Usanii wa nabii Malisa na miujiza feki

Usanii wa nabii Malisa na miujiza feki

Habari wakuu,

Jana wakati naangalia Star Tv kipindi cha mahuburi ya huyu jamaa Malisa nilishangazwa na jambo moja ambalo yeye analiita muujiza wa kuwaingizia watu pesa kwenye akaunti zao kama ni mpesa tigopesa au airtell money.

Sina shaka na uwezo wa kufikiri wa waumini wa makanisa ya miujiza kuwa ni mdogo ndio maana wanatapeliwa ila kinachonisikitisha ni huyu nabii kuhisi kuna wajinga hata nje ya kanisa lake anaweza kuwadanganya kwa miujiza feki ya kuwawekea watu kwenye pesa na kuna wajinga kama watatu walikimbilia mbele kwenda kushuhudia kuwa wamewekewa pesa na malaika kimiujiza ila hawakuonyesha ushahidi wowote katika kitu kinachoonyesha.

Ile hali ilikuwa staged maneno waliyokuwa wanaongea wale watu ni very identical, mwisho kabisa huyu nabii mwenye uwezo wa kuwawekea watu pesa kimiujiza yeye alikuwa anaomba achangiwe kwa mpesa na tigo pesa kwa namba alizokuwa anataja yaani muujiza haufanyi kazi kwake ila kwa waumini tu.

Amkeni wakristo wezangu tusiwe kondoo kwenye kila kitu.

Islaam is only solution !

Chungu na riziki.jpg
 
Mwakasege ni mwalimu anaejua kufundisha, Mimi ni mwislamu lakini huwa nasikiliza mafundisho ya Mwalimu Mwakasege kwa lengo la kukuza ufahamu. Kwa taarifa tu ni kuwa Mwakasege sio nabii bali ni Mwalimu na pia hana kanisa analomiliki. Yeye hupita sehemu mbalimbali kufundisha wala mafindisho yake kamwe hayalengi Sadaka! Ni wachache sana aina ya mwakasege
Aisee mngekua mnawajua kwa upande wa pili msingethubutu kuwapa ata cheo cha ualomu.
 
Mkuu kwahiyo sheikh Yahaya hakuwa sheikh? Unauhakika waislam kweli hawaendi huko kweli au unajisemea upande wako na baadhi ya unawafahamu. Nakushauri ufanye research ujiridhishe kwanza kabla hujakanusha andiko langu mkuu.
Sheikh maana yake nini? Waislamu sisi kwa sisi huitana sheikh hata kama hatuna weledi wa dini! Sidhani kama Sheikh ina maana yoyote katika dini, hilo neno wakati mwingine hutumika kama neno Mzee. Watu waliokuwa wanaenda kwa Mzee Yahaya nadhani wana majina ya kiarabu kama Vile Omar, Ramadhan n.k, lakini sidhani kama ni waislamu haswa wanaojua uislamu. Usichanganye jina la kiarabu na dini!!!! Kama kweli ni waislam walioamini basi walienda kwa mnajimu bila shaka wao walikuwa miongoni mwa walioasi. Kuna sehemu flani niliwakuta watu wanaombea watu wenye mashetani kwa kusoma sura za quran; Halafu mwishoni yakiwashinda kutoka wanaanza Tawile, tawile, tawile! Sitakuja kusahau, hili nilishudia mimi binafsi, watu wamevaa makanzu na kofia na wanaitana masheikh! Tangu hapo sitaki kusikia mtu yeyote ndani ya familia yangu anaenda kuombewa! Je unataka kuniambia hao niliowakuta hapo ni waislamu?? Mm kwangu hao ni waganga tu.
 
binafsi nilishaachana na wahubiri waongo kama hao .... miaka ya tisini kuna mhubiri alizunguka nchi nzima akitangaza mwisho wa dunia kuwa ni 2000, alisahau kuwa maandiko yanasema hata mwana wa Mungu haijui siku wala saa.
Uongo ukiufanyia 'promotion' huwa 'unafanana' na ukweli, ingawa bado unabakia kuwa uongo !
 
