Usanii wa nabii Malisa na miujiza feki

Usanii wa nabii Malisa na miujiza feki

Kwahiyo Bandiwe, muislaam aliyepotoka akaenda huko kwa sheikh yahaya ama kunako ramli kwingineko, atakuwa siyo muislaam tena? Navipi katika toba? Toba maanake ni nini? Mi naamini binadamu yeyote hukosea. Na baada yakukosea anafanya toba. Ila dini yake inakuwa palepale.
Kuna sharti za toba, mojawapo ni kutorejea dhambi ileile wakati unajua.
 
Huyo ni mfanya biashara na amekua mbunifu kama mwanamazingaumbwe feki wa shule ya msingi.
 
Kwa sababu ya watu wengi kuwa nachangamoto kwa sasa, hao nabii feki wataendelea kupiga tu, sawa sawa na tatizo la ajira lilivyo hivi sasa.
 
Huyo ni mfanya biashara na amekua mbunifu kama mwanamazingaumbwe feki wa shule ya msingi.
Watanzania sijui tutabadilika lini..nawahurumia sana hawa..hivi we ni mtumishi gani anataka utoe sadaka kupitia tigo pesa au M-pesa??akiwa na maana kwamba hajali hata uwepo wako hapo kanisani!
 
Kuna sharti za toba, mojawapo ni kutorejea dhambi ileile wakati unajua.
Wewe mwenyewe unaweza kutuhakikishia sisi na mola wako kwamba hujawahi kuirudia dhambi ambayo tayari ulishaifanyia toba mkuu? Kwamaana nyingine inamaana dhambi ulizonazo zooote nimpya ukilinganisha na ulizotubu ktk ramadhan iliyopita.

Kuandikwa ni suala moja nakuyaishi ni suala jingine mkuu.
 
Habari wakuu,

Jana wakati naangalia Star Tv kipindi cha mahuburi ya huyu jamaa Malisa nilishangazwa na jambo moja ambalo yeye analiita muujiza wa kuwaingizia watu pesa kwenye akaunti zao kama ni mpesa tigopesa au airtell money.

Sina shaka na uwezo wa kufikiri wa waumini wa makanisa ya miujiza kuwa ni mdogo ndio maana wanatapeliwa ila kinachonisikitisha ni huyu nabii kuhisi kuna wajinga hata nje ya kanisa lake anaweza kuwadanganya kwa miujiza feki ya kuwawekea watu kwenye pesa na kuna wajinga kama watatu walikimbilia mbele kwenda kushuhudia kuwa wamewekewa pesa na malaika kimiujiza ila hawakuonyesha ushahidi wowote katika kitu kinachoonyesha.

Ile hali ilikuwa staged maneno waliyokuwa wanaongea wale watu ni very identical, mwisho kabisa huyu nabii mwenye uwezo wa kuwawekea watu pesa kimiujiza yeye alikuwa anaomba achangiwe kwa mpesa na tigo pesa kwa namba alizokuwa anataja yaani muujiza haufanyi kazi kwake ila kwa waumini tu.

Amkeni wakristo wezangu tusiwe kondoo kwenye kila kitu.

Aisee kwa hiyo miujiza inafanyika kwa waumini wake tuu ila kwake hola....
 
Wewe mwenyewe unaweza kutuhakikishia sisi na mola wako kwamba hujawahi kuirudia dhambi ambayo tayari ulishaifanyia toba mkuu? Kwamaana nyingine inamaana dhambi ulizonazo zooote nimpya ukilinganisha na ulizotubu ktk ramadhan iliyopita.

Kuandikwa ni suala moja nakuyaishi ni suala jingine mkuu.
Mkuu, leo unazini, kesho unaenda kutubu. Kesho tena unazini, keshokutwa unaenda kutubu! Hiyo ni toba au kumchezea Mwenyezi MUNGU!! Mkuu Mwenyezi MUNGU sio wa kuchezea chezea kama watu wanavodhani. Lakini pia mwenyezi MUNGU anaseama " na Mwenyezi MUNGU ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu" (quran 2: 218). Kuna aya nyingi zinazungumzia toba ya kweli, na ni mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia kweli. Toba ya kweli inaambatana na kujutia. Vilevile Mwenyezi MUNGU anawajua wenye kutubia kwelikweli.
 
