonyesha.
Ile hali ilikuwa staged maneno waliyokuwa wanaongea wale watu ni very identical, mwisho kabisa huyu nabii mwenye uwezo wa kuwawekea watu pesa kimiujiza yeye alikuwa anaomba achangiwe kwa mpesa na tigo pesa kwa namba alizokuwa anataja yaani muujiza haufanyi kazi kwake ila kwa waumini tu.
Amkeni wakristo wezangu tusiwe kondoo kwenye kila kitu.