Aisee mngekua mnawajua kwa upande wa pili msingethubutu kuwapa ata cheo cha ualomu.
Hicho cheo sijampa mimi. Mwalimu kazi yake ni kufundisha, Mwakasege ndio kazi anayoifanya ulitaka nimwite Daktari mkuu?? Halafu kumsikiliza mtu haina maana unachukua kila analofundisha, kuna mengine unayaacha hapo hapo. Jifunze hekima, pumba unaziacha hapo hapo, na wala sijasema yupo sahihi au wrong, bali kuna mafundisho yake mengine ni mazuri sana bila kujali dini yako.
Halafu mimi nilishafunguliwa zamani sana kwenye mtego unaitwa dini au dhehebu, mimi ninamwamini Mwenyezi MUNGU muumba wa mbingu na nchi kwa kutii sheria zake, na sheria zake ni universal, kwenye quran utazikuta, kwenye biblia utazikuta, kwenye analects of Confuciuous utazikuta hata kwenye vitabu vya hindu utazikuta. Mwenyezi MUNGU anapenda utende haki kwa kila jambo! Utende lile ambalo ungependa utendewe! Thats all.
 
Imani ukiipa kipaumbele kiasi hicho, unaweza kuwa mtumwa wa imani hiyo. Wakristo wanapaswa waamke, wauepuke uovu huu uliopo ndani ya kisingizio cha imani
 
Mungine tunaye huku mahubiri yake asilimia 95 wanahudhuria wanawake. Nimeshindwa kuelewa kabisa!
 
Mkuu kwahiyo sheikh Yahaya hakuwa sheikh? Unauhakika waislam kweli hawaendi huko kweli au unajisemea upande wako na baadhi ya unawafahamu. Nakushauri ufanye research ujiridhishe kwanza kabla hujakanusha andiko langu mkuu.
Makele mbele Muislaam haendi kwa Sheikh Yahaya kupigiwa 'ramli' !
'Enyi mlio amini (Waislaam) ! Bila shaka ulevi, na kamari na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, (huo) ni uchafu na katika kazi za Shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa
Qur'an:5:90
 
Mungine tunaye huku mahubiri yake asilimia 95 wanahudhuria wanawake. Nimeshindwa kuelewa kabisa!
Kuna mmonya anaelezea bikira ! ........duuh anawaweka wanawake katika wakati mgumu kweli : Eti yule alye mbikiri ndiye kaweka naye agano. Na mambo mengine yakuchanga changanya hayan mbele wala nyuma !
 
Sheikh maana yake nini? Waislamu sisi kwa sisi huitana sheikh hata kama hatuna weledi wa dini! Sidhani kama Sheikh ina maana yoyote katika dini, hilo neno wakati mwingine hutumika kama neno Mzee. Watu waliokuwa wanaenda kwa Mzee Yahaya nadhani wana majina ya kiarabu kama Vile Omar, Ramadhan n.k, lakini sidhani kama ni waislamu haswa wanaojua uislamu. Usichanganye jina la kiarabu na dini!!!! Kama kweli ni waislam walioamini basi walienda kwa mnajimu bila shaka wao walikuwa miongoni mwa walioasi. Kuna sehemu flani niliwakuta watu wanaombea watu wenye mashetani kwa kusoma sura za quran; Halafu mwishoni yakiwashinda kutoka wanaanza Tawile, tawile, tawile! Sitakuja kusahau, hili nilishudia mimi binafsi, watu wamevaa makanzu na kofia na wanaitana masheikh! Tangu hapo sitaki kusikia mtu yeyote ndani ya familia yangu anaenda kuombewa! Je unataka kuniambia hao niliowakuta hapo ni waislamu?? Mm kwangu hao ni waganga tu.
Kwanini wasiwe waislam mkuu? Hao niwaislam kama ulivo wewe sematu wamepotoka nje ya uislam. Kwahiyo kwamaana hiyo kwaupeo wako wewe mtu aliyetoka kwenye misingi ya uislam kidogo hata kwa bahati mbaya, kwako wewe si muislamu? Ingekuwa nihivo basi hata kusingekuwa na ibada yatoba kama mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambapo kila muislam hutumia kipindi hicho kujikosoa na kumrudia mola wake.

Muislam atakuwa mwislam tu hata awe nadhambi au asiwe na dhambi. Zambi zake hazimuondolei uhalali wake katika dini yake, bali nikwa toba tu. Hata muumba anajua vema kwamba binadamu tu wadhaifu wakati mwingine tunamkosea sana. Ndomaana kwakujua hilo akatuwekea kipindi cha toba. Kamwe dhambi haimuondolei mja uislaam wake. Muislam ni mwislam tuu, awe nadhambi ama laa ilimradi ni muislam na anamwamini mtume.
 