NDO MANA KANISA MAMA LINA AMINI MAPADRE WAO WAANZE NA FALSAFA KWANZA KABLA YA TEOLOJIA ILI WAPATE UFAHAMU MKUBWA JUU YA IMANI. HIVYO NI LAZIMA UKIJUE KITU KABLA YA KUAMINI.
Kuna ndugu yangu alipata tatizo la kuchanganyikiwa kiaina yan kuona vitu ambavyo havipo kiuhalisia. Walokole wakamdaka wakasema amepata mapepo wacha wapige sala. Nisivowaamini to the extremely highest degree, mimi nkaenda kwa padri nkamweleza story nzima. Padri akanifafanulia vizuri akanambia muwahisheni hospitali mkichelewa ataokota makopo. Alivopata tiba amepona mpk leo mzima. Kama ni pepo mbona limetoka kwa sindano?? Walokole acheni kujitoa ufahamu.
 
Mkuu, leo unazini, kesho unaenda kutubu. Kesho tena unazini, keshokutwa unaenda kutubu! Hiyo ni toba au kumchezea Mwenyezi MUNGU!! Mkuu Mwenyezi MUNGU sio wa kuchezea chezea kama watu wanavodhani. Lakini pia mwenyezi MUNGU anaseama " na Mwenyezi MUNGU ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu" (quran 2: 218). Kuna aya nyingi zinazungumzia toba ya kweli, na ni mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia kweli. Toba ya kweli inaambatana na kujutia. Vilevile Mwenyezi MUNGU anawajua wenye kutubia kwelikweli.
Najua sana mkuu kwamba mwenyezi Mungu sikama sisi wanadamu nawala hakuna wakujilinganisha wala wakulinganisha naye katika nyanja yoyote.

Yeye anajua waliowake namimi nawewe hatujui tuko ktk fungu lipi mbele zake. Kwahiyo tukazane katika kumcha yeye, kuwatendea wenzetu yaliyokuwa mema nakuwaombea wale wenye kupotoka ili wafanye toba wamlejee mola wao na si kuwahukumu. Mwenye kumuhesabia mwanadamu haki ama dhambi ni yeye mwenyewe Allah kwahiyo tuhepuke kutoa maneno yenye mwelekeo yakuhukumu wenzetu kana kwamba sisi tu malaika.
 
Siku hizi dini ni biashara

Ntabaki kwenye dhehebu langu LA toka utotoni
 
Kitu kingine wakristo wengi tunataka muujiza ya haraka na tunasahau kuutafuta ufalme WA Mungu

Hakika ukisoma NENO LA Mungu na kuliweka moyon hutakaa na kuhangaika na miujiza isiyo na Baraka za Mungu
 
Najua sana mkuu kwamba mwenyezi Mungu sikama sisi wanadamu nawala hakuna wakujilinganisha wala wakulinganisha naye katika nyanja yoyote.

