Usanii wa Clouds: Mshindi wa Brazuka akataa ushindi wa kwenda brazil

mie ndo maana hii media huwa siikilizagi sana radio ya boss akisema tu wote mnafuata sasa hapa naona ipoo kwa ajili ya bosi na sio sisi jamii
 
Tunapenda kulalamika sana, sasa ajabu yao ni nini? Terms and conditions lazima zizingatiwe.

Terms and conditions zipi? Unazijua sheria za michezo ya bahati na sibu au unaongea tu!!!!

Nenda pale Tanzania Gambling Board,ukapate shule kidogo!!

Kama huyo amekataa wangemtafuta mtu mwingine!!

Voda,Airtel wakiweka mchezo wa bahati na sibu,wakikupigia ukawa off air,au hupokei simu wanampigia mwingine!!

Kwa nini wasiseme mshindi kapigiwa simu hakupatikana hewani au hakupokea simu??

Na sheria ya Tanzania Gambling Board ndo inavyosema!!!
 
Brazuka kwani ni promotion ya clouds au Ya cocacola?
Na kama mtu kakataa kwenda Brazil anauguliwa na wazazi utapeli wa clouds upo wapi hapo??
 
Brazuka kwani ni promotion ya clouds au Ya cocacola?
Na kama mtu kakataa kwenda Brazil anauguliwa na wazazi utapeli wa clouds upo wapi hapo??
Brazuka ni tofauti na ile promosheni ya coca cola. Kwa kuwa wamesema mshindi lazima apatikane, wangetafuta mshindi mwingine kwani walioshiriki ni wengi. Huyo kwa kuwa kashinda na anauguliwa eti shindani ndio linaishia hapo, huo kama sio utapeli ni nini?
 
kwa nijuavyo mimi lazma shindano lolote kama hilo gambling board lazima ipitishe na kusimamia. in that case board inabidi itoe maelezo kwa kina lasi ivyo huu ni utapeli. utapeli wa waziwazi
 
Watanzania tunalalamika kweli. Mtu kapigiwa simu kasema anauguliwa hawezi enda. Final clouds sio wajinga kupanga mtu afu awakatae
 
tena wakamwambia {dj fetty}basi wamuonnee huruma wampe tishet 2 huyo mshindi...nikachoka kabisaaaa!!!
 
Pia lile shindano la ubunifu wa nembo ya Taifa (miaka 50 ya Muungano wa Tz) waliahidi milioni 1 kwa mshindi. Sijui ni mimi tu sikusikia mshindi akitangazwa, maana lilipotea ghafla.

Kwanza hata mimi sijaelewa mshindi alitangazwa lini hawajamaa ninoma vipindi vya tv yao hata havidumu.iko wapi ile series.
 
kwanini wasingerudia kuchezesha hiyo bahati nasibu ili apatikane mwingine!
 
tena wakamwambia {dj fetty}basi wamuonnee huruma wampe tishet 2 huyo mshindi...nikachoka kabisaaaa!!!

Hahahahaha duh nmeipenda hyo, haka karedio ukisikiliza muda wa stress unaweza vunja home theater yako sio ishu kabisa huu mpango
 
Ahahahaaa clous ni janga jamani nakumbuka bonanza lao la mbeya makampuni yalioshiriki yalitoa ml 2 yalikuwa nane which means ml 16 walipata mengine yalitoka sumbawanga lakini nishindi wa kwanza jamaa wakatoa kikombe chenye thamani ya elfu hamsini mpaka sumbawanga veterani wakaondoka kwa hasira ahahahaaa hawa jamaa wahuni sana
 
Brazuka kwani ni promotion ya clouds au Ya cocacola?
Na kama mtu kakataa kwenda Brazil anauguliwa na wazazi utapeli wa clouds upo wapi hapo??

kumtoa mtu ndani ya gereza ni rahisi tofauti ng kulitoa gereza ndani ya mtu. hebu fikiri nje ya box mkuu.
 
Back
Top Bottom