Mwakasege ni mwalimu anaejua kufundisha, Mimi ni mwislamu lakini huwa nasikiliza mafundisho ya Mwalimu Mwakasege kwa lengo la kukuza ufahamu. Kwa taarifa tu ni kuwa Mwakasege sio nabii bali ni Mwalimu na pia hana kanisa analomiliki. Yeye hupita sehemu mbalimbali kufundisha wala mafindisho yake kamwe hayalengi Sadaka! Ni wachache sana aina ya mwakasege
Utakuwa Muislaam mjinga !
Dini ya haki.png
 
Kwanini wasiwe waislam mkuu? Hao niwaislam kama ulivo wewe sematu wamepotoka nje ya uislam. Kwahiyo kwamaana hiyo kwaupeo wako wewe mtu aliyetoka kwenye misingi ya uislam kidogo hata kwa bahati mbaya, kwako wewe si muislamu? Ingekuwa nihivo basi hata kusingekuwa na ibada yatoba kama mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambapo kila muislam hutumia kipindi hicho kujikosoa na kumrudia mola wake.

Muislam atakuwa mwislam tu hata awe nadhambi au asiwe na dhambi. Zambi zake hazimuondolei uhalali wake katika dini yake, bali nikwa toba tu. Hata muumba anajua vema kwamba binadamu tu wadhaifu wakati mwingine tunamkosea sana. Ndomaana kwakujua hilo akatuwekea kipindi cha toba. Kamwe dhambi haimuondolei mja uislaam wake. Muislam ni mwislam tuu, awe nadhambi ama laa ilimradi ni muislam na anamwamini mtume.
Sitaki kukupinga mkuu, umenena haki. Nafikiri ni waislam waliopotoka. Sina hakika sana juu ya suala la kuamini bila matendo hukumu yake ni ipi.
 
Makele mbele Muislaam haendi kwa Sheikh Yahaya kupigiwa 'ramli' !
'Enyi mlio amini (Waislaam) ! Bila shaka ulevi, na kamari na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, (huo) ni uchafu na katika kazi za Shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa
Qur'an:5:90
Kwahiyo Bandiwe, muislaam aliyepotoka akaenda huko kwa sheikh yahaya ama kunako ramli kwingineko, atakuwa siyo muislaam tena? Navipi katika toba? Toba maanake ni nini? Mi naamini binadamu yeyote hukosea. Na baada yakukosea anafanya toba. Ila dini yake inakuwa palepale.
 
Utakuwa Muislaam mjinga !
View attachment 346003
Ww ni mjinga zaidi. Aya ya kwanza kushuka katika uislam inaanza na neno " soma.." . Hivi kila mtu akisema asisome dini ya mwenzake au asisikilize mahubiri ya dini nyingine hivi kutakuwa na wislamu wapya kweli?? Unawapata waislamu wapya kwasababu wamekubali kusoma na kusikiliza dini yako na wakiona kuwa ni ya haki wanaifuata, kama wao wanakusikiliza kwanini ww usiwasikilize!! Ww ni kipofu!
Soma na sikiliza upate maarifa ww. Unaonekana bado mtoto au umekuwa brainwashed kihusu suala la dini. Ww ni jamii ya wale ambao wakimuona nguruwe wanamlaani au wanamuua bila kujua kuwa nguruwe aliumbwa kwa kusudi maalumu na ana kazi maalumu na akiwa na njaa unapaswa kumpa chakula na akiwa na kiu unapaswa kumsaidia maji. Weledi wako umeishia kwenye kuimba aya za quran kwa kiarabu bila hata kuelewa maana au kutafakari maneno.
 
Sitaki kukupinga mkuu, umenena haki. Nafikiri ni waislam waliopotoka. Sina hakika sana juu ya suala la kuamini bila matendo hukumu yake ni ipi.
Hiyo hata yeye mwenyewe mola wetu anajua kwamba sie tu wadhaifu ndomaana akatuwekea toba. Kibaya nikutotubu mala baada yakujitambua kwamba nilichofanya nikinyume na mapenzi ya Allah. Kwahiyo watu wa ainahiyo nikuwaombea wakumbuke toba na si kuwahukumu kana kwamba sisi hatuna kosa lolote tulowahi kulitenda la kumuudhi Allah.
 