Yeye anajua waliowake namimi nawewe hatujui tuko ktk fungu lipi mbele zake. Kwahiyo tukazane katika kumcha yeye, kuwatendea wenzetu yaliyokuwa mema nakuwaombea wale wenye kupotoka ili wafanye toba wamlejee mola wao na si kuwahukumu. Mwenye kumuhesabia mwanadamu haki ama dhambi ni yeye mwenyewe Allah kwahiyo tuhepuke kutoa maneno yenye mwelekeo yakuhukumu wenzetu kana kwamba sisi tu malaika.
Mkuu maneno ya Mwenyezi MUNGU yapo wazi kabisa, haki imejipambanua na batli imejipambanua. Neno la Mwenyezi MUNGU ndio linalohukumu, si mimi, wala si yeyote yule, bali ni Neno. Mwenyezi MUNGU ni mwaminifu wa neno lake na kamwe havunji miadi. Hata mtoto wako akikukosea leo na akatubu utamsamehe na kesho utamsamehe, na mara ya tatu lakini akirudia kosa lile lile kila mara, ni lazima utamuadhibu ili asipotee ikiwa kweli unampenda. Kadhalika Mwenyezi MUNGU anaweza kukuadhibu hapa hapa duniani ili usipotee moja kwa moja. Adhabu ya duniani inakukumbusha utubu ili usiwe wa shetani moja kwa moja! Nataka nikwambie ukweli; Ukifanya toba ya kweli utasamehewa; Na hakika Mwenyezi MUNGU anawajua wafanyao toba ya kweli, kamwe huwezi kumletea maigizo halafu asijue. Kumbuka, kama upo hai basi tambua kuwa milango ya toba ipo wazi kwako. Usipende kuwapa moyo watu watende dhambi kwa makusudi na kwa kurudia rudia kosa lilelile eti watarajie toba, hakuna neno hilo katika Kitabu.
Ni lazima tuseme ukweli kuwa toba ipo, lakini ina sharti zake. Kuna watu wanamichezo ya kipuuzi sana, mtu anaishi na kimada weee halafu mwezi wa Ramadhani ukifika tu anaoa au anafukuza, Ramadhani ikiisha tu anaachana na mke au anamrudisha tena yule kimada. Hiyo sio toba bali ni kubadili ratiba ya mlo.
Neno linasema hivi "enyi mlioamini, mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wacha MUNGU" (Quran...). Hivyo kwa neno hilo ike hoja yako ya Mwezi wa ramadhani ni kwa ajili ya toba pekee inafutwa. Lengo la funga ni kuja kuwa mcha MUNGU na kama uchamungu usipopatikana tafsiri nyepesi ni kuwa ulibadilisha ratiba ya mlo. Kuoga na kisha kujitumbukiza kwenye matope ni umbumbu kabisa, mtu yeyote mwenye akili anajua hili. Nakusihi tena, tusiwafariji watu kutenda dhambi kwa makusudi eti kwa vile Mwenyezi MUNGU anasamehe, kumbuka dhambi moja huzaa dhambi nyingine na tena na tena hadi mauti, ili ushinde ni lazima uvunje mnyororo wa dhambi, tushirikiane kukemea dhambi na kuwasihi watu wamrejee Mola wao.
 
Siku hizi dini ni biashara

Ntabaki kwenye dhehebu langu LA toka utotoni
Hata kama dhehebu lako ni kuabudu mbuzi?? Ndugu, Usiabudu katika dini au dhehebu bali Muabudu Mwenyezi MUNGU tu kama alivyoandikwa katika vitabu vyake. Fuata andiko linasema nini, sio dhehebu linasema nini.
Wanaofuata madhehebu na wachungaji ndio hawa wanaopotea. Ukweli juu ya Mwenyezi MUNGU upo kwenye maandiko sio madhehebu wala dini, watu wana dini zao na wana madhehebu yao lakini wanawanga usiku! Shika neno mkuu.
 
Makanisa mengi sasa hivi hasa ya Kilokole yapo kimaslahi zaidi
 
shida ni kumtegemea mtumishi akufanyie kitu au akuombee hata kwa jambo dogo tu, na wakati vingine unaweza ukalia na Mungu akakupa direct, Mungu anasema nawapenda wale wanipendao na wanitafutao kwa bidii wataniona, mithal 8:17, tungekuwa tunafanya juhudi ya kumtafuta MUNGU kwa bidii kama tutafutavyo pesa tungejua nabii yupi mkweli na yupi Muongo, lakini tumekua wavivu sana kumtafuta MUNGU, MUNGU anatafutwa. tumekua tunategemea watumishi kama wao ni Mungu. sitaki kusema huyo malisa kama ni nabii wa ukwel au uongo, MUNGU anajua yupo wapi kama ni wa ukwel au uongo, MUNGU atufungue macho ya rohoni.
 
Back
Top Bottom