Kinachowafanya Watu Watapeliwe Ni Imani Zao Jamani, Wameruhusu Imani Izidi Utashi.
Lakn Pia Kwa Upande Wa Waislam Wapo Pia Ambao Wanatabiri Nyota Yako Kwa Kutumia Njia Mbali Mbali Ikiwemo Quran, Mfano Mtoto Wa Shekh Yahya, So Haya Ni Mambo Yalogawanyika Tu. Hawa Wanafanyia Kwny Ofisi Zao Kanisani Na Wale Wanafanyia Kwny Ofis Zao Nyumbani Au Kwingineko.
Kuna vitu unachanganya mkuu,Uislamu kama dini hautumiki kufanya utabiri nnachomaanisha ni kuwa kwenye Quran hakuna mafunzo ya kutabiri chochote.Quran haitoi mafunzo hayo na pia uislamu unakemea sana haya mambo,sababu kujua mambo yajayo(ilm ghaib) kama inavyoitwa kwenye quran ni elimu ambayo anayo mwenyezi mungu peke yake.na wanaofanya utabiri mara nyingi huwa wanatumia majini(against islamic teachings) na majini(pepo wabaya) wana sifa ya uongo ndio maana hakuna utabiri 100% ukweli.sheikh yahya na mwanawe sio mifano mizuri ya waislamu na hawako kwenye njia ya kiislamu,na hawakubaliki kwenye waislamu wajuao hata kama wanatabiri na kuandika kiarabu kwenye mambo yao.kiarabu na Qurani vinafanana ki lugha lakini ni vitu viwili tofauti.
Ova!
 
Hiyo hata yeye mwenyewe mola wetu anajua kwamba sie tu wadhaifu ndomaana akatuwekea toba. Kibaya nikutotubu mala baada yakujitambua kwamba nilichofanya nikinyume na mapenzi ya Allah. Kwahiyo watu wa ainahiyo nikuwaombea wakumbuke toba na si kuwahukumu kana kwamba sisi hatuna kosa lolote tulowahi kulitenda la kumuudhi Allah.
Umenena vyema chief. Nakushukuru kwa kunituelewesha kwa ujumla. Mtume anasema Dini ni Kunasihiana; hivyo tunapaswa kuwanasihi tunaowaona wanaenda kinyume na Mwenyezi MUNGU anavotaka. Yeyote atakayesoma post yangu ile atarekebishwa kidogo na post yako kwa yale niliyomwenda too extreme maana hata Mwenyezi MUNGU mwenyewe anasema tusiwafungie watu wasione rehema zake. Shukran.
 
Kuna vitu unachanganya mkuu,Uislamu kama dini hautumiki kufanya utabiri nnachomaanisha ni kuwa kwenye Quran hakuna mafunzo ya kutabiri chochote.Quran haitoi mafunzo hayo na pia uislamu unakemea sana haya mambo,sababu kujua mambo yajayo(ilm ghaib) kama inavyoitwa kwenye quran ni elimu ambayo anayo mwenyezi mungu peke yake.na wanaofanya utabiri mara nyingi huwa wanatumia majini(against islamic teachings) na majini(pepo wabaya) wana sifa ya uongo ndio maana hakuna utabiri 100% ukweli.sheikh yahya na mwanawe sio mifano mizuri ya waislamu na hawako kwenye njia ya kiislamu,na hawakubaliki kwenye waislamu wajuao hata kama wanatabiri na kuandika kiarabu kwenye mambo yao.kiarabu na Qurani vinafanana ki lugha lakini ni vitu viwili tofauti.
Ova!
Mkuu Nakuelewa Sana, Nilikuwa Namaanisha Dini Zote Hizi Hutmika Vibaya Kwa Mlengo Wa Kupiga Pesa Lakn Kwa Njia Tofauti.

Sote Tunatoka Mwenge Uelekeo Kariakoo Lakn Tukifika Bamaga Mmoja Anapitia Shekilango Mwingine Ananyoshea Moroco
 
Kuna mmonya anaelezea bikira ! ........duuh anawaweka wanawake katika wakati mgumu kweli : Eti yule alye mbikiri ndiye kaweka naye agano. Na mambo mengine yakuchanga changanya hayan mbele wala nyuma !
Je, kuvunja bikra nje ya ndoa ni haki?? Nafikiri fundisho lake linafocus watu wasivunje bikra zao kabla ya ndoa, sidhani kama huo ni ubaya. Huenda pia hujui agano maana yake nini. Si kila kitu cha kupinga mkuu. Soma upate maarifa.
 
Umenena vyema chief. Nakushukuru kwa kunituelewesha kwa ujumla. Mtume anasema Dini ni Kunasihiana; hivyo tunapaswa kuwanasihi tunaowaona wanaenda kinyume na Mwenyezi MUNGU anavotaka. Yeyote atakayesoma post yangu ile atarekebishwa kidogo na post yako kwa yale niliyomwenda too extreme maana hata Mwenyezi MUNGU mwenyewe anasema tusiwafungie watu wasione rehema zake. Shukran.
Naam mkuu. Kujisahihisha ama kusahihishana nijukumu letu sisi waja. Maana hakuna aliyemkamilifu mbele zake mwenyezi mungu.
 
Back
Top Bottom